G.Man
JF-Expert Member
- Feb 9, 2014
- 1,214
- 2,546
Sikufanya conclusion, ila ninachoona na nilivyokusoma kwenye threads unacho taka ni uthibitisho wa Mungu tangibly kwako, wakati huohuo hauamini uwepo wake.Hapana, iko sawa.
Ni kosa la kimantiki la hoja zisizofuatana.
Inawezekana ukawa kwenye mashindano ya comedy mbaya ya kutoa hoja zisizofuatana, ukafanya logical non sequitur ya kukusudia isiyo fallacy.
Conclusion gani umefanya?
Sasa Mungu ni Roho,na uthibitisho wake unamhitaji yeye mwenyewe kujidhihirisha kwenye maisha yako, maana chochote anachofanya ni kwa utukufu wake. Siku akitaka kujithibitisha kwako atafanya yeye kama apendavyo.
Mimi nina hakika yupo, Na amefanya mambo mengi kwangu na hata kwa watu wengine kupitia mimi, wala sio kwa kuhadithiwa au ku-act. Ni swala la kuamini tu.(kuwa na uhakika hata kama hujaona kwa macho)
Mungu anakupenda mkuu Kiranga hata kama unampinga, na alitumia gharama kubwa sana kwaajili yako. Neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu imefunuliwa ili ikutoe ndugu katika Uasi. Ni maombi yangu Mungu aonekane kwako. Amen