Habari wadau,
Wale wenye maduka ya bidhaa za rejareja (mangi) tukutane hapa tubadilishane mawazo kidogo, tujadili ili kila mmoja aiweke biashara yake kwenyw kipimo kwa kulinganisha na wengine ili tuweze kuboresha zaidi.
Binafsi sina duka ila nna kijiduka au kibanda nilichokianza baada ya kupoteza kazi yangu niliyokuwa nayo mwanzo,
Wakuu mi nitagusia mambo yafuatayo;
1. Mauzo.
Hapa tujue mauzo ya kawaida kwa siku.
Mimi binafsi siku hazilingani, siku za j3 na j4 mauzo hushuka sana na kufikia angalau 120K kwa siku. Siku zingine hupanda kidogo mpaka kwenye 170, 150,... Siku za jmos na jpili mauzo hufika laki mbili au zaidi kidogo kwa siku.
2. Ushindani.
Hapa wakuu tushee picha halisi ya mazingira tunayofanyia biashara, na unakabiriana vipi na changamoto ya ushindani.
Binafsi mi nilipo nilikuta maduka mawili, mimi nikawa wa tatu. Mmoja wetu ana duka na genge, hivyo wateja wengi hupenda kwenda pale kwa sababu wanapata huduma zote kwa pamoja. Mi niliona nifanye tofaut, nikamix bidhaa za kawaida na nyingne kama baadhi ya vifaa vya umeme (taa, holder,..) Makufuli, etc.. maana niliona huduma hizi hakuna hapa mtaani, imenisaidia kufanya nizoeleke maana wateja wengine huja kufata vitu hivyo baada ya kuvikosa kwa hawa wenyeji.
3. Imani.
Wengi uhuhusisha hizi biashara na imani za kishirikina, na huenda sana kwa waganga kutafuta kitu kinachoitwa mvuto au king'amuzi.
Binafsi naamini hayo mambo yapo na watu wanachangamsha sana biashara zao kupitia mambo haya. Lakini mimi sijawahi kujihusisha na sina mpango sababu mambo haya huchukua hela nyingi na ukishayaanza ni ngumu kuacha. Vile vile mwisho wake mara nyingi sio mzuri.
Je nyie wadau mnalichukuliaje suala hili? Je wewe huwa unaenda?
4. Faida. Je hii biashara ina faida? Na ni kiasi gani? Unaijuaje au unaiona kwa namna gani hiyo faida?
Binafsi huwa sicomplicate, kila siku nachukua elf 20 naweka akiba. Haijalishi nimeuza kiasi gani.
Chakula cha kupika kinatoka dukani pamoja na mahitaji mengine, (hiyo yote ni faida). Lakini ninatoa kwa umakini sana. Na biashara yangu haijawahi kurudi nyuma, zaidi naongeza bidhaa mpya na kupanua kidogo kidogo.
Nawakaribisha wote wenye biashara ya namna hii tujadili, tubadilishane uzoefu, tufundishane, tufunguane, tunaeza pia kugusia na mengine zaidi kama namna ya kununua bidhaa, sehemu za kununua na mengine mengi.
Karibuni.