Kilimo kinalipa kama ukikifanya kama kazi

Labda vuli isinyeshe, mvua za vuli zikinyesha, mwezi pili watu wanavuna na bei inaporomoka ghafla.
Sio mikoa yote inayolima vuli, kumbuka mwaka huu karibia maeneo yote ya nchi mvua zilikua hafifu
 
Sema mwaka huu wakulima wa mahindi wanachekelea. Miaka mingine kwa hayo mavuno ungeishia kupata laki 7 au 8 ambayo ni sawa na bureee.
 

kaka kilimo chako unakifanyia wapi?
 
Nina ekari kumi zangu ila sijaona manufaa ya kilimo..nip3ni maarifa mkuu
cha msingi elewa kila shughuli hapa duniani inalipa kulingana na wakati wake. wakulima wa mahindi msimu huu wanajinasibu kwa sababu ya hali ya hewa ilikuwa mbovu na wengi wameangukia pua kwenye mahindi, wachache waliotoboa ndio wanatusisimua hapa kuwa kilimo cha mahindi kinalipa.

"Usiingie shambani kwa kusisimuliwa na shuhuda za watu". Ingia shambani kwa sababu umejiandaa kukutana na hali zote mkuu
 
Mshukuru Mungu umevuna kipindi ambacho mahindi yapo bei nzuri. Ungekutana na bei ya gunia elf 30 mpaka 40 ndo ungefahamu kama kilimo kinalipa kweli au ni story tu.
Hakuna nyakati gunia lingeuzwa kwa bei ya 30 au 40 kwa miaka 10 nyumaila serikali ndio ilikuwa inawaminya wakulima kwa kufunga mipaka kwa kigezo cha kuepusha taifa na njaa ikimnufaisha mfanyakazi,biashara, bila kujali mkulima nguvu,muda na gharama anayotumia kwa msimamo wa Sasa wa serikali hata vijijini tutaanza kuona nyumba za bati na wale wa mijini waidai serikali ongezeko ktk kile walichokuwa wanamdhurumu mkulima ili kubalance maisha.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kwa heka moja kwa makadirio yako alitakiwa apate gunia ngapi mkuu? Tupe uzoefu wako mkuu.
nakazia tu ekari moja huwa ni around 13 up 18 hili ni kadirio kwa mkulima mzoefu gunia 22 ekar tatu daah hapana aise maana yake kalma ekar moja na nusu
 
kweli mkuu aingie uwanja wa vita akutane na hali halisi kilimo kina changamoto asikuambie mtu,naongea kama shahidi kwa yaliyo nikuta mwaka huu ekar nne cjavuna

ekari 4 kukodi 100000 *4=40 0000
kulima na trekta kila ekar 45000

mbegu mifuko 12 kila mfuko 12000elfu

palizi kwa kila ekar elfu 44000


bado dawa na dharura mkuu shkuru umepata hcho kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…