Kim Younhoon ndio mtu mwenye akili kubwa kuliko wote duniani, amesema Yesu ni Mungu

Kim Younhoon ndio mtu mwenye akili kubwa kuliko wote duniani, amesema Yesu ni Mungu

Magodi Katuni

Member
Joined
May 18, 2023
Posts
27
Reaction score
68
Kim YoungHoon, raia wa Korea Kusini na mbeba rekodi ya IQ (kipimo cha akili) cha juu zaidi duniani, amevunja ukimya na kugonga vichwa vya habari kwa ujumbe mzito wa kiimani. Kupitia ukurasa wake wa X, alitweet: “As the world’s highest IQ record holder, I believe that Jesus Christ is God, the way and the truth and the life.” (Nikiwa kama mtu mwenye IQ kubwa zaidi duniani, naamini kwamba Yesu Kristo ni Mungu, njia, kweli na uzima). Kauli hii imezua mijadala mitandaoni, ikizingatiwa imetoka kwa mtu anayehesabiwa kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kiakili duniani.

IQ (Intelligence Quotient) ni kipimo kinachotathmini uwezo wa mtu kufikiri kimantiki (logic), kutatua matatizo, na kuelewa dhana tata kwa haraka. Young-Hoon alijulikana kimataifa baada ya kushinda mashindano ya World Memory Championships, akipata alama ya IQ ya 276 kiwango kisichowahi kufikiwa na binadamu mwingine katika historia. Mafanikio yake yamekuwa yakihusishwa na uwezo wa kukumbuka, kuunganisha taarifa kwa kasi, na uwezo mpana wa mantiki (logic).

Japo wengi hufikiri kuwa maarifa ya kisayansi yanapingana na imani ya kiroho, Young-Hoon anaonesha tofauti. Kauli yake inaonesha kuwa hata kilele cha akili kinaweza kuungama mamlaka ya Yesu Kristo kama Mungu. Kwa kusema haya, si tu amehamasisha Wakristo duniani, bali pia amewachanganya wale waliowahi kufikiri kwamba imani ni ya watu "wanaoshindwa kufikiri sana".

SISI NI KINA NANI TUKATAE KAMA MWENYE AKILI AMEKIRI😁
 
Mimi sihitaji maprove ya iq test bali kazi zangu zitadhihirisha hivyo na legacy ntakayoiacha ni moja ya legacy kubwa kuwahi kutokea duniani

Mtu atakayezaliwa mwaka 2500, au mwaka 3000 lazima ataijua legacy yangu in a good way alama ntakayoiacha sio ya kitoto sijisifu hapana bali najaribu kuongea ukweli
 
Watu wenye IQ kubwa huwa wanakosa EQ wanakuwa hawana uwezo wa kusocialize hivyo ni vyepesi kumcontrol aende unapo taka wewe, we hutumii akili sababu anatajua una manipulate kwa kutumia emotions, akipata kasichana kakamcomtrol atafanya kanachotaka😁😁
 
Mimi sihitaji maprove ya iq test bali kazi zangu zitadhihirisha hivyo na legacy ntakayoiacha ni moja ya legacy kubwa kuwahi kutokea duniani

Mtu atakayezaliwa mwaka 2500, au mwaka 3000 lazima ataijua legacy yangu in a good way alama ntakayoiacha sio ya kitoto sijisifu hapana bali najaribu kuongea ukweli
Na wewe ni nani tena huko daslam?
 
Back
Top Bottom