Kilimo kinalipa kama ukikifanya kama kazi

Kilimo kinalipa kama ukikifanya kama kazi

Mshukuru Mungu umevuna kipindi ambacho mahindi yapo bei nzuri. Ungekutana na bei ya gunia elf 30 mpaka 40 ndo ungefahamu kama kilimo kinalipa kweli au ni story tu.
Kuna sehemu mwaka 2018 mahindi debe buku 3

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Mshukuru Mungu umevuna kipindi ambacho mahindi yapo bei nzuri. Ungekutana na bei ya gunia elf 30 mpaka 40 ndo ungefahamu kama kilimo kinalipa kweli au ni story tu.
kwa Sasa sio rahisi mahindi kununuliwa 40 au 30
 
Kweli.. kabisa, mimi niliogopa kulima mahindi nikaamua kupanda viaz na mihogo kulinda shamba, dalali kanipigia simu anataka viazi lishe kwa 800/kg...

Nimeamua kuwa serious na kuacha uvivu pia kuweka degree pembeni...
Mkuu vipi naweza kupata mawasiliano yako zaidi
 
Natoa ushuhuda wangu wa kilimo cha mahindi nilichofanya msimu wa 2022

Niliandaa shamba ekari 3 kwa tsh 180,000.

Nilinunua mbegu aina ya Dk mifuko 7 ya kilo 2 kwa garama ya tsh 91,000.

Gharama za kupandà ni tsh 60,000.

Palizi 180,000.

Jumla ya garama zote ni tsh 511,000.

Mavuno niliyopata ni gunia 22.

Bei ya gunia moja kwa sasa ni elfu 95.

Siwezi kuuza sasa hivi kwa sasa nitayahifadhi mpaka mwaķani mwezi wa pili.

NB:
Mbegu zimeìngia chache sababu shamba lina mazao mengine kama michungwa, minazi na miģomba
Vijana tuacheni kulalamika kilimo kinalipa ukiwa makini
Una lengo la kugusa jamii kwa kumotivate ila bado.
Kwa ekari moja ni mifuko 4 mpaka 5.5 kwa space aidha ya 30cm kwa 75cm au 45cm kwa 90cm.

The rest ukianza mifuko 7 ekari tatu plus mavuno gunia 22 hapana kubwa sana. Wastani kwa ekari umekosa ni gunia 15. Mwisho mqnagerial practices haikuwa sawa
 
Mahindi na kipunga bei imeporomoka. 2024 kutakuwa na mpunga aka Michele ya kufa mtu. Kilo tunaidakia sh 1000
 
Una lengo la kugusa jamii kwa kumotivate ila bado.
Kwa ekari moja ni mifuko 4 mpaka 5.5 kwa space aidha ya 30cm kwa 75cm au 45cm kwa 90cm.

The rest ukianza mifuko 7 ekari tatu plus mavuno gunia 22 hapana kubwa sana. Wastani kwa ekari umekosa ni gunia 15. Mwisho mqnagerial practices haikuwa sawa
Utakuwa hujasoma mpaka mwisho. Mbona kaelezea kwanini mbegu zimeingia chache?
 
Natoa ushuhuda wangu wa kilimo cha mahindi nilichofanya msimu wa 2022

Niliandaa shamba ekari 3 kwa tsh 180,000.

Nilinunua mbegu aina ya Dk mifuko 7 ya kilo 2 kwa garama ya tsh 91,000.

Gharama za kupandà ni tsh 60,000.

Palizi 180,000.

Jumla ya garama zote ni tsh 511,000.

Mavuno niliyopata ni gunia 22.

Bei ya gunia moja kwa sasa ni elfu 95.

Siwezi kuuza sasa hivi kwa sasa nitayahifadhi mpaka mwaķani mwezi wa pili.

NB: Mbegu zimeìngia chache sababu shamba lina mazao mengine kama michungwa, minazi na miģomba
Vijana tuacheni kulalamika kilimo kinalipa ukiwa makini
Duuh hekari 3 kumbe unapat gunia 22😥
 
Duuh hekari 3 kumbe unapat gunia 22😥
Inategemea mm kuna jamaa tumechanga tukalima ila huduma tuliweka kwa kiwango stahiki na tumevuna kipande cha heka kama mbili pekee kwanza Ila kimetoa karibu gunia 50
 
Wanasema Kilimo Cha Umwagiliaji Kinalipa, Je Ni Maeneo Gani Ambayo Unaweza Kufanya Kilimo Cha Umwagiliaji. Na Serikali Yetu Inazuia Kufanya Shughuli Za Kilimo Kwenye Vyanzo Vya Maji?
 
Back
Top Bottom