Kimara, Dar: Polisi wawakamata kwa uzururaji Daktari chriscyrilo na Daktari Shindo Kilawa

Tuna sheria za aina yake...
 
Return Of Undertaker, Kumbe ni makamanda? Siku nyingine tafuta Uzi Wa makamanda halafu uwataarifu makamanda wenzenu,mana kwa raia Wa kawaida kama sisi yanakuwa hayatuhusu
 
Ndugu kuna utaratibu wa kisheria wa namna polisi anavyotakiwa kufanya ili kumkamata mtu. Utaratibu huo usipofuatwa polisi wanageuka kuwa watekaji tu na wasiojulikana. Na mambo haya ya kukamatana kienyeji ni kawaida sana ambapo polisi wenyewe walibainisha ukamataji huo kuwa ni watu wasiojulikana
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya ndio makosa na matokeo ya kuajiri watu wenye elimu duni kufanya kazi yenye kuhitaji kureason! Hata polisi wa kikoloni hawakuwa na ubazazi huu uliopo Sasa! Hakika, jeshi la polisi ni la kuvunjiliwa mbali na kusukwa upya kitaalaamu!
 
Naifananisha hii ishu na scenario ya Prof Assad. Mtu kaenda shambani simu haipatikani kuna mwanasiasa(kapuni) akasema ametekwa.

Kutekwa imekuwa kama mbinu ya upinzani kuipaka nchi matope. Japokuwa kuna tatizo pia namna gani polisi wanawakamata watuhumiwa. Labda hili nalo linaleta shida kwa wananchi.

Hasa ukiangalia Eric na wale jamaa wa lhrc walivyokamatwa inaleta picha mbaya.
 
Nionavyo Mimi hawa vijana wetu wanafanya fujo sana, hawafuati sheria wala utaratibu.

Mimi ninafikiria mamlaka hasa IGP awatangazie wananchi kwamba hawa watu wanapokuja kumkamata mtu wafuate sheria na utaratibu.


Ndiyo wakati mwingine mtu anakamatwa mjini sio nyumbani basi waoneshi vitambulisho na kuwaruhusu mtuhumiwa aongee na wakili wake kwamba amekamatwa na askali flani namba flani na anaelekea kituoni.


Kwa kweli huu ujinga ujinga umepitwa na wakati tena ni ushamba tu.

Wanapokataa kuonesha vitambulisho maana yake wanapoteza utambulisho wao, kwa hiyo wanakuwa hawana tofauti na majambazi, wezi na magaidi.

Je Jeshi la polisi linafuga magaidi?.


TUNAOMBA UFAFANUZI KWA IGP AU JESHI LA POLISI KUHUSU UTARATIBU WA KUMKAMATA MTUHUMIWA NA HAKI ZAKE KAMA RAIA NA HAKI YA POLISI KAMA AFISA MTIMZA WAJIBU.


Kwa kweli huu utaratibu wa kuja na madifenda na kuwakamata watu na kisha ndugu na jamaa hawajui walipo, baadaye kwa aibu mnakuja kusema mnawashikilia.

Tuanhisi Hofu

Tuanhisi hatuko salama.

Tunahusi kunyanyaswa.

Tunahisi jeshi letu halifanyi kazi zake kiutaratibu..



Any way tukikumbuka ya Tundu Lissu mpaka leo hakuna aliyekamatwa na wala hakuna kinachoendelea tunawaza kama Mbunge akiwa bungeni anapigwa risasi na Polisi wapo, Usalama wapo na hakuna kinachoendela.

Nachelea wananchi hatuko salama na hata nchi ipo mashakani.
 
Ni makada/waamini/ wafuasi wa chama gani cha siasa hapa Tanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…