Madam punguza hayo maneno,unajua wengi tuliohumu hatujuani kila mtu kaja hpa anajua lililomleta na ukihisi mmoja wapo kakukwaza au kakwambia maneno iwe kweli au sio kweli tuchukulie kma changamoto tu za kujuana na watu kwani hya hta mitaani hutokea.
Maneno mengine huweza yakakujenga na mengine kukubomoa linalohitajika ni kupima kati ya hao mawili na kuamua ila sasa mmoja kaambiwa mwengine akaanza kurusha maneno ambayo hyapendezi halaf mkijiangalia watu wazima sio,naamini wapo ambao wanasoma na hawaridhishwi na mambo mnayoyafanya hpa.
Skuiz matusi yalishapitwa na wkti tueni watu wazima mambo madogo tu hya.
Wewe wasema.
Ungelijua tangu awali wala usingefika hapa.
Kila siku nasema, usiichukulie Jf serious, usiifanye Jf kuwa ndio kila kitu chako.
Kuna vitu vingine huwa vinakera na kukwaza.
Mimi hapa, ningekuwa nachukua vitu serious nadhani leo hii ningekuwa siongei na members karibu wote, ila huwa inakuwa ni ubinadamu na kustahamiliana tu.
Mangapi tunakwazika, mangapi wanaume mnatusema ila tunachat, tunacheka na tunafunga mjadala.
Ila sasa huyu jamaa yako naona mambo kayabeba juu juu na u-serious juu.
Afu sasa kafika katikati kajikuta kapotea njia.
Mimi formula yangu ya maisha iko hivi, mtu akini-attack kwa minajiri ya kunidhalilisha huwa siangalii kama hapa kuna nani au nani, napunguza hamu zangu kisha tunaendelea.
Msitumie utu uzima wetu kutuweka hatiani.
Sina utu uzima huo wa kupiga msamba juu ya nyaya za umeme.
Nina utu uzima wangu wa kumuheshimu kila mmoja.
Ila linapokuja suala la kukashifiana, huwa sinaga msalie mtume kwa kweli.