SoC03 Kilio cha vibarua viwandani

SoC03 Kilio cha vibarua viwandani

Stories of Change - 2023 Competition

Euphra

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2023
Posts
522
Reaction score
1,082
Salaam wakuu naomba niende moja kwa moja kwenye mada, jamani hili linaloendelea viwandani linanihuzunisha, hivi ni kweli haya malalamiko hayawafikii viongozi wanaohusika? Au wananyamaza kwa lengo maalum? na ni lengo gani hasa yaani maswali ni mengi kuliko majibu,

Inafahamika wazi kabisa kwamba vibarua viwandani wanateseka sana jamani hivi ni kweli hamna watetezi kabisa au wanaogopa kuongea kuhofia kupoteza vibarua vyao au hawajui ni wapi wanastahili kupeleka malalamiko yao au ni hii nidhamu ya uoga tuliyonayo waTanzania wengi? Kwa maana wakati mwingine wanaotumia kuwakandamiza wenzao ni weusi wenzao waliopewa jukumu la kuwasimamia.

Inasikitisha mtanzania mzawa anafanyishwa kazi ngumu kwa masaa zaidi ya kumi na mbili bila utaratibu maalum kwa malipo chini ya elfu tano wakati mwingine na usipofikisha lengo lao la siku haulipwi kabisa hiyo pesa unabaki kuwafanyia kazi bure huku wakikusistiza kesho ujitahidi ili kufikia lengo upate kulipwa kwahiyo mtu anajikuta amelaliza siku nzima bure na hayo yote yanaambatana na lugha zisizofaa masimango na mfano wake jumlisha mazingira magumu ya kazi yanayohatarisha afya zao.. hapa hata itokee umeumia kazini hawatohusika na lolote

Naongea haya kwa ushahidi na wala si kwa kusimuliwa jaribu kupitia viwandani huko mbagara ujionee mwenyewe, kuna kimoja cha rasta kipo pale mbagara unaambiwq ukipata kazi wiki mbili za mwanzo unalipwa elfu mbili na miatano halafu baada ya hapo ndio wanakusajili sasa unaanza kulipwa elfu tano yaani hapo ndio wamekupitisha rasmi kwahiyo hizo wiki mbili za mwanzo utajua mwenyewe upambane vipi ili ufike kwenye kulipwa elfu tano ni dharau za wazi kabisa hizi kwa nguvu kazi ya taifa letu, ila cha ajabu unakuta watu wamerundikana nje wakijaribu bahati zao wengine hata kwa kutoa hongo ili tu wachaguliwe kuingia humo utumwani, naelewa hawafanyi kwa kupenda bali ni hali ngumu ya maisha waliyonayo ndio hupelekea hayo ni masikitiko.

Hawa mabosi wakihindi waarabu sijui wachina wanapata wapi hii jeuri ya kugeuza watanzania watumwa ndani ya nchi yao wenyewe? yani wakati mwingine wanatoa majibu yanayoothibitisha wanajiamini kwa kiwango kikubwa mno kwamba hakuna mtu anayeweza kuwafanya lolote, kuna mchina aliwahi kuwadhurumu pesa vibarua wake na akawajibu kwamba hamuogopi kiongozi aliyekua madarakani kwa wakati huo kwa kumtaja jina kabisa hebu jiulize huyo mtu wanapata wapi ujasiri wa namna hivyo kwenye nchi ya watu? yani wao wanafata tu ule msemo wa heri punda afe mzigo ufike.

Nchi za wenzetu huwezi kukutana na madudu haya ya hapa kwetu na ndiomana wametudharau sana kwa sababu hata tuliowapa jukumu la kutusimamia na kutuongoza hawatujali wanajali matumbo yao na familia zao, wenzetu wanasheria ngumu kwa wageni kuwekeza kwenye nchi zao huwezi kuta mzawa ananyanyasika kizembe akiwa chini ya boss wa kigeni ,

Raisi wangu ulisema huwa unapitia jamii forum naomba Mungu uone na hili bandiko langu ili angalau utoe tamko litakalowaokoa wapiga Kura wako hawa wa hali ya chini waliopo huko utumwani panapoitwa viwandani palipobatizwa jina la kazini ili watunyonye kwa urahisi, naelewa sio kila kitu lazima ufanye wewe bali una wateule wako ambao umewateua kusimamia maeneo hayo lakini kwa makusudi au bahati mbaya hatuwaoni kusikia vilio vyetu maana machozi yetu ni machozi ya samaki hayaonekani na hata wakiyaona hawayajali kwakua hayawahusu wao wala familia zao lakini kwa tamko lako ewe muheshimiwa linaweza kuwaamsha usingizini na kukumbuka ni nini wajibu wao kwa raia wa Tanzania waliowaamini na kuwapa madaraka ya kuwaongoza,

Pia napendekeza itungwe sheria ngumu kuhusu maslahi ya vibarua na haki zao na kuwepo na kiwango cha chini kinachotambulika kisheria kuwalipa vibarua na mwekezaji yeyote atakayeshindwa kufikisha kiwango hicho asipewe kibali cha kuendesha kiwanda na kama tayari anacho afikishwe mbele ya sheria kwa kosa la dhurma pamoja na uvunjifu wa sheria.. Viongozi pia wawe na utaratibu wa kutembelea huko viwandani ili kusikiliza hizi kero na malalamiko kutoka kwa vibarua wenyewe ili kujua kama sheria na katazo zilizowekwa au zitakazowekwa zinafuatwa kikamilifu au wanaendelea tu kufanya kazi kwakua hawana namna nyingine ,

Na mwisho sisi raia wenyewe tuwe na umoja tuache nidhamu ya woga tulionayo ambayo inachangia kutukandamiza sisi wenyewe bali tuamke tupaze sauti tusiwe warahisi wa kukubali kutumikishwa kitumwa na wageni ndani ya nchi yetu wenyewe ikiwemo hata kufanya migomo yenye nguvu kwa umoja ili kutetea maslahi yetu hata kama hatujaajiriwa tuna haki zote kama wafanyakazi tunaochangia uzalishaji na kuleta maendeleo kwenye jamii na mara zote sauti ya wengi ni sauti ya Mungu naamini tukifanya hayo tutafanikiwa kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo hili hata kama halitoisha kabisa lakini angalau itaonekana kwa kiwango kikubwa, naomba kuwasilisha.
 
Upvote 30
Kwani wamelazimishwa?

Uchaguzi ni wao waende au wasiende
Huoni wawekezaji wa hivyo wanafanya nchi yetu kuwa shamba la bibi? waonee huruma mkuu hakuna aliyeomba hayo maisha
 
Kazi ikiwa ngumu, Unaiacha tu.
 
Nimesha'vote mkuu. Hongera sana, you've made so many valid points in between na hopefully wahusika wataona na kukumbushwa maana sio kwamba hawajui, la hasha! wanajua ila huenda wana maslahi na jambo hili maana malalamiko hayajaanza jana wala juzi.

Mama zetu, baba zetu na vijana wenzetu wanateseka sana sana sana sana sana sana kule. Back breaking works ila hela anayolipwa ni aibu.

Nothing short of UTUMWA.
 
Shindano limefungwa ila hadi leo kimya hawajatoa update yoyote
 
Ukitaka msaada usiandike kwa ujumla orodhesha majina ya viwanda, sehemu vinapopatikana ikiwezekana jina la mmiliki wa kiwanda na vitua anavyo fanya ili iwe rahisi kusaidika
 
Hizo bei za viwandani mkuu zipo kihalali,
Kima cha chini kwa vibarua viwandani ni 3,000/- kwa siku,

Serikali haiwez pandisha mana ukipandisha gharama za uwekezaji zitakuwa juu, hivyo wawekezaji wataenda nchi nyingine na hivyo kukosa hata kidogo tulichopata saizi,
Kikubwa serikali ipambane tupate wawekezaji wengi zaidi, ili ushindani wa kupata vibarua upande,
Pia serikali iboreshe sekta ya kilimo na ufugaji, (kwa kiasi fulani wanajitahidi kwa sasa) ili vijana wajikite huko,

Mazingira ya biashara ndogo ndogo pia yaboreshwe
Mwisho sisi wenyewe wananchi tujitume, sio kwenda kufanya kazi za 3000/- kisa tu jina nimeajiriwa wakati ungepika uji au kwenda kubeba mizigo stand ya Magufuli ungepata 20k per day
 
elfu tatu aisee bora uuze maandazi tu
 
Kwa kifupi kazi za viwandani nyingi ni mateso kwenye utendaji wa kazi mpaka kwenye kulipana.
Ndio uchumi wa viwanda huo wa Tanzania, sheria za kumlinda mfanyakazi /kibarua lazima ziwepo ili uchumi wa viwanda uwe wa kweli kwa kila mtu, tatizo viongozi ni wapiga domo tuu, hata kwa mabeberu wafanyakazi walikuwa wanaonewa sana miaka ya zamani lakini union na migomo zilisaidia kuondoa huu ujinga, tuanzie at least na kuweka kiwango cha minimum wage kinachokubalika, usalama wa kazi na idadi ya masaa ya kazi kabla ya overtime
 
Back
Top Bottom