Kimasihara masihara nikajikuta kwenye mahusiano na mwanamke mtu mzima

Kimasihara masihara nikajikuta kwenye mahusiano na mwanamke mtu mzima

Nina stress Leo kuna mishe yangu inakataa kusoma (maana hamchelewi kusema ni mapenzi) Ila imebidi nisome af ni smile
Pole sana mdada, kila kitu kitakuwa sawa, labla unaona imeshindikana hilo n kwa sababu kuna kingine kizuri zaidi kitakuja.

Subir japo labla itachukua muda mrefu

💪
 
Portion 2

Nakumbuka ilikuwa asubuhi tulivu sana. Nilikuwa nimepanga na Irene kwamba tukutane mida ya saa sita kwenye Stand X kwa ajili ya meeting yetu ya kwanza ya uso kwa uso.

Kweli bhana, baharia wa nchi kavu nikajikawai kinoma. Kama naenda kuposa familia fulani hivi ya wenye nchi. Kisha nikachukua baiskeli ya Faza — ile ambayo mara nyingi tunaitumia kubebea maji na mazao ya shambani — nikasepa nayo mpaka stand.

Mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kufika.

Nikajipigilia chobingo fulani. Lengo langu lilikuwa moja tu; kuhakikisha mimi ndiye wa kwanza kumwona huyo mwanamke niliyekuwa naenda kukutana naye.

Baada ya dakika kadhaa simu yangu ikaita.

Mpigaji alikuwa Irene.

Nikapokea haraka huku mapigo ya moyo yakiongezeka.

“Hello Mudrick, nimeshafika stand.”

Nikamuuliza haraka haraka: “Umevaaje?”

Bila hata kupepesa macho akanitajia dress code alizovaa.

Aisee… nilipogeuza macho huku na kule nikamuona.

Ilikuwa ni pisi age fulani mshangazi mwenye figure 8. Kwa sekunde kadhaa nilibaki nashangaa tu. Nilikuwa siamini kama huyu ndiye mtu ambaye nimekuwa nikichat naye usiku kutwa.

Ili kuhakikisha vizuri nikamwambia: “Hebu sogea pale kwenye kibanda cha wakala.”

Naye kweli akasogea.

Hapo ndipo nikapata uhakika kabisa kwamba yule niliyekuwa namtazama kwa mashaka ndiye Irene mwenyewe.

Sasa sijui nilitoa wapi ujasiri, ila baharia ikabidi ijitokeze rasmi. Nikaanza kukokota baiskeli taratibu mpaka karibu yake.

Nikamsalimia kisha nikasema: “Mimi ndiye Mudrick.”

Akanitazama kuanzia kichwani mpaka miguuni halafu akabaki kushangaa.

“Wewe ndiye Mudrick? Mbona unaonekana bado mdogo sana?”

Mimi kwa kujiamini ambako hata sikujui nilikotoa nikajibu “Hamna aisee, mimi mkubwa tu… na…”

Lakini kabla hata sijamalizia kujitetea, Irene akasema

“Ujue mimi nina miaka 39. Na kwa kukuangalia, sidhani hata kama miaka 30 umefikisha.”

Nikacheka kidogo halafu nikasema

“Kweli lakini miaka siyo kila kitu Irene. Watu wengi wakiniona hudhani mimi mdogo, lakini mpaka hapa nilipo maisha yashanichapa kuliko hata mtu mwenye miaka 50.

Kuna watu wana miaka mingi lakini mawazo yao bado ya kitoto, na kuna wengine umri mdogo ila wanajitambua na wana majukumu makubwa.”

Akanitazama.

Nikazidi kujitetea taratibu: “Halafu usinipime kwa sura. Kuna wengine ndevu zimejaa lakini akili sifuri. Mimi naamini kikubwa ni namna mtu anavyojielewa, anavyoongea na anavyomheshimu mwenzake.”

Irene akacheka.

Hapo ndipo hali ikaanza kuwa nyepesi kidogo.

Kisha akaniuliza: “Sawa haina shida… sasa tunaelekea wapi Mudrick?”

Kwa kweli kwa hali niliyokuwa nayo akili ilikuwa imegoma kufanya kazi. Nikamjibu

“Kwa sasa hata sielewi.”

Akanisogelea kidogo akasema

“Sikia… kwa hali niliyokuwa nayo siwezi kurudi nyumbani. Naomba tutafute lodge yoyote mimi na wewe tukapumzike pamoja.”

Aisee…

Moyo ulipiga “PAAAH!”

Kwa sekunde chache nilihisi kama dunia ilisimama.

Hili tukio lilikuwa halina tofauti na swala kujipeleka lenyewe mbele ya simba. Simba lazima aishie kuduwaa tu . Na mimi ndiyo hayo yalinikuta.

Tatizo kubwa lilikuwa moja.

Nyumbani nimetoka na baiskeli.

Mfukoni sina hata mia.

Halafu time hii mama mtu ananiambia twende lodge!

Nikamtazama kwa sekunde kadhaa nikifikiria nimjibu nini mwisho nikamwambia.

“Sawa haina shida… lakini kwanza itabidi nirudishe hii baiskeli home.”

Akaniangalia straight usoni halafu akauliza

“Sawa… tutaongozana eeenh?”

Wallahi hili swali ndilo lilizidi kunichanganya kabisa.

Anataka tuongozane ili iweje sasa?

Kwa mfano nikifika nae home… Mzee Dingi akitoka nje alafu anikute na mshangazi wa miaka 39 pembeni yangu, tena nimeshikilia baiskeli ya kubebea maji… nitajieleza nini?

Na Bi Mkubwa akimwona sindo kitakuwa kiama.

Kusoma muendelezo gusa hapa 👇

 
Kwa mfano nikifika nae home… Mzee Dingi akitoka nje alafu anikute na mshangazi wa miaka 39 pembeni yangu, tena nimeshikilia baiskeli ya kubebea maji… nitajieleza nini?

Na Bi Mkubwa akimwona sindo kitakuwa kiama.
Kabla hatujafika mbali. Ulilichapa limshangazi?
 
Back
Top Bottom