Kilimo ni biashara pekee inayolipa kwa 100%

Kilimo kinalipa wadau mmsikate tamaa tatizo watu wanakataga tamaa mapema hakuna kisichokuwa na changamoto
 

Kuweni makini kuna watu sio wa kweli hata Kama Ni rafiki yako. Ekari moja ya kitunguu itoe gunia 113?!! Na bei ya shambani 90,000!! Usije kuja kuwa disappointed. Mwambie aseme ukweli maana kuna watu hawataki kuonekana kuwa wamepata hasara
 
Kuweni makini kuna watu sio wa kweli hata Kama Ni rafiki yako. Ekari moja ya kitunguu itoe gunia 113?!! Na bei ya shambani 90,000!! Usije kuja kuwa disappointed. Mwambie aseme ukweli maana kuna watu hawataki kuonekana kuwa wamepata hasara
Asingeweza kunidanganya. Maana pia alinipa ushauri zaidi.
 

Mahindi wewe ulitumia mbegu zipi?
ulinunua wapi hizo mbegu?
 
Mkuu hiyo mbegu ina sifa zipi? Ntaipataje mm niko dar.
Best Mbegu hainunuliwi ivyo utaumia,
Kila mbegu hufaa mazingira fulani (hali ya hewa)
Mfano pale mbeya kila eneo hufaa mbegu tofauti kwakuwa kunamaeneo yana baridi kali kuliko mengine.

Pia kuna suala la mvua
Kuna mbegu inamudu mvua nyingi wakat nyingine mahindi huoza mvua ikizidi (kwakuwa Mhindi hauinami ili maji yatereze)
So naamini kama wewe inalima pwani jiridhishe kuona hali ya hewa inafanana na ya kule alikolima yeye
 
Mwenye Enzi Mungu atutangulie!
 
Complications mnazoweka kwenye kikimo zimewageuza waoga
Danganya walioko mjini! Najua yes kilimo sometime kinayo faida lakin sio hii uliyoiweka kwenye keyboard
 
Binafsi sishangai ekari moja kutoa gunia 37. Majuzi hapa nilikuwa ninaangalia Star TV walikuwa wanarusha mahojiano na watafiti wa kituo cha utafiti Arusha, wakawa wanatambulisha mbegu ya mahindi aina ya "wema" na nyingine inaitwa "star" wakaeleza ina uwezo wa kutoa gunia 80 kwa ekari(sio hekta) na wakasema zinavumilia hali ya ukame na ikitokea uhaba mkubwa wa mvua MTU aliyelima vizuri hawezi kukosa gunia 40.

Wakati nashangaa nikawaza ni-google mbegu aina ya wema ili kujua kuna wakulima washaitumia? Nikakuta shuhuda ya MTU mmoja tanga anajiita mkulima bora mkoa wa tanga, akieleza namna mbegu hiyo ya wema ilivyomtoa na ameitumia zaidi ya miaka 4 na hupata wastani wa gunia 37 hadi 45 kwa ekari.

Mdau hongera sana! Na endelea!

Mnaoombea msimu ujao aje na kilio mtabakia hivyo hivyo. Kitendo cha kukwambia amelima kwa kutumia ngombe zake ni ushuhuda ni mkulima na mfugaji mzoefu! Hivyo sio msimu wake wa kwanza, amependa tu kushare matokeo makubwa ya mbegu mpya ya mahindi aina ya DK!
 
We endelea na utafiti wako bro.
Nimemaliza chuo kikuu with a 4.7 GPA nikiwa overall best student, nikaamua kuingia kwenye kilimo na ufugaji kwa kuanzia na sh Laki saba, ndani ya miaka hii mitatu now nazungumzia mgahawa, shamba la mifugo na assets zinazo kimbilia mil 15...
Kinacho maliza wasomi ni hayo ma theory yenu...
Komaa tu na notes bro
 
Hakika huyu bwana ni mzoefu, na kwa maelezo yake inaonesha kabisa huu msimu emegonga extreme output toka kuanza hivyo amepata NGUVU ya kushare hapa
ushauri kwa mtoa mada napenda aelezee upande wa pili bila kuficha changamoto alizokutana nazo mbali na mafanikio hayo aliyobahatika nayo. nasema ni bahati kwa sababu mie nimekulia familia ya kulima.
 
Yes sio mtoa mada atoe positive side pia aseme kuna changamoto gan ili MTU aweze kujipanga vyema
 

Acha fix kilimo kwa nchi yetu kina changamoto nyingi kuanzia shambani hadi sokoni,tena huko sokoni ni kikwazo utawakuta madalali wana vitambi kupitia migongo ya wakulima acha kabisa ndugu,ukitaka kilimo sharti ujipange na kilimo kinacholipa ni cha kisasa na niliazima uwe na mtaji vinginevyo utaambulia patupu.
Watu wanang'ang'ania ajira ni kwa sababu hawana starting point ambayo ni mtaji!
Ni hayo tu....Asante kwa kusoma
 
Ushauri wako ni mzuri na wewe unafaa uigwe na kila kijana mtanzania mwenye akili. Wewe Sio kama wale vijana wanaoshinda humu eti wanapiga kura kuhusu uhalali wa kanisa la Gwajima!

Nakuunga mkono kijana mwenzangu
 
Ndugu ni kweli kwamba kilimo kina changamoto nyingi ikiwemo hizo ulizozitaja lakini kwa mtu anaeanza maisha kilimo ni njia nzuri ya kupata mtaji, usiogope changamoto zitumie kama fursa.
 
Safi sana mkuu, vijana wamejikalia mjini wakati mali ipo shambani.

Mimi nawashauri vijana wasijidanganye kwenda shambani ni bora wabaki mjini wakiwa wanabeti kuliko kufuata hizi porojo za huku mitandaoni. Hivi kilimo kingekuwa kinalipa leo tungewaona wakulima wakiwa wamechoka kiwango kile? Mbona hata hao mabwana shamba wenyewe hawawekezi kwenye kilimo? Kuliko kwenda kulima ni bora uajiriwe kazi ya ulinzi huko kwa wahindi. Ukitaka kuwa masikini nchi hii danganywa ukalime.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…