Kama akili yako inafanya kazi sawasawa, na Roho wa Mungu akakupa akili na ufunuo, lazima utakiri bila ya mashaka kuwa Yesu ni Mungu. Zingatia yafutayo:
Yohana 14: 6
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Hapa unaweza kusema yeye siyo Mungu, Mungu ni Baba yake.
Yohana 14:8
Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu?
Hapa inaonesha Yesu ni Mungu, bali Mungu aliamua tu kuchukua tu umbo la mwanadamu, lakini kilichokuwemo ndani ya umbile hilo ni Mungu mwenyewe. Na kwamba Mungu ana uwezo wa kuchukua umbile lolote lile: mwanadamu, wingu, jiwa, upepo, Moto, au kingine chochote.
Yohana 11: 25
Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi. Hii inaonesha kuwa mwenye uwezo wa kufufua siku ya mwisho ya Yesu. Na mamlaka na uwezo huo ni wa kiMungu.
Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. Yesu akajibu, "Kweli nawaambieni, kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko."
Hii inadhihirisha kuwa Yesu alikuwepo kabla ya mwanadamu yeyote. Hivyo kuzaliwa kwake lilikuwa ni tukio tu la kuubeba mwili wa mwanadamu ili afanane naye, na aweze kumwonesha mwanadamu anatakiwa kuenenda vipi katika ubinadamu wake.