Mkuu nawe ushabiki umekujaa. Jua kuwa hakuna aliye juu ya KATIBA si Bunge, Serikali wala Mahakama. Hivyo mtumishi yeyote anaweza kuachia /kuachishwa utumishi wa wa Umaa kwa mujibu wa Katiba. Aidha tambua kuwa Rais ni sehemu ya Bunge na ni Mwenyekiti wa Chama kinachoisimamia Serikali hivyo ana nguvu kubwa. Kama anataka kabisa kusimamia Katiba, kwa kuhakikisha utawala wa sheria unazingatiwa hata kwa asilimia 80 anauwezo usio na shaka wa kumuondoa Spika madarakani: Njia ya kwaza ni kupitia Bunge. Kuna njia nyingi za kutekeleza hadi bunge kuvunjwa. Pili kwa kutumia Chama, yeye kama Mwenyekiti wa Chama Dola anauwezo wa kuitisha kikao cha na kujadili tuhuma na makandokando haya ya Covid 19 kwa manufaa ya Chama chake na hatimaye mtu kunyang'aywa kadi. Tatu, kupitia MAHAKAMA, anaweza kuitumia Wizara ya Sheria na Katiba kwa kushirikiana na Tanzania Law Society kuhoji mahakamani juu ya suala hili pamoja na matumizi ya fedha. Hakuna kisichowezekana kwa RAIS kwa kutumia KATIBA ya JMT