Killy na Cheed wajitoa King's Music

Killy na Cheed wajitoa King's Music

Huyo mwenye sauti ya Ali kiba sitashangaa WCB wakimchukua

keep-hoping-5be28f.jpg
 
Hao walishaona safari ya kupelekwa Mombasa kwa Sheikh Joho imewadia wamekula kona.
 
Waliyokuwa wasanii wa kingsmusicrecords, cheed na lkilly wametangaza leo asubuhi kujitoa kwenye lebo hiyo kupitia ujumbe wa pamoja walioweka kwenye kurasa zao Instagram.

Wawili hao wamemshukuru alalikiba pamoja na Uongozi mzima wa KingsMusic kwa nguvu na sapoti waliyoiwekeza kwao tangu walipoingia kwenye lebo hiyo ya muziki.

Killy na Cheed ni miongoni mwa wasanii wa awali waliotambulishwa katika lebo hiyo mwanzoni mwa Oktoba 2018.
Wagendua Gari mbovu huwa hazivutwi na mbovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umetambulishwa rasmi kwenye lebo ya mwanamuziki anayejiita King tangu Oktoba 2018 leo unakuja kuzidiwa umaarufu na idadi ya mashabiki na msanii (tena wa kike) aliyetambulishwa ndani ya wiki moja iliyopita kwenye lebo nyingine halafu usiondoke kwenye hiyo lebo ya King uliyopo?

Yani toka ulipoanza kupromotiwa na bosi wako kwa zaidi ya mwaka na nusu mpaka leo una wafuasi 108k pekee kwenye Instagram halafu demu amepromotiwa kwa siku chache tu ana wafuasi 201k na namba inakuwa kwa kasi ya Kovid19; Bado usiondoke? Utakuwa una moyo wa chuma.

Umetoa video yako na kumshirikisha msanii mwenye jina kubwa kama Marioo miezi miwili iliyopita kwenye mtandao wa YouTube halafu una watazamaji 800k pekee; Kidemu kimetoa video ndani siku tano halafu ina zaidi ya mara mbili ya watazamaji wa video yako wewe; Bado usiondoke kwenye hicho kikundi cha wasanii wachanga wanachojaribu kukiita lebo? Utakuwa mzembe.

Na wewe mwingine uliachia video dunia ikiwa na kesi 3 tu za Corona (huko Wuhan) ukimshirikisha King, leo hii umeachwa mbali kwa views na demu alieachia video juzi kukiwa na kesi karibu 2M za Corona duniani. Na mwenzio hakumshirikisha mtu yeyote. Je, angemshirikisha yule bosi wake mwenye sifa? Ondoka hapo. Hao hawajui biashara ya muziki.

Nawashauri kama ni 'kiki' kwa sasa hakikisheni mnaondoka kweli. Wasanii wa WCB nao wanaanzisha lebo zao hivi punde ambazo bado zitakuwa chini ya WCB hata hivyo. Kwa hiyo Cheed na Killy mtapewa kipaumbele cha kujiunga nasi. Wewe Cheed unaweza kusainiwa kama msanii wa Mbosso kwenye lebo yake. Killy tutakuweka chini ya Zuchu ambaye pia ataanzisha lebo yake kabla ya kufanya hata shoo moja.

Njooni huku kwenye utamu wa kufikisha mamilioni ya views bila kupoteza muda wala nguvu nyingi.

Narudia; Kama ni 'kiki' badilini mawazo mfanye kweli. Mtafika mbali zaidi kiumaarufu na kiuchumi mbaka mtakuja kushindanishwa na huyo mnayemtambua kama King ndani ya miezi miwili.
😃😃😃😃😃😃😃
 
Kama sio kiki wamefanya la maana sana na kiba anatakiwa awalipe kwa kuwapotezea muda.

Haiwezekani wasainiwe 2018 mpaka leo hawana hata baiskeli na career yao yote wamezidiwa kila kitu na zuchu aliesainiwa hata wiki haijaisha.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Waliyokuwa wasanii wa kingsmusicrecords, cheed na lkilly wametangaza leo asubuhi kujitoa kwenye lebo hiyo kupitia ujumbe wa pamoja walioweka kwenye kurasa zao Instagram.

Wawili hao wamemshukuru alalikiba pamoja na Uongozi mzima wa KingsMusic kwa nguvu na sapoti waliyoiwekeza kwao tangu walipoingia kwenye lebo hiyo ya muziki.

Killy na Cheed ni miongoni mwa wasanii wa awali waliotambulishwa katika lebo hiyo mwanzoni mwa Oktoba 2018.
Muangalie Tve ijumaa kipindi cha Homa, king Kiba live music

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa wangekuwa WCB hapa pangewaka humu JF .

Wangeanza

" Mondi kachuja,Babutale,Sallam wanyonyaji,Mondi siku hizi anatoa matataka nyimbo alikuwa na tungiwa na madogo........mara hee.....mara hooi.....Mondi anawadhulumu.."

Threads hapa zingekuwa mia humu JF.Mondi ana moyo sio kazi ndogo unakaa na msanii zaidi ya miaka mitatu,haingizi hata senti unamfundisha na kumwandaa na maisha ya mziki,una mbrand,unampromote ,unamtengenezea connection ktk Industry kubwa za Africa mpaka anafika kileleni si kazi ndogo unahitaji uwe na moyo wa uvumilivu.
Mkuu ukiona mtu anakuongelea sana ujue umemzidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom