Kilwa Masoko, Lindi: Zaidi ya Tani moja ya Dawa za Kulevya yakamatwa

Kilwa Masoko, Lindi: Zaidi ya Tani moja ya Dawa za Kulevya yakamatwa

Wadau huu mzigo mkubwa mnoooooo mnooooooooo
Nashangaa kwanini wameusafirisha ki local kiasi hicho yaani tani 2 za heroine au cocaine usafirishe kindezi hivyo?

Hao jamaa wanaujasiri na roho ngumu sana aisee yaani wamerisk maisha yao dadeq zao hao wapakistan!

Anyway tani mbili ni dharau kwa nchi yetu hao pimbi hao!
[emoji23][emoji23][emoji23]
Huo ndiyo usafirishaji wao wamekuwa wakitumia
Miaka ya nyuma unga watu walikuwa wanaingiza nchini kwa njia ya kumeza
Kuanzia miaka ya 2006 watu wakaanza
Kuleta kwa njia hii

Ova
 
duh wote huo si kuuana na kupunguza nguvu kazi za taifa. Jela maisha inawahusu
Sio jela maisha tu, Inabidi wanyongwe live tushuhudie kwa runinga kama ilivyokua kwa Sadam Hussein...

Tani 2 za heroine sio mchezo na pia ni dharau wameonyesha, Hizi records za mzigo mkubwa hivo ya Ngada ilizoeleka miaka ya 80's-90's enzi zake Pablo Escobar wa Columbia tena yeye alikua anasafirisha na ndege zake binafsi kupeleka USA!
 
Magu ameshafariki hawezi rudi tena naona nikukumbushe hilo. Madhaifu unayo yaona kwa Raisi wa sa hivi ndo ambayo walikuwa wakiona wengine wakati wa Magu.
Sema ulikuwa unamkubali sana magu hivyo kipindi chake huezi ukawa ulielewa alikuwa anakosea sana tu.
Madawa yalizibitiwa ndio ila bado yalipita na mateja walikuwepo wengi tuu.
Ili kuonesha polisi wamejitahidi ndo maana yameshikwa Au we ulitaka yasikamatwe yaingie mtaani? Au kutangazwa ndo shida?
Kuna watu wakipenda wanakuwa vipofu sijawahi kusikia utawala wa magu kukamatwa na mzigo mkubwa hivi.
Maana yake mizigo ilikuwa inapita tu lkn mama kateua kiongozi mpya wa kuzuia madawa ndio tunaona matunda yake.
 
Kuna watu wakipenda wanakuwa vipofu sijawahi kusikia utawala wa magu kukamatwa na mzigo mkubwa hivi.
Maana yake mizigo ilikuwa inapita tu lkn mama kateua kiongozi mpya wa kuzuia madawa ndio tunaona matunda yake.
Kwa sababu walikuwa wanashushia msumbiji ndy wanafanya mchakato wa kuingiza bongo,hii biashara ni sawa na mchezo wa paka na panya

Ova
 
Kiwango kama hiki cha madawa hakiwezi kupatikana kwa urahisi hata kwa wauza unga sugu, mpaka kuwe na mkono wa serikali fulani-fulani na taasisi kubwa. Watu walioweza kuuza madawa kwa viwango vya kuanzia tani ni aida ya Pablo Escobar na El-Chapo, ambao wao kupata tani 7 hadi 15 kwa siku ilikuwa ni kawaida tu. Inakuja kufahamika mwishoni kwamba wao hawakuwa wanafanya hivi kupata faida au utajiri, bali kulikuwa na ajenda kubwa sana wanaitekeleza.

Uelewa wangu wa kawaida tu, unanikumbuka kwamba kuna uhusiano mkubwa sana baina ya biashara ya MADAWA YA KULEVYA, UTAKATISHAJI PESA na UGAIDI. Pia, ili fedha zisionekane kirahisi basi taasisi ambazo zitatumika kufanya utakatishaji zitakuwa ni zile kubwa sana. Kuna mambo ukiyafikiria yanaogopesha sana.....
 
Back
Top Bottom