Kilo moja ya nyama kuuzwa 13,000 ni laana au ni nini?

Acheni kuthamini sana nyama ya ng’ombe, mbuzi na kondoo. Kutegemea hao wanyama ndio shida inapoanzia.
Jifunzeni kula samaki nchanga, mbuzi wa iringa, mbuzi katoliki,sungura, simbilisi na wanyama wengine. Hata tumbili na jamii zake, piga tu. Na viumbe vya majini, tafuna tu, almradi havina sumu.
 
Hii nyama kupanda bei ni hatari sana kwa afya za wananchi. Wananchi wataanza kula vibudu, mifugo inayojifia na kutupwa hovyo bila kufukiwa kama zile ng'ombe, mbuzi, kondoo, kuku wanaokufa minadani wakiwa wanauzwa. Wananchi wataanza kula hata mizoga kama ng'ombe waliokufa machungani na kutelekezwa na wenyewe. Kuna hatari ya kula hata wanyamapori kimagendo, kijangili na kiharamia. Wanyama wasioliwa kama simba, chui, fisi, mbweha, nyani, mamba, mwewe na ndege wengine wasioliwa wataanza kuliwa na tayari walafi wa nyama wameanza kuwala, ni hatari sana kwa afya zao
 
Vibudu vinaliwa daily km hujui kaka na huku Dodoma PUNDA ndo wanaliwa ogopa nyama ya elf 7
 
Pale pugu mnadani pembeni ya reli kuna vichaka vibudu hufukiwa huko. Kwa usawa huu bei ya nyama iko juu, ukiwapa kazi vibarua wakafukie mizoga ya ng'ombe waliojifia hawataifukia, ni fursa ya kupata hela chapchapu kwa kuuza mzoga mitaani kwa kificho, ni hatari sana nyama kupanda bei
 
Hao ng'ombe watawakuta porini huko au watapewa bure?
 
Huyo anayetoa bei elekezi anafuga hata mbwa kweli?
usidharau MBWA bro. kumtunza mbwa kuna gharama kuliko kumtunza ng'ombe. Hata bei ya mbwa (wale walio MBWA kwelikweli) Iko juu ya bei ya ng'ombe.
 
Kupanda bei nyama wananchi hawatashindwa kula mbwa na paka mradi tu wale nyama kama nyama za buchani ni ghali
 
usidharau MBWA bro. kumtumza mbwa kuna gharama kuliko kumtumza ng'ombe. Hata bei ya mbwa (wale MBWA kwelikweli) Iko juu ya bei ya ng'ombe.
Naelewa mkuu kuna jamii ya mbwa bei ziko juu sana.
Ila hapa nililenga mbwa wetu hawa wa kiswahili
 
Kula kuku au fuga kukuwako kuku 150kwa mwka ukiwazalisha unakuwa ushakwepa hizo gharama za nyama ya ngombe baada ya siku mbili unachinja kuku au unauza kuku mmoja...case closed..kwenda huko maporini bila uchawi na roho ngumu huwezi kufuga NI mateso na mauaji..faanya uchunguzi wafugaji wa kisukuma maporini wanita lubaga...NI story za kusikitisha zaidi ya vita
 
Tutakula utumbo,nao ikishindikana tutabakia kula finyango za miguu ya kuku,filigisi na vichwa,muhimu hapo upate nyanya za kutosha...
 
Nasikia enzi za mtume ndiyo ilikuwa mlo wa kifalme mpaka mtume akapiga marufuku kitimoto kuliwa hadharani ila mpaka siku maalum tena inaliwa na wafalme tu
Mbona supu wanakunywa?
 
LAANA kivip ilhali Wafugaji na mnyororo wa thamani sekta ya uvuvi unaongezeka?

Hiyo ni fursa ichangamkie.

Peleka huko nyama yenye Bei nafuu kidogo uwe tajiri.
 
Solution ni watu wengi kujikita kwenye ufugaji automatically, chakula na madawa vitafall down na nyama itakuwa bei cheap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…