Uchaguzi 2020 Kilochopelekea Tundu Lissu kwenda kwa haraka kumwaga sumu Zanzibar

Uchaguzi 2020 Kilochopelekea Tundu Lissu kwenda kwa haraka kumwaga sumu Zanzibar

Kejuu

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2020
Posts
645
Reaction score
906
Ndugu watanzania wenzangu,

Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuiona siku ya leo.

Kwa kifupi sana, nadhani baada ya Tundu Lissukuona trend ya kampeni za Mh. Magufuli: Dodoma, Tobora, Shinyanga, Simiyu, Mara, na baadaye mapokezi yake kule Mwanza, wanamwanza ndiyo walivunja rekondi ya kutoa sauti kubwa ambayo ilisababisha kumtoa nyoka pangoni na hatimae TL aliamua kuweka pembeni kampeni za bara na kukimbilia Zanzibar ili aanze kusaka kuungwa mkono kwa kulazimisha, na hii ni sawa na mwanamke kutafuta kuolewa kwa lazima. Na haya ndiyo madhara ya kutojipanga katika kusaka kinyang'anyiro nyeti kama hiki, na katika siku hizi 49 zilizobaki tutaona sarakasi nyingi na kukurupuka kwingi kwa TL.

Kwa wote msiompenda Magufuli, hata mtaungana wote, bado Mh. Magufuli ndiyo atakuwa Rais watz kwa miaka mingine 5, na sijaona chama mbadala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). kama vyama vilivyotegemewa kuwa na sera mbadala vimegeuka na kuwa vyama vya mabeberu, what else should I expect from them rather than kubaki na CCM ambayo Mh. Magufuli ameonyesha substantial changes ndani ya chama na taifa kwa ujumla?

Asante sana,
Nawasilisha,
Kejuu
 
Hongera mleta mada. Ninavyojua kadiri ya mtandao ni kwamba Chama hiki kilijipanga siku 10 za kwanza kufanya amshaamsha ktk ngazi ya kanda. Shughuli hii imefanikiwa kama ulivyojionea, wamemalizia Zanzibar. Kesho wanaanza sasa Jimbo kwa Jimbo.

Muombe Mungu tuendelee kuwepo TUPATE mazuri ya wagombea hawa. Kikubwa tupunguze upenzi, tuandike uhalisia
 
Uwezo wake unaishia kwenye Mipasho, Sijui baada ya Matatizo kumpata kuna katatizo kama jinsia kalisheki.
NB: Nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema usirudie kuitamani 😎😎😎😎
Halafu wanaiblackmail serikali
 
[SUB]Mmmh, siyo kweli kajiendea, ni Ratiba ya Tume na inafuatwa, hawajiamlii tu, ukiwa wanajiamlia so watagongana sehemu moja? Hapo mleta mada umepotoka[/SUB]
Wanaelewa nini hawa bendera fuata upepo?
 
Uwezo wake unaishia kwenye Mipasho, Sijui baada ya Matatizo kumpata kuna katatizo kama jinsia kalisheki.
NB: Nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema usirudie kuitamani 😎😎😎😎
Hivi kuna mtu wa kupiga risasi 38 kwenye nyumba za viongozi mchana kweupe... halafu Magufuli aendelee kumchekea IGP?... kichwa sio pambo
 
Mikutano ya CCM Bila wasanii, malori na wanafunzi ni sawa na hashimu Rugwe hebu itafute ile video imefika mahali stand imehamia CCM Kirumba
 
Tuliaminishwa kuwa CHADEMA imekufa, mwimbo huu ukaimbwa sana mpaka sisi wengine tuka amini. Sasa mbona kelele nyingi, maiti inawanyima usingizi?

Tukaaminishwa pia kuwa kuna mtu hana haja ya kufanya campaign, sasa kelele za nini mbona huyo jamaa yuko barabarani 24/7 badala ya kwenda Likizo akingojea kuapishwa.

Sasa najiuliza je huko ni salama au gogo ndio laanza kuanguka?
 
Wacheni upotoshaji na ramli za kijinga, CHADEMA walishapanga ratiba zao kuwa watafanya uzinduzi kwa kanda zao zote KUMI kwanza then watarudi kujipanga kuanza kushambulia Jimbo kwa jimbo, na hii yote ilienda sambamba huku wakisubiri rufaa zao wajua wapite wapi na wanaenda kufanya nini.

kifupi ilikuwa rasharasha subiri kumbunga soon kitaanza.
nadhani watapiga CHOPA round ya pili kama kawaida yao.
 
Ndugu watanzania wenzangu,

Kwanza napenda kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuiona siku ya leo.

Kwa kifupi sana, nadhani baada ya TL kuona trend ya kampeni za Mh. Magufuli: Dodoma, Tobora, Shinyanga, Simiyu, Mara, na baadaye mapokezi yake kule Mwanza, wanamwanza ndiyo walivunja rekondi ya kutoa sauti kubwa ambayo ilisababisha kumtoa nyoka pangoni na hatimae TL aliamua kuweka pembeni kampeni za bara na kukimbilia Zanzibar ili aanze kusaka kuungwa mkono kwa kulazimisha, na hii ni sawa na mwanamke kutafuta kuolewa kwa lazima. Na haya ndiyo madhara ya kutojipanga katika kusaka kinyang'anyiro nyeti kama hiki, na katika siku hizi 49 zilizobaki tutaona sarakasi nyingi na kukurupuka kwingi kwa TL.

Kwa wote msiompenda Magufuli, hata mtaungana wote, bado Mh. Magufuli ndiyo atakuwa raisi watz kwa miaka mingine 5, na sijaona chama mbadala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). kama vyama vilivyotegemewa kuwa na sera mbadala vimegeuka na kuwa vyama vya mabeberu, what else should I expect from them rather than kubaki na CCM ambayo Mh. Maguli ameonyesha substantial changes ndani ya chama na taifa kwa ujumla?

Asante sana,
Nawasilisha,
Kejuu
Unaandika content isiyokuwa na hoja ya msingi. Wagombea wote wanafuata ratiba ya tume ya uchaguzi na sio wanajiamlia tu

Kazi ya Siasa achana nao infact hujui
 
Back
Top Bottom