What?? Hivi unadhani Leo ni 1st April? Umewahisha hiyo kauli kuhusu Professa mstaafuWanaCCM tumeshaeleza wazi kuwa hatuna shida na vijimisaada vyenye masharti. Hili hata mstaafu Kikwete alilizungumza na sasa rais Dkt Magufuli anazidi kulikazia.
Hata nusu ya fedha za Japan, EU, china hurudi kwa mataifa husika, jambo hilo liko wazi. Wala siyo hao US pekee, na watoa misaada na mikopo wote. Au hujui Wachina wafanyavyo?!Hivi unajuwa zaidi ya nusu ya fedha za MCC hurudi US?..Hivi unajuwa kauli ya Raisi kukataa kuongeza mikataba kwa Syimbion ni sababu ya kusitish?...Hivi unajuwa US hupata faida ya hadi mara tano ya kila dola anayotowa?..hivi unajuwa kampuni binafsi za kimarekani zimepata pigo?...Hivi unajuwa US/EU na vibaraka wao wa ukawa kwa pamoja walishindwa uchaguzi?...Hivi unajuwa kwamba Luwasa aliingia mikataba ya siri na serikali za kimagharibi wakiamini angepitishwa na CCM...na hata wamefadhili kampeni zake?
Gamba, hili la kura za Muungano mbona nilishajibu wakati ule ule wa Uchaguzi. Hakukuwa na hoja hapo kwa sababu hizi ni chaguzi mbili tofauti. Tafadhali rejea posti zangu za wakati ule. Tatizo ni kuwa tunataka kuaminishwa kuwa kwa vile wapinzani wamedai basi ni kweli. Kama mantiq unayofuata ni kweli basi wakati ule ule wao wangeenda hata mahakamani kupinga kufutwa kwa uchaguzi wakipinga madaraka ya Jecha; hawakwenda na wao hawakushtakiwa... siasa za Zanzibar hizo.Kama hayo unayoyasema ni Ukweli wenye kupanga njama za kuiba uchaguzi wangekuwa Lupango sasa hivi, hizo unazozisema ni conspiracy theory!
Eti kwa kuwa Zanzibar walielekea kushindwa, wakifuta uchaguzi unaona sawa kwa kuwa " Waliiba".
Lakini kumbuka hata huko Zanzibar kuna kura za Raisi wa Muungano, Nikuulize swali, Je nazo waliiba ngapi?, Iweje basi waiba uchaguzi wa huko Zanzibar ambao kimsingi ni walewale tu wa nchi nzima waibe za Raisi wa Zanzibar lakini wasiibe na kura za Muungano kwa upande wa Zanzibar?
Vipi uchaguzi wa Raisi wa Muungano na Wabunge kwa huko Zanzibar uwe sahihi kwa muktadha huo?
Hautakiwi kulialia au kushangilia misaada...akikupa masharti ya kipuuzi kama US unapiga chini!Hata nusu ya fedha za Japan, EU, china hurudi kwa mataifa husika, jambo hilo liko wazi. Wala siyo hao US pekee, na watoa misaada na mikopo wote. Au hujui Wachina wafanyavyo?!
Yaani Mkuu unatumia nguvu sana Ktk issue simple! Iko Hivi; Hapa hatubishani kuhusu kujitegemea, Hilo liko wazi, NI LAZIMA TUJITEGEMEE! Lakini hoja inayopingwa hapa Ni sababu zilizopelekea mpaka tumefikia hatua ya kuwaza kujitegemea! Hebu ona Huku tunakataa ya MCC Huku tunapokea billion 6 ya kijapani! Huoni hapo kuna unafiki wa kupitia mgongo wa kujitegemea ili kuzima hoja Za kusigina katiba ya Zanzbar?Hapo sasa angalau ubongo umeanza kufanya kazi; kila mmoja anatakiwa kuwa na mawazo ya namna gani tunaweza kujitegemea, siyo kusema hatuwezi. Hivi kesho MCC wakiamua kurudisha misaada yao na mambo ya Zanzibar hayajabadilika si mtageuka kinyume nyume tena?
US katoa masharti gani ya kipuuzi, tuanzie hapo kwanza!Hautakiwi kulialia au kushangilia misaada...akikupa masharti ya kipuuzi kama US unapiga chini!
Ya kutupangia sheria gani itungwe na pili kulazimisha kuwa Seif kashinda kwa kauli yake tu,yaani demokrasia ni Seif kushinda....kama huo ndio uliberali wawachukuwe ukawa wakafanye nao huo upuuzi.US katoa masharti gani ya kipuuzi, tuanzie hapo kwanza!
Hakuna issue ya kuitwa "free lunch Mkuu" Kila msaada unamasharti Yake Na mostly inalenga maslahi ya mtoa msaada! Nikuulize tu, kwanini hii hoja hamkuileta Kabla ya MCC kutoa msimamo wao?WanaCCM tumeshaeleza wazi kuwa hatuna shida na vijimisaada vyenye masharti. Hili hata mstaafu Kikwete alilizungumza na sasa rais Dkt Magufuli anazidi kulikazia.
Wapi wamesema mtangaze Kua Seif Kashinda? Weka ushahidi hapa mezani?Ya kutupangia sheria gani itungwe na pili kulazimisha kuwa Seif kashinda kwa kauli yake tu,yaani demokrasia ni Seif kushinda....kama huo ndio uliberali wawachukuwe ukawa wakafanye nao huo upuuzi.
Yaani Mkuu unatumia nguvu sana Ktk issue simple! Iko Hivi; Hapa hatubishani kuhusu kujitegemea, Hilo liko wazi, NI LAZIMA TUJITEGEMEE! Lakini hoja inayopingwa hapa Ni sababu zilizopelekea mpaka tumefikia hatua ya kuwaza kujitegemea! Hebu ona Huku tunakataa ya MCC Huku tunapokea billion 6 ya kijapani! Huoni hapo kuna unafiki wa kupitia mgongo wa kujitegemea ili kuzima hoja Za kusigina katiba ya Zanzbar?
Kama Kweli tuko serious tunataka kujitegemea tuwarudishie wajapani yen Yao! Kinyume Na hapo Ni ujinga kushabakia hoja ya kujitegemea Wakati hatupo tayari!
Mkono wa kulia unakataa unasema nataka kujitegemea mkono wa Kushoto unapokea unasema Asante sana! Hizo Ni akili Kweli? Na Mungu alivyo waajabu analeta mambo yote hayo Kwa Wakati Mmoja ili kutuumbua!
Kwa nini hutaki kujibu hoja zao za kusitisha huo msaada?Utajiandaa vipi kujitegemea wakati hata kufikiria kujitegemea hutaki? Utaweza vipi kujiandaa kuacha kunyonya wakati kila nyonyo ikichomolewa unalia "mama kaa chini ninyonye". Well.. ikisitishwa labda tutapata watu wenye akili ya kuona ni vipi tutaweza kujitegemea kwa sababu hatuna 'mjomba' wa kuturushia vijihela...
Kama kweli tunapinga misaada, tuanze kwanza kulipa madeni sugu ya nje
Heshima kuu Mwanakijiji,Usaliti ni kuwa na msimamo katika ukweli; wasaliti wa demokrasia ndio wamekuwa mashujaa wenu sasa?
Kwa nini hutaki kujibu hoja zao za kusitisha huo msaada?
Kama ulikuwa na dhamira ya kujitegemea kwa nini ulikubali msaada wenyewe in the first place?
Unawezaje kuukejeli msaada wa MCC halafu kesho yake unaupokea msaada wa Japan kwa mbwembwe? Dhamira ya kujitegemea iko wapi hapo?
Huwa nawashangaa sana watz walioko marekani ,na wafananisha na mambwa majibwa; sina maana ya kutusi bali,wanaongea na kupiga kelele bila kufanya lolote,ikiwa pamoja na kuponda .Shida sio misaada, Hoja walizojenga mbona hamzungumzii???? mbona unajitoa ufahamu bure? wewe upo marekani, unaelewa maana ya kukaa na kiza mwezi mzima? acha kufurahisha genge kaka....
Tumejiandaaje kujitegemea kama sio unaongea vitu vya kufikirika? unadhani maisha ni riwaya?
Heshima kuu Mwanakijiji,
ndani ya jamvi hivi tuna uelewa tofauti nami binafsi kuna thread nashindwa kufuatilia kwa kuwa nahisi si level yangu.
Mwanakijiji ulikuwa role model wetu humu ndani lakini naona kwa sasa unaelekea kupungukiwa na uwezo wa kusimamia ukweli.
MCC wamesitisha msaada kwa Tanzania na sababu wamezitoa,ningetegemea tungejikita katika kuona sababu walizotoa MCC kuwa na sawa au wamekosea.Kwa mfano tungetetea uchaguzi wa marudio kwa vifungu vya sharia na reference kwa case zingine.Pia cybercrime tungeeleza na kufafanua kwa kina hii ingesaidia wote kuwa wamoja kama inavyokuwa kwa Myahudi anapokabiliana na Mpalestina.
Kwa uwezo wako wa kudadisi ungeweza hata kutusaidia kuhusu hili la iwe iweje SEIF hawezi kutawaka Zanzibar kwani binafsi nahisi viongozi wetu kuna jambo kubwa wanalijua kuhusu SEIF lakini hawatueleze na inatufanya tuendelee ku sympathisize na SEIF.
Mwanakijiji naamini unakumbuka Mwalimu alivyojitahidi kupingana na mashirika ya fedha ya kimataifa na naamini pia unakumbuka nchi hii ilifikia hata nguo kukosekana,ulanguzi,sukari na unga wa foleni,maduka ya RTC.Hatuna la kujifunza kweli?
Hii hoja ya 'kurudi nyumbani' ni miongoni mwa hoja muflisi. Hivi hakuna waliorudi nyumbani huko? Kwani kurudi nyumbani ndio sauti zetu zitasikika saaana? Kama mnao waliorudi nyumbani na hamkuwasikiliza na sisi wengine tukirudi tuna uhakika gani mtatusikiliza? Na nani alikuambia kurudi nyumbani ndio kuwa mzalendo sana au kuwepo Tanzania ndio uzalendo zaidi?Huwa nawashangaa sana watz walioko marekani ,na wafananisha na mambwa majibwa; sina maana ya kutusi bali,wanaongea na kupiga kelele bila kufanya lolote,ikiwa pamoja na kuponda .
Kama mnataka mabadilioko ya kweli? Basi mrudi nyumbani kubadilisha mambo sio kuponda na kujenga hoja mufilisi