Kina Mama wawafunze mabinti kubalance Elimu, Career, Ndoa, Uzazi. Complications za Uzazi,Ugumba, ndoa migogoro zimekuwa nyingi sana

Kina Mama wawafunze mabinti kubalance Elimu, Career, Ndoa, Uzazi. Complications za Uzazi,Ugumba, ndoa migogoro zimekuwa nyingi sana

Basi Ile solution ya watu WA pwani itumike ...waolewe mapema ...huku wanaendelea na shule...
Sheria yetu ya ndoa ya 1977 inasemaje kuhusu umri wa kuolewa? Sheria za kumtambua mtoto zinasemaje? Kuna contradiction za kisheria... kuna changamoto za kimtaala kuhusu aina na malengo ya elimu tunayotoa, kipindi cha nyuma kulikuwa na masomo kama sayansi kimu...
inahusisha lishe na mapishi, ushonaji na shughuli za nyumbani kwa ujumla wake. Kulikuwa na sayansi kilimo pia self-reliance iliwajengea uwezo wanafunzi kufahamu kujitegemea baada ya std 7. Leo hii yako wapi? Tuna JKT ambayo tunaamisha watoto kujifunza kujitegemea na uzalendo within 3mnths kweli?

Na bado hata hiyo wazazi wengi wanaojifanya kuwapenda kinafiki watoto wao hawawapeleki jeshini eti watateseka. Unajiuza akipata kazi mkoani inakuwaje? Enzi hizo nilienda Mgambo JKT Tanga nimepiga mwendo wa kunyakua miezi 6 akili ilikuwa imara.

Point yangu ni nini?.... jukumu la kusaidia taasisi ya ndoa kuwa imara ina viungo vingi ambavyo vinategemeana. Kwa sasa tuna modernization theory ambazo impact yake ndio hii ya sasa mwanamke anaamini anaweza kila kitu bila mwanaume even to opt surrogacy hata kama hana shida ya uzazi.

Jukumu letu kama jamii ni kusema bila kuchoka ili tukiokoe kizazi kinachoacha asili yake na kung'ang'ania usasa unaowapoteza. Kuna mambo mazuri ya kuiga sio vibaya kuyachukua lakini yale yanayo ondoa asili, mila na desturi zetu nzuri nikuyapuuza.
 
Mademu Kama mademu waachwe tu, hata usimamie mifumo watatafuta njia ya kutokea.
 
Back
Top Bottom