Kilimo kinalipa kama ukikifanya kama kazi

Kilimo kinalipa kama ukikifanya kama kazi

Natoa ushuhuda wangu wa kilimo cha mahindi nilichofanya msimu wa 2022

Niliandaa shamba ekari 3 kwa tsh 180,000.

Nilinunua mbegu aina ya Dk mifuko 7 ya kilo 2 kwa garama ya tsh 91,000.

Gharama za kupandà ni tsh 60,000.

Palizi 180,000.

Jumla ya garama zote ni tsh 511,000.

Mavuno niliyopata ni gunia 22.

Bei ya gunia moja kwa sasa ni elfu 95.

Siwezi kuuza sasa hivi kwa sasa nitayahifadhi mpaka mwaķani mwezi wa pili.

NB: Mbegu zimeìngia chache sababu shamba lina mazao mengine kama michungwa, minazi na miģomba
Vijana tuacheni kulalamika kilimo kinalipa ukiwa makini
Kilimo.siku zote ni msala unless ufanye kilimo Cha Mkataba..

Jana tuu nimeona kwenye tv jinsi wakulima wa zabibu wanalalamika hakuna pa kupeleka zabibu yaani hakuna soko.
 
Kilimo cha umwagiliaji kinalipa, cha mvua ni bahati nasibu.

Halafu unatakiwa uwe na usimamizi mzuri, madawa na mfumo wa uhifadhi mazao
Hv wapi ni sehemu nzur na mahsus kwa kilimo cha mahindi kwa umwagiliaji, na je naweza pata shamba? hata Kama ni nje na hapa nnapo ishi" nko morogoro mjini hapa[emoji120]
 
Wakuu ni mbegu gani ya mahindi inafaa kwenye ardhi ya kichanga
 
Mshukuru Mungu umevuna kipindi ambacho mahindi yapo bei nzuri. Ungekutana na bei ya gunia elf 30 mpaka 40 ndo ungefahamu kama kilimo kinalipa kweli au ni story tu.
Kwani hata katika biashara kila siku mtu anapata faida ya kuridhisha? Chochote unachokifanya hakiwezi kukulipa 100% kila mwaka

Kilimo kinalipa sawa na biashara nyingine tu ukiwa serious

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Hv wapi ni sehemu nzur na mahsus kwa kilimo cha mahindi kwa umwagiliaji, na je naweza pata shamba? hata Kama ni nje na hapa nnapo ishi" nko morogoro mjini hapa[emoji120]
Nenda Handeni kwasunga mashamba yapo kibao ekari moja unapata 300k

Ardhi ya kule ina rutuba sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zipo za kununua ,laki na nusu kwa eka ,handeni,miono chalinze laki mbili kwa eka.pia za kukodi zipo ruvu kitonga pembeni ya mto msumbiji,laki kwa eka ,maji muda wote
Mkuu naomba connection ya mashamba ya kukodi hapo ruvu chief
 
Unaposema kilimo hakilipi jifikirie unasema hivyo ukiwa umeshiba au una njaa, usifananishe kilimo na kazi za kuajiriwa ambapo utaiba, utaenda semina na kula rushwa.
 
Kilimo.siku zote ni msala unless ufanye kilimo Cha Mkataba..

Jana tuu nimeona kwenye tv jinsi wakulima wa zabibu wanalalamika hakuna pa kupeleka zabibu yaani hakuna soko.
Nipe mawasiliano yao, hakuna soko la zabibu kivipi yaani?!
 
Mshukuru Mungu umevuna kipindi ambacho mahindi yapo bei nzuri. Ungekutana na bei ya gunia elf 30 mpaka 40 ndo ungefahamu kama kilimo kinalipa kweli au ni story tu.
Hahaa acha uoga ukiamua kufanya fanya tuu utafaidika ila faida ni kubwa zaidi kama utafanya kilimo cha umwagiliaji
 
Natoa ushuhuda wangu wa kilimo cha mahindi nilichofanya msimu wa 2022

Niliandaa shamba ekari 3 kwa tsh 180,000.

Nilinunua mbegu aina ya Dk mifuko 7 ya kilo 2 kwa garama ya tsh 91,000.

Gharama za kupandà ni tsh 60,000.

Palizi 180,000.

Jumla ya garama zote ni tsh 511,000.

Mavuno niliyopata ni gunia 22.

Bei ya gunia moja kwa sasa ni elfu 95.

Siwezi kuuza sasa hivi kwa sasa nitayahifadhi mpaka mwaķani mwezi wa pili.

NB: Mbegu zimeìngia chache sababu shamba lina mazao mengine kama michungwa, minazi na miģomba
Vijana tuacheni kulalamika kilimo kinalipa ukiwa makini
We mzee mwezi wapili ndo huu soko linasema sh ngapi??? Pia tupe na Gharama ulizohifadhia, usafiri nk
 
Yaani ikifika mwakani mwezi wa tatu au wa nne naamini nitapata mtajì wa kulimia na wa biashara, naamini gunia moja la mahindi si chini ya 150000
Mkuu utakuwa unajidanganya, mwezi wa 3 na 4 maeneo ya kanda ya ziwa huwa wameanza kuvuna, hivyo mahindi hayawezi kufika 150k kwa gunia!
 
Back
Top Bottom