PORTION 4
Kitendo cha kuonekana na jinsi watu walivyopokea jambo lile kilinichanganya sana akili. Nilihisi kwamba sasa chochote kinaweza kutokea.
Sikumbuki hata mazungumzo yote yalianzaje, lakini jambo la kwanza nililosikia ni mwenyekiti akiniambia
"Kijana, kaa chini kwanza."
Kisha akamgeukia mama yangu na kusema
"Mama Ali, tafadhali tulia kidogo. Ukizidi kuwa na hasira utamchanganya huyu kijana."
Baada ya hapo maswali yakaanza.
"Siku mbili zote ulikuwa wapi?" waliuliza.
Nikavuta pumzi kisha nikajieleza.
"Nilienda mjini kuchukua movie mpya kwa ajili ya library."
Lakini maelezo yangu hayakumridhisha mama yangu.
"Kwani unaenda mjini bila kuaga? Wewe mtoto unataka nife presha ndo ulizike?" aliongea kwa hasira.
Nikainamisha kichwa.
"Samahani mama, sikukusudia."
Kwa kweli siku hiyo mwenyekiti alijitahidi sana kumtuliza mama yangu. Wakati huo Faza alikuwa amenikazia macho kwa hasira kali sana. Nilijua kabisa kwamba asingekuwa mbele za watu, angeniua.
Baada ya mazungumzo yale hali ilianza kutulia kidogo. Siku ikaendelea kama kawaida.
Lakini changamoto kubwa haikuwa nyumbani kwetu.
Changamoto ilikuwa kwa Irene.
Nilianza kugundua kwamba mimi na Irene tulikuwa tunaangalia uhusiano wetu kwa namna tofauti. Mimi nilichukulia mambo kawaida sana, lakini yeye alionekana kuyachukulia kwa uzito mkubwa.
Kadiri siku zilivyopita nilianza kumpa nafasi ndogo. Mara nyingi nilikuwa sipokei simu zake wala kujibu ujumbe zake kwa wakati.
Baadaye niligundua kwamba jambo hilo lilikuwa linamuumiza.
Nakumbuka siku moja nilikuwa library muda wa mchana.
Simu yangu ikaita.
Nikatazama nikaona ni Irene. Sikupokea.
Baada ya dakika chache akapiga tena.Sikupokea.
Akapiga mara ya tatu, bado sikupokea.
Baada ya kuona sipokei, akanitumia message .Nilipoufungua ilisomeka
"Endelea tu kutopokea simu zangu. Lakini nakwambia jambo moja, kesho nitakuja kwenu kujitambulisha mwenyewe."
Niliposoma message yake nilicheka,niliweka simu pembeni na kuendelea na kazi zangu.
Nilijua ni maneno ya hasira tu.
Kwanza, Irene hakuwahi kufika nyumbani kwetu.
Pili, niliamini hana ujasiri wa kufika mbele ya wazazi wangu na kusema wazi kwamba mimi ndiye mtu anayenipenda.
Kwa hiyo sikuipa uzito wowote ile message yake.
Lakini kumbe nilikuwa nimekosea.
Siku iliyofuata ilikuwa Jumapili.
Siku hiyo sikwenda library. Nilikuwa nyumbani tu, nikiwa chumbani kwangu.
Time ya asubuhi ghafla nikasikia sauti ya mtu akigonga mlango.
"Hodi!"
Nikatega sikio kusikiliza.
Kabla hata sijafanya maamuzi yoyote, mama alikuwa tayari ameitikia.
"Karibu!"
Wakaanza kuzungumza.
Niliposikia sauti ya mgeni, moyo wangu ukaanzs kwenda mbio.
Nikajiuliza
"Inawezekana kweli ni Irene?"
Ili kujiridhisha nikatoka chumbani.
Nilipofika sebuleni nilikuta jambo ambalo sikulitegemea hata kidogo.
Mlangoni alikuwa amesimama Irene.
Wakati huohuo baba yangu naye alikuwa anatoka chumbani kwake.
Kwa sekunde chache tukajikuta watu wanne tumetazamana kimya.
Mimi, Mama, Baba na Irene.
Nilihisi kama moyo wangu umesimama kwa muda.
Irene naye alionekana kuchanganyikiwa kidogo. Ujasiri wote aliokuwa nao ulionekana kupotea ghafla.
Badala ya kujitambulisha, akaanza kuulizia chumba cha kupanga.
Baba yangu akaamua kwenda na mchezo ule.
"Chumba kipo, lakini pesa ipo?" akauliza kwa utani.
Irene akacheka kwa aibu.
"Ndiyo baba, pesa ipo."
Wakaanza kuzungumza kuhusu bei ya chumba.
Mwisho wa mazungumzo Irene akatoa pesa na kulipa hapo hapo.
Kisha akasema:
"Kwa sasa naondoka. Lakini baada ya siku chache nitarudi na vitu vyangu ili nihamie rasmi."
Baada ya kusema hivyo akaondoka.
Mimi nikabaki nimesimama nikiwa sielewi kilichokuwa kimetokea.
Siku ya kwanza ikapita.
Siku ya pili ikapita.
Siku ya tatu nayo ikapita.
Lakini Irene hakuonekana tena.
Nilianza kujiuliza maswali mengi.
Je, alikuwa anatania?
Au kuna jambo lilitokea njiani likabadilisha mipango ya
ke?
Majibu ya maswali hayo sikuwa nayo.
Nilichokuwa najua ni kwamba ukimya wake wa ghafla ulianza kunitia wasiwasi mkubwa...
ITAENDELEA…