Hawa wabunge 19 wanamaliza muda wao , je watarudisha pesa zetu walichuma isivyo halali pale bungeni ? , nini kifanyike ?
Hao wabunge ni wabunge halali wa Bunge la JMT,na hayo malipo,ni malipo yao halali na mimi hili niliwaeleza Chadema wenyewe kule kijiweni kwangu,
CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao nilisema “Wanabodi,
huu ni ushauri wangu kwa Chadema, Its do or die! Chadema is left with only two options, kuchagua kufa, au kuchagua kuendelea kuishi. The choice is theirs.
Ili CHADEMA kiendelee kuishi ni lazima kiukubali ukweli, kikubalini matokeo ya uchaguzi, kiendelee kuvuta ruzuku and survives, or kiendelee kushupaza shingo, kuwa hakiyatambui matokeo ya uchaguzi, hakimtambui rais wa Jamhuri ya Muungano wa hakilitambui Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, then CHADEMA will be succumbed to death by poverty and just go straight to hell by being buried 6ft Under!.
Mbele ya macho ya jamii, hao ambao kwao ni wasaliti, kwa wengine hao ni makamanda mashujaa wapambanaji ambao ni wa kiwango cha makomandoo, ambao wameipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, na licha ya kufutwa uanachama wa CHADEMA, wataendelea kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ubunge wao sasa utakuwa ni ubunge wa Spika, Ubunge wa Taifa.
A Way Forward Kwa Chadema
Kwa vile wabunge hao wameisha apishwa ni wabunge halali wa Bunge la JMT, hata kama Chadema imewafuta uanachama, ni mambo ya ndani ya chama, kama ni kweli Chadema haiyatambui matokeo ya uchaguzi, then hao wabunge 19 wa Chadema, hawahitaji kukata rufaa popote, wala kwenda mahakamani kupinga chochote, kwasababu Chadema haiwezi kufanya chochote. Sasa wataendelea na ubunge wao kama wabunge wa Taifa wa Chadema.
Chadema wakiamua kuacha ujinga wa kujifanya hawayatambui matokeo, wakiyatambua matokeo, watavuta ruzuku, wata survives ila zoezi hili lina changamoto moja kuu,wameisha kopeshwa mkopo wa magari unaolipwa ndani ya miaka 5!.
Nini Kifanyike, A Way Forward Kitaifa
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini kwenye siasa zetu, haiwezekani kiongozi achaguliwe na umma wa Watanzania, halafu chama chake kwa sababu za kijinga jinga tuu, kimvue uanachama, ili Tanzania tupate maendeleo ya kweli ya kisiasa, ni lazima tubadilike, sheria za kijinga jinga zenye masharti ya kijinga jinga lazima tuzibadilishe.
Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya na nchi nyingine zenye kuheshimu demokrasia ya kweli na sio hii demokrasia fake ya vyama!.
Tubadili Katiba yetu na sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na wagombea binafsi.
Tuibadili Tume yetu ya Uchaguzi iwe Tume huru zaidi na shirikishi, tujenge uwanja sawa wa ushindani wa haki kwa vyama vyote, uchaguzi uendeshwe kwa transparency ya hali ya juu kwa kuruhusu mawakala hadi kwenye tallying, na vyama au taasisi zozote ziwe free kuwa na tallying centers zake, kitu ambacho hakitaruhusiwa na talling centers hizo ni kutangaza matokeo, kama matokeo yote ya uchaguzi hadi wa rais yanahesabiwa kituoni na kubandikwa ukutani, kama hakuna jambo lolote la kificho, yaani nothing to hide, kwanini uzuie independent tallying?!. Uchaguzi wa 2025, kila mwenye uwezo wa kufanya tallying aruhusiwe afanye ila zisitangaze matokeo, hii itazuia bao la mkono!
Hitimisho
Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa na kufanya siasa za ukweli, naamini kabisa rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, anaweza kuleta maendeleo ya kweli ya taifa letu la Tanzania kwa kuleta maendeleo ya kiuchumi na wakati huo huo akiiacha demokrasia ikishamiri.
Nawatakia Jumanne Njema.
”
P