Kim Younhoon ndio mtu mwenye akili kubwa kuliko wote duniani, amesema Yesu ni Mungu

Kama akili yako inafanya kazi sawasawa, na Roho wa Mungu akakupa akili na ufunuo, lazima utakiri bila ya mashaka kuwa Yesu ni Mungu. Zingatia yafutayo:

Yohana 14: 6
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Hapa unaweza kusema yeye siyo Mungu, Mungu ni Baba yake.

Yohana 14:8
Filipo akamwambia, Bwana, utuonyeshe Baba, yatutosha. Yesu akamwambia, Mimi nimekuwapo pamoja nanyi siku hizi zote, wewe usinijue, Filipo? Aliyeniona mimi amemwona Baba; basi wewe wasemaje, Utuonyeshe Baba? Husadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu?
Hapa inaonesha Yesu ni Mungu, bali Mungu aliamua tu kuchukua tu umbo la mwanadamu, lakini kilichokuwemo ndani ya umbile hilo ni Mungu mwenyewe. Na kwamba Mungu ana uwezo wa kuchukua umbile lolote lile: mwanadamu, wingu, jiwa, upepo, Moto, au kingine chochote.

Yohana 11: 25
Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi. Hii inaonesha kuwa mwenye uwezo wa kufufua siku ya mwisho ya Yesu. Na mamlaka na uwezo huo ni wa kiMungu.

Yohana 8:58
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko. Yesu akajibu, "Kweli nawaambieni, kabla Abrahamu hajazaliwa, mimi niko."
Hii inadhihirisha kuwa Yesu alikuwepo kabla ya mwanadamu yeyote. Hivyo kuzaliwa kwake lilikuwa ni tukio tu la kuubeba mwili wa mwanadamu ili afanane naye, na aweze kumwonesha mwanadamu anatakiwa kuenenda vipi katika ubinadamu wake.
 
Unamfahamu Albert Einstein?

Unajua huyo biggie anaingia mara ngapi kwenye akili ya Einstein?

Hebu nenda kagoogle ajabu la Einstein la8 duniani.

Halafu fuatilia alikua ana maoni gani kuhusu Mungu.
 
Haiwezekani na haiyumkiniki kiumbe chochote kilichoumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kisimjue Mungu huyo.

Kutomjua huko kuna contradict uwepo wa Mungu huyo.

Kutomjua Mungu huyo kwa kiumbe chochote, bila shaka, ni ukatili mkubwa sana wa uumbaji kwa upande wa Mungu huyo.

Na Mungu huyo, kwa sifa hizo, hana ukatili..

Kwa hiyo, ama una Mungu mwenye upendo wote ambaye ni katili sana, a contradiction.

Au.

Mungu huyo hayupo. No contradiction.

Conclusion.

Mungu huyo hayupo.

Ukibisha, tatua contradiction kwanza.
 
Bila kumjua Hashim Rungwe bado nina wasiwasi na IQ yake🌞
 
Ameshinda mashindano ya kuhifadhi kumbukumbu (kukumbuka alivyomezeshwa/kukariri) na hiyo haimuhalalishi kuwa ana uwezo wa kuchanganua mambo kuliko watu wote duniani.
Tofautisha uwezo wa kukariri na uwezo wa kuchanganua mambo ni vitu vilivyoachana kwa mbali kabisa. Mfano mzuri ni ndege kasuku ana uwezo wa kukariri na kurudia maneno yaliyotamkwa ila hajua hata maana ya alichokariri.
Usichanganye mimba na kitambi kwakuwa tu vyote huwa vinakaa kwenye tumbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…