Kilwa Masoko, Lindi: Zaidi ya Tani moja ya Dawa za Kulevya yakamatwa

Kilwa Masoko, Lindi: Zaidi ya Tani moja ya Dawa za Kulevya yakamatwa

Dar es Salaam. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na kikosi cha wanamaji wamewakamata watu saba wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroin zaidi ya tani moja wakizisafirisha kwa kutumia jahazi katika Bahari ya Hindi eneo la Kilwa Masoko mkoani Lindi.

Waliokamatwa ambao wote si raia wa Tanzania ni nahodha wa jahazi hilo, Jan Mohammad Miranira, Amir Hussein, Yusuph Bin Hamad, Salim Bin Mohammad, Ikbal Pakir Mohammad, Jawid Nuhan Nur Mohammad na Mustaphar Nowani Kadirbaksh..

Akizungumza na Mwananchi Digital kamishna wa DCEA, Gerald Kusaya amesema raia hao wamekamatwa usiku wa kuamkia leo Jumamosi Aprili 24, 2021 eneo la Kilwa Masoko wakisafirisha dawa hizo.

Amebainisha watu hao bado wapo safarini kuletwa nchi kavu na watakapofika watahojiwa kuhusu dawa hizo, walikuwa wanakwenda wapi.
 
Mkuu Naona bado unaakili za jana usiku,
Mwenye akili za jana usiku ni wewe ulieweka picha ambayo haina maelezo ya wenye picha hiyo halafu unatulazimisha tuitumie kama source ya habari yako.Kama viroba vilivyopo kwenye picha ni viroba vya nafaka tutajuaje?Tutajuaje kuwa viroba vilivyopo kwenye hiyo picha ni viroba vya heroin na wala siyo viroba vya maharage?
 
Tuliokua tunasema now hatuna raisi Naona mnaanza kutuelewa tu taratibu ... rest in power magufuliI
Magu ameshafariki hawezi rudi tena naona nikukumbushe hilo. Madhaifu unayo yaona kwa Raisi wa sa hivi ndo ambayo walikuwa wakiona wengine wakati wa Magu.
Sema ulikuwa unamkubali sana magu hivyo kipindi chake huezi ukawa ulielewa alikuwa anakosea sana tu.
Madawa yalizibitiwa ndio ila bado yalipita na mateja walikuwepo wengi tuu.
Ili kuonesha polisi wamejitahidi ndo maana yameshikwa Au we ulitaka yasikamatwe yaingie mtaani? Au kutangazwa ndo shida?
Tuliokua tunasema now hatuna raisi Naona mnaanza kutuelewa tu taratibu ... rest in power magufuli
 
Back
Top Bottom