Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Dear Mama Samia,
Pole na majukumu ya kulitumikia taifa letu. Kwa heshima na taadhima, naomba kukufikishia kilio cha askari kadhaa wa Jeshi la Polisi ambao wamehamishwa hivi karibuni lakini bila kupewa senti tano ya uhamisho.
Kwa upande mmoja, uhamisho huo wa ghafla na usio na posho za uhamisho umeziacha familia za maafande hao katika wakati mgumu kwa sababu hawana hela za kuziachia familia zao, na kwa upande mwingine, hawawezi kuondoka na familia zao kwani hata huko walikohamishiwa, hali ni mbaya kimakazi na kimaisha.
Kwa mujibu wa taarifa, IGP Camillus Wambura amekuwa na vikao kazi mikoa ya Kaskazini kuanzia majuzi ambapo alikuwa Tanga na baadaye Arusha ambapo baada ya kukagua gwaride alikuwa na kikao na maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbali mbali.
Katika vikao hivyo ameongelea suala la askari waliohamishwa bila kulipwa posho za uhamisho. Lakini badala ya kutafutia ufumbuzi suala hilo, IGP Wambura amewakaripia vikali askari wake kwamba wamekimbilia kulalamika kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kadhia hiyo.
Dear Mama, kilichopelekea askari hao kuomba msaada nje ya utaratibu ni kutokana na vilio vyao kupuuzwa katika ngazi zote za uongozi wa jeshi hilo. Kadhalika, lengo la askari hao lilikuwa kufikisha kilio chao wewe Mama ambaye sio tu ni kama mzazi wao bali pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.
IGP Wambura aliwaeleza askari hao kwamba kamahakuna skari atakayelipwa posho za uhamisho, na kama askari yeyote miongoni mwa hao waliohamishwa atashindwa kuripoti kituo kipya akisubiria kulipwa asubiri kuona kitakachomkuta.
Dar Mama Samia, kwa mujibu wa taarifa, ni wiki ya pili hii sasa suala la posho za uhamisho wa askari hao limekuwa halizungumzwi kabisa japokuwa taratibu na kanuni za uhamisho zinaeleza bayana kuwa askari atakayehamishwa atalipwa posho ya uhamisho.
Askari waliohamishwa wanaishi maisha magumu huko walikohamishiwa ilhali hawajui hali ya familia zao zikoje kwani walitakiwa kuripoti vituo vipya vya kazi bila kupewa fedha zozote za kuachia familia zao/kuwasaidia katika mchakato wa uhamisho.
Kauli za vitisho za IGP ambaye alitarajiwa kulipatia ufumbuzi suala hilo, limeathiri morali wa askari husika.
Dear Mama Samia, kazi ya askari inahusisha kubeba silaha katika utekelezaji wa majukumu yao mbalimbali. Kwa hali ya maisha wanayoishi huku wakizongwa na hali ngumu ya familia zao, yayumkinika kuhisi kuwa inahatarisha usalama wao na wa raia pia kwa sababu ya msongo wa mawazo unaowakabili.
Dear Mama Samia, huenda IGP Wambura akachukua hatua kali dhidi ya askari husika lakini hadi wao kufikia hatua ya kuwasilisha kilio chao kwa njia zilizo nje ya utaratibu kumetokana na viongozi wao chini ya IGP Wambura kupuuzia stahili za askari hao katika mchakato huo wa uhamisho.
Mwisho, Dear Mama Samia, kunradhi endapo kukufikishia ujumbe huu kwa njia hii ni kukukosea heshima. Kwangu, sio rahisi kufikisha kilio cha polisi hasa kwa kuzingatia matukio ya hivi karibuni huko Mbeya, lakini kama mtetezi wa haki, natambua kuwa haki haibagui. Haki za askari waliohamishwa zina umuhimu kama zilivyo haki za Watanzania wengine.