Portion 3
Nikiwa nawaza nifanye nini, mwisho wa siku nikaona bora nijitoe muhanga tu nimwambie ukweli.
Nikamwambia Irene
"Sawa, haina shida. Ila kwanza nirudishe baiskeli nyumbani, halafu tutaenda lodge."
Irene akaniangalia kwa sekunde chache kisha akasema
"Sawa."
Akapanda nyuma ya baiskeli yangu na safari ikaanza. Mimi nikawa napiga pedeli huku moyo ukidunda kwa kasi. Kwa upande wake Irene alikuwa ametulia kabisa, hana wasiwasi wowote.
Mpaka leo sijui nini hasa kilikuwa kinaendelea kichwani mwake. Ila kwa jinsi alivyokuwa ametulia, ilionekana kama alikuwa ameshapagawa na mapenzi. Nami kwa upande wangu nilikuwa makini sana. Kila step nilikuwa najiuliza kama kweli haya mambo yanayotokea ni ya kweli au ni ndoto.
Tulipokaribia nyumbani kwetu, umbali wa kama mita mia moja hivi, nikasimamisha baiskeli.
Nikageuka nyuma nikamwambia
"Shuka kidogo. Nisubiri hapa. Napeleka baiskeli nyumbani kisha nitarudi."
Akanijibu
"Sawa, lakini usichelewe sana."
Nikapanda baiskeli kwa kasi kuelekea nyumbani.
Nilipofika nyumbani nikakuta Bi Mkubwa anatoka jikoni.
"Aah, afadhali umerudi!"
Nikamsalimia
Lakini kabla hata sijakaa, akaniongeza
"Dukani maharage yameisha. Itabidi uende Pori ukanunue maharage."
Pori ni eneo ambalo lina mashamba mengi na wafanyabiashara wa mazao. Kutoka nyumbani kwenda huko na kurudi ni safari ndefu sana.
Bi Mkubwa akanipa shilingi elfu kumi na tano mkononi nikabaki nimesimama kama sanamu.
Nikajiuliza "Nikienda Pori, nitatumia karibu masaa mawili au zaidi. Na Irene ananisubiri."
Kwa upande mwingine nilijua pesa ile imekusudiwa kununua maharage.
Kwa kweli nilijikuta kwenye njia panda.
Dakika chache baadaye nikafanya maamuzi ambayo mpaka leo nikiyakumbuka huwa najicheka mwenyewe.
Nikaiacha baiskeli nje.
Nikachukua zile shilingi elfu kumi na tano.
Halafu nikarudi kwa Irene.
Aliponiona akaridhika kwamba sikuwa nimemdanganya.
Basi safari ikaendelea.
Moja kwa moja tukaelekea lodge.
Mambo mengine acha yabaki historia wakulu.
Cha muhimu ni kwamba siku hiyo tulikuwa pamoja muda mrefu sana.
Siku ya kwanza cost zote nilizibeba mimi.
Siku ya pili, kwa mshangao wangu, Irene ndiye aliyesimamia cost zotei.
Baada ya hapo nikahisi si sawa kuendelea kumficha ukweli.
Nikakaa naye chini nikamwambia
"Kuna jambo nataka ujue."
Akanitazama kwa makini.
"Ni jambo gani?"
Nikavuta pumzi ndefu. "Kwanza umri wangu si ule niliokuambia mwanzo. Pili, jina langu halisi si Mudrick."
Akashtuka.
"Kwani unaitwa nani?"
"Naitwa Ali."
Akanikodolea macho.
"Subiri kidogo. Kama unaitwa Ali, kwa nini ulijitambulisha kama Mudrick?"
"Aaah, Mambo mengi kidogo. Lakini pia ilikuwa kwa ajili ya kujilinda. Unajua radio wasikilizaji ni wengi sana. Si wewe peke yako. Kwa hiyo wakati mwingine unakuwa makini na taarifa unazotoa ili mambo yasiwe mengi."
Akatikisa kichwa.
"Sawa, nimekuelewa."
Baada ya ukimya mfupi akaniuliza swali jingine.
"Na kuhusu kuoa je? Mpango wako ukoje?"
Nikajibu bila kusita
"Mpango wangu wa kuoa bado upo pale pale."
Tuliongea mambo mengine machache, lakini mazungumzo hayakuchukua muda mrefu. Hatimaye kila mmoja akaanza kujiandaa kurudi kwake.
Lakini sasa tatizo kubwa lilikuwa upande wangu.
Nilikuwa najiuliza
"Narudi nyumbani kwa sura gani?"
Kwanza sikuwa nimeonekana nyumbani kwa siku mbili nzima.
Pili, nilikuwa nimetoweka bila taarifa yoyote.
Tatu, zile hela za maharage zilikuwa nimetumia kwenye matumizi tofauti kabisa.
Nilianza safari ya kurudi nyumbani huku moyo ukinienda mbio.
Kadiri nilivyokuwa nakaribia nyumbani, ndivyo hofu ilivyokuwa inaongezeka.
Nilipofika karibu na home nikaanza kutembea kwa kunyata kama mwizi.
Nilidhani ningeingia kimya kimya bila mtu kuniona.
Kumbe mambo yalikuwa yamefika mbali kuliko nilivyodhani.
Wakati mimi niko huko na Irene, nyumbani kulikuwa na taharuki kubwa.
Faza na Bi Mkubwa walikuwa tayari wamefika polisi kutoa taarifa kwamba nimepotea.
Majirani walikuwa wanajulishana.
Wengine walikuwa wanapiga simu kwa ndugu mbalimbali.
Hata Mwenyekiti wa mtaa alikuwa ameshafika nyumbani.
Walikuwa wanapanga jinsi watu watakavyogawanywa kwenye makundi ili waanze kunitafuta maeneo mbalimbali.
Mimi hayo yote sikuwa najua.
Nikaendelea kusogea taratibu.Ghafla nikasikia sauti kubwa.
"Aaaah! Ali mwenyewe si huyo hapo?"
Ilikuwa sauti ya Mwenyekiti. Alikuwa mtu wa kwanza kuniona kabla ya mtu yoyote.
Wote waliokuwa pale wakageuka kunitazama.Nikajua sasa nimeumana.
Bi Mkubwa aliponiona tu, machozi yakaanza kumtoka.
Faza naye akasimama ghafla.
Majirani wakaanza kusogea karibu.
Na hapo ndipo nikagundua kuwa
kwa siku mbili nilizokuwa nimetoweka, watu walikuwa wakihangaika kunitafuta huku wakidhani labda nimepatwa na jambo baya.
Lakini kumbe wangejua.
Kusoma muendelezo gusa hapa 👇
PORTION 4
Kitendo cha kuonekana na jinsi watu walivyopokea jambo lile kilinichanganya sana akili. Nilihisi kwamba sasa chochote kinaweza kutokea.
Sikumbuki hata mazungumzo yote yalianzaje, lakini jambo la kwanza nililosikia ni mwenyekiti akiniambia
"Kijana, kaa chini kwanza."
Kisha akamgeukia mama yangu na kusema
"Mama Ali, tafadhali tulia kidogo. Ukizidi kuwa na hasira utamchanganya huyu kijana."
Baada ya hapo maswali yakaanza.
"Siku mbili zote ulikuwa wapi?" waliuliza.
Nikavuta pumzi kisha nikajieleza.
"Nilienda mjini kuchukua movie mpya kwa ajili ya library."
Lakini maelezo...