Killy na Cheed wajitoa King's Music

Killy na Cheed wajitoa King's Music

Kiba wa zamani alikuwa hot sana, nlikuwa naskiliza sana ngoma zake enzi hizo Makmuga,dushelele, Nakshinakshi, sindelela, na nyinginezo nyingi tu,


Sent using Jamii Forums mobile app
🤣🤣🤣🤣🤣🤣Sasa hivi dodo,kiufupi huu wimbo katoa Boko la hatari,bora angeendelea kukakaa kimya,ingekuwa anatoa back to back tungechukulia kawaida,lkn anakaa mwaka then anakuja kutoa nyimbo kama hiyo.
 
[emoji23]

Mkuu usishangae wakajoin WCB

Sent using Jamii Forums mobile app
Sisi mashabiki wa WCB hatuna noma mzee... hata Ali Kiba akija kwetu tutampokea kwa mikono miwili... Noma inaanzaga pale tu wanapomshindanisha boss wa WCB na local artists km Kiba na Harmonize!

Harmonize alipotoa bedroom tukamkabidhi Mbosso na tamba yake... mmakonde huyo aligaragazwa vibaya mno

Kiba akatoa dodo, tukamkabidhi mtoto Zuchu ambaye ndo kwanza alitambulishwa siku hiyohiyo, lakini umeona anavomuendesha Kiba huko mitaani na youtube

Kwahiyo wasisindanishe hizo takataka na Almasi... Wakija huku usafini wajiandae kuwa juu ya Kiba au kuwa zaidi yake
 
Waliyokuwa wasanii wa kingsmusicrecords, cheed na lkilly wametangaza leo asubuhi kujitoa kwenye lebo hiyo kupitia ujumbe wa pamoja walioweka kwenye kurasa zao Instagram.

Wawili hao wamemshukuru alalikiba pamoja na Uongozi mzima wa KingsMusic kwa nguvu na sapoti waliyoiwekeza kwao tangu walipoingia kwenye lebo hiyo ya muziki.

Killy na Cheed ni miongoni mwa wasanii wa awali waliotambulishwa katika lebo hiyo mwanzoni mwa Oktoba 2018.
Na nyie mmeanza kiki eeeh,mammaee,game imekuwa ngumu hivyo Hamna budi mfuate nyayo za WCB za enzi zileee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umetambulishwa rasmi kwenye lebo ya mwanamuziki anayejiita King tangu Oktoba 2018 leo unakuja kuzidiwa umaarufu na idadi ya mashabiki na msanii (tena wa kike) aliyetambulishwa ndani ya wiki moja iliyopita kwenye lebo nyingine halafu usiondoke kwenye hiyo lebo ya King uliyopo?

Yani toka ulipoanza kupromotiwa na bosi wako kwa zaidi ya mwaka na nusu mpaka leo una wafuasi 108k pekee kwenye Instagram halafu demu amepromotiwa kwa siku chache tu ana wafuasi 201k na namba inakuwa kwa kasi ya Kovid19; Bado usiondoke? Utakuwa una moyo wa chuma.

Umetoa video yako na kumshirikisha msanii mwenye jina kubwa kama Marioo miezi miwili iliyopita kwenye mtandao wa YouTube halafu una watazamaji 800k pekee; Kidemu kimetoa video ndani siku tano halafu ina zaidi ya mara mbili ya watazamaji wa video yako wewe; Bado usiondoke kwenye hicho kikundi cha wasanii wachanga wanachojaribu kukiita lebo? Utakuwa mzembe.

Na wewe mwingine uliachia video dunia ikiwa na kesi 3 tu za Corona (huko Wuhan) ukimshirikisha King, leo hii umeachwa mbali kwa views na demu alieachia video juzi kukiwa na kesi karibu 2M za Corona duniani. Na mwenzio hakumshirikisha mtu yeyote. Je, angemshirikisha yule bosi wake mwenye sifa? Ondoka hapo. Hao hawajui biashara ya muziki.

Nawashauri kama ni 'kiki' kwa sasa hakikisheni mnaondoka kweli. Wasanii wa WCB nao wanaanzisha lebo zao hivi punde ambazo bado zitakuwa chini ya WCB hata hivyo. Kwa hiyo Cheed na Killy mtapewa kipaumbele cha kujiunga nasi. Wewe Cheed unaweza kusainiwa kama msanii wa Mbosso kwenye lebo yake. Killy tutakuweka chini ya Zuchu ambaye pia ataanzisha lebo yake kabla ya kufanya hata shoo moja.

Njooni huku kwenye utamu wa kufikisha mamilioni ya views bila kupoteza muda wala nguvu nyingi.

Narudia; Kama ni 'kiki' badilini mawazo mfanye kweli. Mtafika mbali zaidi kiumaarufu na kiuchumi mpaka mtakuja kushindanishwa na huyo mnayemtambua kama King ndani ya miezi miwili.
 
Killy amesema amejitoa katka rebo ya King music inayomilikiwa na msanii Ally kiba ameongeza kua amechukua uamzi huo binafsi ili kuendeleza mziki wake

Hii imekuja baada ya msanii mwenzie CHEED kutangaza kujitoa katka lebo hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo slow Mzee hii taarifa ilisharushwa na watu 2 teyari humu usishangae mod akiunganisha Uzi wako na wawenzio.
 
We ulikuwa wapi hii taarifa tushaipata tangu Jana usiku hapa Jf
 
Nikishaonaga post kama hizi huwa naongeza speed ya ku scroll


#Bagwell
 
Killy amesema amejitoa katka rebo ya King music inayomilikiwa na msanii Ally kiba ameongeza kua amechukua uamzi huo binafsi ili kuendeleza mziki wake

Hii imekuja baada ya msanii mwenzie CHEED kutangaza kujitoa katka lebo hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.




Sent using Jamii Forums mobile app
"rebo" ndiyo nini? Ina sound kama Kirusi kipya!
 
Sasa Umeandika nini nachukia sana kuona mtu mzima unaandika Ujinga. Wewe ukishajiunga JF unabidi uandike vitu vyenye ualisia sio kuandika Upuuzi.
 
Back
Top Bottom