Ali Nassor Px
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,433
- 4,043
(BASED ON A TRUE STORY)
Portion 1
Kuna baadhi ya matukio nikiyakumbuka mpaka leo najiona nilikuwa bonge la mpuuzi. Na naamini kabisa kama ingewezekana huyu mimi wa sasa kukutana na mimi wa miaka ile, Mimi wa sasa angempiga makofi mengi sana.
Nisikuchoshe usinichoshe directly kwenye story.
Ilikuwa miaka kadhaa iliyopita kipindi bado namiliki Nokia Obama ambayo baadhi ya button zilikuwa zimegoma kufanya kazi.
Kipindi hicho nilikuwa kwenye umri ambao akili yote ilikuwa imejaa wanawake na mapenzi.
Tatizo kubwa zaidi nilikuwa sina kazi, sina hela, wala maisha yaliyonyooka. Nilikuwa bado naishi kwa wazazi wangu, nalishwa nyumbani, na hata boxer nilizovaa zilikuwa zimenunuliwa na mama yangu.
Japo nilikuwa sina kazi, muda mwingi nilikuwa naupitisha kwenye library ya brother wangu mmoja hivi. Hapo ndipo nilikuwa napata buku tatu tatu za kula mihogo na vocha.
Na stress zilikuwepo kweli. Kipindi hicho girlfriend wangu wa secondary alikuwa ameniacha vibaya sana. Alinibwaga akaenda kudate na teacher aliyekuwa anatufundisha mimi na yeye. Kwa kweli niliumia sana, ila nilikuwa nifanye nini? Mimi mtoto wa mkulima.
Siku moja usiku baada ya kutoka library nikiwa nimechoka na mawazo mengi kichwani, nikakumbuka story za baadhi ya wanangu niliokuwa nafunga nao library.
Walikuwa wananiambia kuwa kuna vipindi vya radio vya usiku vinavyozungumzia mambo ya mapenzi na hata kutafuta wachumba. Unaweza kutuma SMS ukataja sifa za mtu unayemtaka, baada ya time mtangazaji atatangaza.
Basi siku hiyo nikawasha radio nikaweka volume kiasi cha kusikia mimi mwenyewe tu, maana nilikuwa bado naishi kwa wazazi wangu. Baada ya mtangazaji kutaja namba za kutuma SMS, haraka sana nikachukua simu yangu nikatuma ujumbe.
“Natafuta mchumba. Awe mweupe, mwenye elimu fulani, awe na mtoto mmoja tu. Ila kama ana watoto wawili basi wawe wa baba mmoja. Lengo ni kuoa.”
Leo nikikumbuka najiuliza ile confidence nilikuwa naitoa wapi. Mimi sina kazi, sina future plan ya maana, bado nalala kwetu, ila natafuta mke wa kuoa kana kwamba nishajipata hivi.
Siku ya kwanza message yangu haikusomwa.
Siku ya pili pia kimya.
Lakini siku ya tatu usiku, ghafla nikasikia tangazo langu linasomwa live redioni.
Aisee, ndani ya dakika chache simu yangu ikaanza kuita. Nikapokea kwa sauti nzito ya kujifanya mwanaume mwenye maisha yaliyonyooka.
Upande wa pili alikuwa mwanamke. Akajitambulisha vizuri, akanieleza anakaa wapi, halafu akasema ana mtoto mmoja aliyempata Morogoro. Kisha akaniambia
“Nimesikia tangazo lako redioni kuwa unatafuta mchumba wa kuoa.”
Mimi nikajibu kwa kujiamini
“Ndiyo, ni kweli natafuta mchumba wa kuoa.”
Kumbuka muda huo bado nalala kwa wazazi wangu, sina kazi wala hela ya kueleweka, lakini kichwani najiona husband material wa hatari.
Yule dada akaamini kabisa amepata mwanaume serious wa kumuoa, kumbe amepata kijana wa kubangaiza maisha ambaye hata matumizi yake mengi alikuwa anategemea nyumbani.
Usiku ule ule nikapigiwa simu nyingine tatu kutoka kwa wanawake tofauti. Wengine walituma mpaka meseji ndefu za kujielezea, lakini huyu wa kwanza ndiye niliempa attention zaidi.
Baada ya kuongea kwa dakika kadhaa, yule dada akaniambia
“Jina langu Naitwa Irene (Sio jina halisi), Wewe unaitwa nani?”
“Naitwa Mudrick”. Sikumtajia jina langu halisi lakini hata radioni pia nilijitambulisha kwa jina la Mudrick ili kutojulikana na raia wa mtaani ninaokaa.
Baada ya hapo Irene akasema.
“Mudrick, nahitaji tuonane.”
Na hakumaanisha mwezi ujao wala wiki inayofuata.
Alitaka tuonane kesho yake kabisa.
Aisee, hapo ndipo balaa lilipoanzia, Kwani mwanzo wa matatizo na majanga ndipo yalianzia.
Kusoma muendelezo gusa hapa 👇

Portion 2
Nakumbuka ilikuwa asubuhi tulivu sana. Nilikuwa nimepanga na Irene kwamba tukutane mida ya saa sita kwenye Stand X kwa ajili ya meeting yetu ya kwanza ya uso kwa uso.
Kweli bhana, baharia wa nchi kavu nikajikawai kinoma. Kama naenda kuposa familia fulani hivi ya wenye nchi. Kisha nikachukua baiskeli ya Faza — ile ambayo mara nyingi tunaitumia kubebea maji na mazao ya shambani — nikasepa nayo mpaka stand.
Mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kufika.
Nikajipigilia chobingo fulani. Lengo langu lilikuwa moja tu; kuhakikisha mimi ndiye wa kwanza kumwona huyo mwanamke niliyekuwa naenda...