Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
True ila sasa ukiwa unatumia baby walker halafu anapita bwana mdogo tena nlulie mgepu umri anaendesha subaru, prado, Mitsubishi, au hata Harrier tu SUV kubwa dah unaona hata mamsapu hapo pembeni anakutazama jicho la dah we nae si ujichange tupate hiyo kubwa. Haka tuna aibika ujue.Noma sana!...ila gari ni gari inategemea pia interest ya mtu
[emoji23][emoji23][emoji23] umenikumbusha. Eeeeewaaa. Kitaulo , vinakuwa viwili kimoja cha kufutia mikono michafu lakini kimoja kinakuwa kisafi cha kufutia vioo na dashboard. Sharti viwe bi vya pamba sio vya Sufi.Leso ya kusafishia dashboard hua haikosekani
Na hamna kitu kinawaumiza madereva wa Passo na vitz jinsi watu wanawachapa mkiwa safariniTrue ila sasa ukiwa unatumia baby walker halafu anapita bwana mdogo tena nlulie mgepu umri anaendesha subaru, prado, Mitsubishi, au hata Harrier tu SUV kubwa dah unaona hata mamsapu hapo pembeni anakutazama jicho la dah we nae si ujichange tupate hiyo kubwa. Haka tuna aibika ujue.
To be honest I was wondering!, How that possible!?, ulipoandika hivi ndo nikaelewa kumbe, when you start driving at early age, huwezi kua hivyo bcoz owning a car inakua kitu cha kawaida sana, tho unakua happy ku own your dream car lakin not that much😆..... by the way I started driving at 15 years na nilikua naend popote napotaka, some of my friends walikua wanaenda secondary school na gari, so today..even if niki own Buggati I don't think nitakua hivyo, zaidi yakuwa proud of myself to own a such expensive car in the world. Sijui kwann Mimi huwa I get bored easily naweza furahia kitu kwa muda mchache sana after that naona kawaida ama nisione thamani yake tena 😟 so sad.Ndo maana wazungu wana utamaduni watoto wao wakitimiza miaka 16 anampeleka driving school. Akipata leseni mzazi anamnunulia mtoto gari ya kuanzia maisha.
Ile inawasaidia vijana kuwa confidence kumiliki na kutumia gari kwa utulivu. Yaani akija nunua gari anakuwa very confident kuitumia na comfortable.
Bongo mzee akununulie gari sijui labda awe ni kibopa au tajiri sana.
Iko siku mkuu utanunua kikubwa ndoto iendelee kusimama.Hahahaaa hapa kama umeniona, nishaandaa list ya nyimbo na uwezo wa kununua kwa sasa sina lakini najua one day yes. Nawaza siwezi acha weka mafuta full tank
Hapo kwenye mbu nimecheka, ila furaha ya gari hata mbu sitowasikia😂Kulala ndani ya gari lazima, ila mbu utawakoma[emoji16]
Ombea ndinga kali zaidi sio IST banaa[emoji2960][emoji2960]
Tunakuombea mkuu utimize haja za moyo wako.Haaha siku nikija nunua gari nahisi day 1 ntalala ndani ya gari[emoji23][emoji23] pia kuiacha gari nje mimi nilale ndani sijui kama usingizi utakuja. Hongereni wote mlioweza kuwa na magari. Napenda IST new model iwe gari yangu ya kwanza[emoji14]
Nasisi tunapenda mkuu, ila mimi na huu uoga huwa nawaza hivi hii Dar hizi vurugu ntaweza kweli kuendesha, naonaga watu wote wako rough barabarani 😂Utapata ni swala la kuweka mkakati tu. Ila wanawake magari ni sehemu ya passion yenu kweli au mnatuiga wanaume?! [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sisi gari ni kama samaki na maji, hiyo ni miaka yote.
Ameeen ahsante mkuu 😍Tunakuombea mkuu utimize haja za moyo wako.
Hiyo namba 11..Gari ya kwanza ni kitu personal sana kwa wanaume. Ni kitu personal ambacho ni ndoto ya jinsia hii ya kiume kama vile kwa mwanamke kuwa na ndoa au familia yake na mumewe.
Gari ni ndoto halisi nay a asili ya kila mwanaume ingawa wapo ambao hawana sana mzuka wa kuwa nazo ila ni kutokana na makuzi na life style aliyopitia muhusika.
Gari ya kwanza kumiliki (sio gari ya kuazima) huja na aina ya kipekee sana ya nguvu za kiume ambazo humfanya mwanaume kujiona wa ziada akilinganishwa na wenzake hata kama nao wana magari kama yeye.
Inawezekana ulishamiliki gari awali ambayo si ya mapenzi yako wakati ukisubiria kupata pesa au uwezo wa kupata gari ya ndoto zako yaani ile gari inayoongeza mapigo ya moyo wako au pisi kali yako,hii ndio nazungumzia hapa sasa.
Gari ya kwanza humfanya muhusika kupata wehu fulani ambao huamsha aina fulani ya sifa na mbwembwe ambazo kama mtu si muelewa utabakia kusema huyu jamaa anadharau sana au anajiona au ana misifa sana. Katika maisha yetu,wale wamiliki wa magari private utagundua kunakupitia hali fulani ambayo inakufanya ubehave tofauti na kawaida.
Sio wote ila wengi wao hujikuta na hiyo hali. Kuna vituko hufanyika kuanzia pale mtu amepata pesa ya kununua gari ya kwanza, amepata zawadi ya gari au kununuliwa, hadi anapoanza litumia kwa mara ya kwanza. Bila kujali brand ya hiyo gari kama ni Toyota,Nissan, BMW,VW,Subaru etc huwa kuna kamzuka huja na watu hujikuta wanabehave tofauti na kawaida.
Katika huu uzi tutashare experience hizo bila kujali nani atajiskia vipi au atasema nini kwasababu kwa waelewa wataelewa nini huwa kinatokea. Nitaongelea baadhi ya experience halafu wengine watajazia zao pia kama ifuatavyo;
1. Muda unakuwa hauendi siku wakala akikuambia gari imefika anamalizia paperwork ili ukalichukue. Unampigia simu kila wakati ili akambie kafikia wapi na kama kuna changamoto yoyote ambayo itakwamisha gari kutoka kwa wakati.
2. Unatamani gari yako ifungiwe kwenye kontena wakati inasubiria clearance ili majizi wanyakua vifaa wasilione wala kuligusa.
3. Unajiapiza hii gari haitakuja itembee na half tank utakuwa unaweka full tank masaa 24 na siku saba za wiki. Na ni kweli gari ikifika na ukaanza iendesha kwa mara ya kwanza huwa unachukia sana kuona mshale wa mafuta au bar ya mafuta ikishuka unataka isome full muda wote.
4. Lazima uwashe A/C muda wote ile mara ya kwanza bila kujali maswala ya madereva wengine kusema inakula wese yaani utaitumia kibabe sana kama kibopa.
5. Bao la kwanza kwa trafiki kwa makosa madogo madogo kama kutokuvaa mkanda,kutokuwa na triangle au kuvuka na taa unakuwa tayari kutoa hela nyingi hata 20,000/= au 40,000/= utatoa tu bila shida yoyote kinyume na madereva wengine kwababu tayari wewe ni mtu muhimu sana mjini sababu ya gari so hauwezi kuonekana dhaifu kizembe.
6. Unaweza lala ndani ya gari, mimi nililala ndani ya gari hadi asubuhi na sikusinzia ile fofofo nilikuwa nalala kisungura maana kuna muda paka walikuwa wanaleta ufala sikuwa nataka gari iguswe kizembe. Hii ni kwasababu nilikuwa so connected na gari kiasi kwamba nikawa naliona kama living being ambapo kuliacha nje nikaona ni bonge la usaliti.
7. Usafi huwa ni kiwango cha Serena gari inaweza pelekwa car wash hata mara 4 kwa wiki na kupigwa ule usafi wa pro max yaani nje ndani, uvunguni, na kwenye engine kote. Na katika kitu cha kwanza utanotice kitakukera ni pale mtu anapoingia katika gari na kugusisha kiatu chake pale katika kizingiti cha lango na kupachafua kama na kuacha alama ya vumbi au tope hii nimenotice huwa inakera sana wamiliki wa gari ya kwanza.
8. Kuhusu swala la mziki, unakuwa ulishaandaa list ya nyimbo za kusikiliza kwa kwenye gari na ziliandaliwa hadi flash ya kuwekea.
9. Mtu akiingia ndani ya gari anatakiwa awe bubu muda wote na asikwambie lolote kuhusu gari yako maana ni yako pekee yako hakukusaidia kununua so hawezi kupangia matumizi.
Mbaya zaidi asijekutokea mtu akaomba kukuazima gari eti anakwenda nayo sehemu dah hiyo inakuwa kama mtu kukwambia naomba mkeo leo akalale kwangu mke wangu kasafiri naogopa kulala pekee yangu. Gari inakuwa nimeshikana na roho.
10. Wauza vitu vya magari pale barabarani watakukoma maana kila wakijileta na kukugongea hautawapuuza kuona wamebeba nini kwaajiri ya gari yako hautakosa cha kununua.
11. Hauta ona shida kumpeleka mtu popote pale atakapokuwa anataka kwenda hapa mjini ingawa ukishazoea baadae hii kitu itakufa na utajionea kero tulabda kama atakuwa ni baba, mama, mkwe,mke au shemeji au mchepuko nje ya hapo upo radhi kumpa pesa ya boda boda au ufunguo aende anapotaka. Kwakifupi hapa utatafutiza safari ili tu upate sababu ya kutekenya gari na kuiendesha.
12. Ufunguo wa gari yako utakuwa ni kama nyara ya serikali kiasi kwamba hata bafuni utaingia nao sababu ya kuogopa gari isiguswe na mtu mwingine hata mwizi.
13. Utatamani upate muda na eneo zuri za kuiendesha gari yako bila kero za foleni na madereva wengine. Mimi huwa nafanya night cruise yaani naweza toka mida ya saa nne usiku au tano naanza kuzurura mitaa ya Dar mfano kutoka tabata hadi mwenge, naingia bagamoyo road naenda hadi salenda nachapa ya cocobeach hadi penisula narudi tena hadi posta mpya naenda mitaa ya posta hadi mnazi, narudi na nyerere hadi kinyerezi. Kesho tena naanza na sinza kwenda kawe etc hadi nizoee gari.
Kwa muda huo barabara zinakuwa ni nyeupe hazina magari mengi na unaendesha kwa speed yako utakayo mradi kuchukua tahadhari tu usikutane uso kwa uso na madereva walevi wakajaa kwako.
Haya ni baadhi ya mengi ambayo hutokea katika umiliki wa gari ya kwanza. Wajumbe wengine mtakumbuka mbwembwe za umiliki wa gari ya kwanza so please share ili wengine wakumbuke au wajifunze na kujua yajayo kama MUNGU atawawezesha kumiliki gari kwa mara ya kwanza.
Mkuu upo kabsa!? naomba tutaftaneAmeeen ahsante mkuu [emoji7]
Uliyegundua automatic tech kwenye magari agiza kilo mbili na mafungu matano tafadhali.Kabisa. Manual ni technology ya kizamani na gari za sasa za auto zinazidi kuboreshwa Kuna AT, AMT, IMT, CVT, DCT.
Sasa ya nini kujitesa na kuendesha gari hadi miguu inauma. Ndo maana madereva wa zamani viuno ilikuwa shida maana wanakaza tako safari nzima.
Duh ok mkuuHizo ni Ist new model mkuu, zina range bei 17 mil to 21 mil mpaka unaipata mkononi.
[emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787][emoji1787] haahaaaTrue ila sasa ukiwa unatumia baby walker halafu anapita bwana mdogo tena nlulie mgepu umri anaendesha subaru, prado, Mitsubishi, au hata Harrier tu SUV kubwa dah unaona hata mamsapu hapo pembeni anakutazama jicho la dah we nae si ujichange tupate hiyo kubwa. Haka tuna aibika ujue.