Kilio na sala ya Lissu toka Ukonga: Watanzania mmelala? Mimi sijalala

Dah🥺 mkuu Kalamu asante sana ndio unanifumbua macho sasa
 
Huyo Magufuli si ndio aligomea katiba mpya, alikuwa anakwamishwa ana anajikwamisha? Ama alikataa katiba mpya ili aongoze nchi kama familia yake? Unanitajia Mbowe huyo muhuni, mimi naongelea nini kuhusu Mbowe, alikuwa rais? Aliwahi kukataa katiba mpya, ama namlaumu ili uone nimebalance?
 
Hili limama katili sana aisee, hata madikteta waliopo kwenye historia walikuwa na aibu kidogo sio hili dude kabisa na linatoka nje kuhutubia watu waliowaita kenge
 
Hayuko na wengine bali cell ya peke yake, na alisema mahakamani kawekewa cctv ili kumdhalilisha. Hiyo hadi kuongea na wanasheria wake anasikilizwa na askari magereza ni kinyume cha sheria.
Si Kweli Gerezani mtu anatengwa kama kafanya Kosa jela kama kupigana au kukutwa na vitu ambavyo haviruhusiwi kama Bangi, Sigara, Simu , Ugolo, Cash au amefanya kitendo cha Ushoga au Ubasha.

Wengine wanaotengwa ni Kichaa ambaye ni violent anaweza kudhuru wenzake kwa kuwapiga au kuwajeruhi kwa namna yoyote hakuna mtu anatengwa tuu bila sababu.
 
Si kweli wakati alilisema hilo gerezani, na akawataka majaji waende wakajiridhishe na maneno yake maana wanaruhusuwa kisheria. Lakini majaji hawajathubutu kwenda. Yaani mahakama na magereza wanatumika kipuuzi mpaka hata wasio na ufahamu wanaona wazi.

Achia hayo, mahabusu anaruhusiwa kuongea na wanasheria wake kwa faragha, hilo halifanyoki na amesema mara kibao hapo mahakamani, na mjaji walisema lifanyiwe kazi lakini halifanyiki. Na hilo utasema si kweli? Yaani mnachezea sheria kijinga mno mpaka mnadharaulika.
 




Kwani kwa kadiri ya uelewa wako,hii Nchi imeshakuwa na viongozi wa juu(Rais)wangapi kabla ya JPM kuwa Rais?

Je wangapi kati yao walikubali hiyo KATIBA MPYA?

Kwamba unaamini kwa dhati kabisa matatizo ya Taifa hili yatakoma pindi tu KATIBA MPYA ikipatikana?


Na mwisho kabisa,kama mpaka leo hii unashindwa kujua mbowe ana mchango upi kwenye yanayoendelea hivi sasa,basi endelea kuamini unavyoamini kuwa JPM ndio chanzo cha yote

NB: kwa sababu mbowe hajawahi kuwa Rais,hapaswi kulaumiwa,lakini wakati huo huo upo mstari wa mbele kuwalaumu kina makonda,mwigulu,chalamila,,sirro ,wambura,Nkunda,lipumba,zitto,salumu mwalimu nk nk,..
 
Magu alipoingia madarakani alitukuta kwenye hatua ya kura ya maoni, usitake kuniambia habari za Marais wengine. Maana ambao hawakuleta habari za katiba mpya ni Mwinyi na Mkapa tu, lakini JK alianzisha mchakato, na akaachia hatua ya kura ya maoni rais anayefuata amalizie baada ya uchaguzi wa 2015. Magufuli akagomea.

Matatizo ya taifa hili hayawezi kumalizwa na katiba mpya maana si yote yanamalizwa na katiba mpya, lakini wangalau kiutawala tungeenda hatua mbele.

Mbowe ni muhuni kama wahuni wengine, sina cha kumlaumu bali nampuuza kwa siasa zake za kidalali. Naona umeniwekea orodha ya wahalifu na wapinzani maslahi, sijui unataka nikujibu nini. Acha kuniwekea orodha utakavyo kisha utake nikupe majibu utakayo ww.
 
Kaka sijamtaja SAMIA popote hapa... Samia sio serikali kaka na ndio mwanzo wa kufeli kwa sababu hamjui mnapambana na nani.... Matusi na kejeli kwa SAMIA ni upuuzi SAMIA sio serikali
 
uko sahihi, sasa kesi si iendelee ama serekali inajilinda nje ya sheria? Unataka kuonyesha serekali ina haki, lakini voters turn out ya juzi imeonyesha serekali haina uhalali wa umma. Usichanganye serekali na genge la majizi liloko madarakani.
Kwa katiba ya TANZANIA uhalali wa Serikali haupimwi kwa turnout naaamini hili unalifahamu na hili ndilo kosa mnalifanya kususa sio suluhu

Wangejitokeza wananchi 20 na mshindi akapata kura 12 angetangazwa tu na asilimia angepewa.
 
Kuna visasi vikubwa vinakuja
 
Kwa katiba ya TANZANIA uhalali wa Serikali haupimwi kwa turnout naaamini hili unalifahamu na hili ndilo kosa mnalifanya kususa sio suluhu

Wangejitokeza wananchi 20 na mshindi akapata kura 12 angetangazwa tu na asilimia angepewa.
Uko sahihi, na ndio maana tuligoma kushiriki huo uchaguzi tukitaka mabadiliko ya hali hiyo. Tumeomba muda mrefu hilo lirekebishwe kwani ni mapungufu yanatumika kuibeba ccm. Hatuwezi kuendelea kushiriki tukitegeme mabadiliko kwa njia hizo hizo.

Bila kuogomea kuonyesha haturidhiki hatutaeleweka, na muendelee kuomba tusikamate silaha, mbona na nyie mtalia kama sisi. Uvumilivi umeshafika mwisho.
 
Ulitaka watu wafanyeje, Mo29 watu wameingia barabarani wakiwa hawana silaha wakauwawa. Je ulitaka nini boss?
Pengine baada ya kutaja 29,nitaishiwa nguvu ya kuendelea kuprove my point.

Itoshe kusema inatosha mkuu.
 
Mbona anajifanya yeye Mandela wa Ikungi? Miezi 11 tu kachoka wakati Nelson Mandela alikaa miaka 27?? Mwambieni bado, hawezi kurudi huku uraiani kuja kukinukisha
 
Mbona anajifanya yeye Mandela wa Ikungi? Miezi 11 tu kachoka wakati Nelson Mandela alikaa miaka 27?? Mwambieni bado, hawezi kurudi huku uraiani kuja kukinukisha
Kuna ufanano wowote wa Africa Kusini na hapa hata kimaendeleo, ili tujue ni mfanano wa kila kilichokuwa Africa kusini na hapa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…