Kina nani hawakupinga misaada ya kigeni kabla ili kutaka kujitegemea?

Nachukia kupewa misaada ( ingawa ukweli wake si misaada maana masharti yake mengi huwa ni ya kuikandamiza nchi husika ama huletwa kama kilainishi kabla ya kuweka miradi mbalimbali isiyo na tija kwa taifa )...

Mikopo nayo siyo mizuri sana kwa kuwa huwekewa mipaka katika matumizi yake lakini
Katika jicho jingine mikopo sio mibaya sana kama nchi itajizatiti katika kuitumia vyema ili tuwe na uwezo wa kuilipa na hii ni kupitia katika uwekezaji ambao huleta faida kama viwanda ama kilimo..

Tatizo letu kubwa huwa tunaitumia misaada aidha kwa kuyalisha matumbo ya wenye serikali yao ama kuwekeza katika vitu visivyoleta faida sana hivyo, huishia kuwa mrundikano wa madeni...

Rasilimali zisitudanganye sana kama hatuzitumii kama fursa.tuzione na tuzitumie kama fursa kwanza kwa kubadili mitazamo yetu katika uchakarikaji wetu NA hapo ndipo tutaweza kusimama wenyewe

** TANZANIA KWANZA **
 
I love this piece.. a very candid take on the whole question of American Aid.. thanks for sharing
I also like the part that the Usa ambassador is treat like any other ambassador.I am sure "they" don't like it.
 

HOJA KWANGU SI MISAADA, MIAADA NI MATOKEO. HOJA KWA NINI DEMOCRASIA INABAKWA ZANZIBAR? HII NI HOJA YETU YA NDANI TUJIBIWE AMA LAZIMA FUJO ITOKEE NDIO TUKUMBUKE?
 
Mkuu MM,
Uwezekano wa kuwa "tumerogwa"upo.

Pamoja na kuwa tunatofautiana kwa kwa namna moja au nyingine.

Niko tayari kusema, Mzee MM alisema haya enzi hizo.

Nimejirudi. "TUMEROGWA"
 
Mimi sijaelewa kitu kimoja hapa, hivi tumeamua kujitegemea kwa kukataa misaada yao ama wamesitisha misaada yao ndo tumeamua kujitegemea??
 
Kama unavyojielekeza, hizo pesa za Japan ni mkopo, sio ufadhili. Kinachogomba ni ile tabia yetu ya kupenda vya bure, bure ni ghali. Lazima tufike mahala tufanye maamuzi ya kutokupenda kuwa ombaomba.
 
Kama unavyojielekeza, hizo pesa za Japan ni mkopo, sio ufadhili. Kinachogomba ni ile tabia yetu ya kupenda vya bure, bure ni ghali. Lazima tufike mahala tufanye maamuzi ya kutokupenda kuwa ombaomba.
Lakini siyo kwa hili la kujitakia, yaani wala siyo tumeonewa au mashart tuliyopewa ni magumu, hapana. Ingekua issue ni masharti kama ushoga, naamini tungepinga wote. Kinachotajwa kuwa ni maslahi ya wachache kuleta madhara makubwa kwa watu million50
 
Lakini siyo kwa hili la kujitakia, yaani wala siyo tumeonewa au mashart tuliyopewa ni magumu, hapana. Ingekua issue ni masharti kama ushoga, naamini tungepinga wote. Kinachotajwa kuwa ni maslahi ya wachache kuleta madhara makubwa kwa watu million50
Mzee hawa watu sio wa kuwaendekeza na masharti yao yanabadilika kama kinyonga na kuna wakati hilo la ushoga litakuja kama ilivyokuwa Malawi na Uganda, sijui itakuwaje. Unakumbuka Septemba 2015 walituambiaje?
 
Demokrasia inakuwepo wakati gani?..kwa hiyo Sefu alivyosema kapata zile kura alizosema ndio demokrasia?

Sheria iko wazi, hakuna anayemtetea Seif kwa kuvunja sheria, alipaswa kukamatwa na kushitakiwa kwa kujitangaza na sio kufuta uchaguzi wote mpaka wa masheha. Ama kwa maneno mengine unataka kusema Seif alitangaza mpaka matokeo ya masheha? Mkubali mkatae ccm imetuingiza kwenye hasara kubwa na uwezo wa kupata 1trilioni kwa ajili ya maendeleo ccm haina. Nikisema hivi simaanishi naisujudia misaada la hasha, ila kiukweli msaada ule kumbuka sio mkopo, hivyo tungeweka mambo mengi sawa kuliko ccm kupata madaraka huko ZnZ. Unaweza ukaniambia kama ZnZ inaweza kuchangia 1trilioni kwenye bajeti ya nchi hii? Kwani tukitumia akili kuna shida gani ndugu zetu wa ccm, ni kwanini muifanye nchi iwe maskini kwa ajili ya nyinyi kutaka madaraka?
 
Mimi sijaelewa kitu kimoja hapa, hivi tumeamua kujitegemea kwa kukataa misaada yao ama wamesitisha misaada yao ndo tumeamua kujitegemea??

Mkuu tuliomba kwanza tukanyimwa then baada ya kunyimwa ndio tukakumbuka oh kumbe kuna kunajitegemea??!!. We are so pathetic.
 


Hata ufisadi na eti tule majani ili Ndege ya Raisi inunuliwe kutakoma ndani ya miaka miwili!
Pale hospitali ,Maji na huduma zingine kama Umeme zitatakapokuwa adimu au ya Mgawayo kama enzi ya Ujamaa umma /jamii itakua kiakili na wanene wataanza kuchomana macho vidole wenyewe kwa wenyewe na lazima kitaeleweka tu!.

Siku tutakapo anzaa kujitegemea tutafikia katika mazingira ambayo wale waliozoea ile kauli ya kusema Ndiyoooooooooooooooo imepitaaaa mjegoni Dodoma hata kwa mambo yaliyowazi ya ulaji pesa hutawasikia wakidhubutu kusema hivyo!. Itafika mahali Bungeni utashindwa kutambua nani CCM na nani Mpinzani!
 
Mzee hawa watu sio wa kuwaendekeza na masharti yao yanabadilika kama kinyonga na kuna wakati hilo la ushoga litakuja kama ilivyokuwa Malawi na Uganda, sijui itakuwaje. Unakumbuka Septemba 2015 walituambiaje?

Yaani huwa nawadharau sana watu wanaoficha ukweli wa kubaka demokrasia kwa kigezo eti cha kuogopa ushoga. Mpaka tunapozungumza hatujapitisha sheria ya ushoga lakini ni maskini wa kutupwa. Sasa si bora ushirikiane na huyo anayekubaliana na ushoga iii ufanikiwe, maana kama ni ushoga mpaka tunavyoongea upo tena wazi kabisa ila haujapitishwa kisheria tu, hakuna anayekulazimisha kuwa shoga bali ni nyege zako tu. Halafu kama ni ushoga utaletwa na hao shirika la MCC tu, mbona bado tuna ushirikiano na serekali ya marekani inayoutambua ushoga. Unafiki usio na tija tuachane nao.
 
Mkuu dharau sio uungwana, niliyemjibu amenielewa na alitaka ufafanuzi, sasa naona limekugusa (sipendi kuweka matusi!) naona wanijia juu na matusi teeele bila sababu.
 
WanaCCM tumeshaeleza wazi kuwa hatuna shida na vijimisaada vyenye masharti. Hili hata mstaafu Kikwete alilizungumza na sasa rais Dkt Magufuli anazidi kulikazia.

Kweli umenena mkuu
 
Mkuu tuliomba kwanza tukanyimwa then baada ya kunyimwa ndio tukakumbuka oh kumbe kuna kunajitegemea??!!. We are so pathetic.

Kichekesho watu wanahubiri kujitegemea wakati mpaka toothpick tunaagiza toka nje!! Ukienda kwenye vijiji vya hao wanaohubiri kujitegemea wakulima ni wachovu ile mbaya na wao hawana suluhu ya matatizo yao zaidi ya ndoto za alinacha eti TZ ya viwanda. Hivi kweli unaweza ukasimama mbele ya wanaume ukasema tutajitegemea huku umekosa 1trilion ambazo ni sawa na kutegemea ulichoshika mkononi ukaanza kuhubiri maendeleo ya viwanda ya kutafuta?
 
Demokrasia inakuwepo wakati gani?..kwa hiyo Sefu alivyosema kapata zile kura alizosema ndio demokrasia?

Kwani Seif alipotangaza kura zake, ilizuia vipi tume ya Uchaguzi ya Zanzibar kuendelea kutangaza matokeo!?
 
Watanzania ni sie kwa kujitutumua tu, hatujambo!

Yote kwa yote, hili la kukosa misaada ni kipimo kizuri kwa uongozi wa JPM.

Nimemsikia anataka kushusha upper cap ya mishahara ya watumishi wa umma kutoka 40m mpaka 15m, anaendelea kutumbua wafanyakazi hewa...etc. Ni mwanzo mzuri tu.

Tunaweza kumsadia kwa kuonesha namna bora ya kupunguza matumizi na kupanua wigo wa kodi huku akichunga kwa umakini uchumi. Asipokuwa makini hatua hizi zinaweza kuathiri sana uchumi wa nchi maana kama hakuna uzalishaji/biashara ya kutosha hata vyanzo vya kodi vitakuwa vichache.
 
Mkuu dharau sio uungwana, niliyemjibu amenielewa na alitaka ufafanuzi, sasa naona limekugusa (sipendi kuweka matusi!) naona wanijia juu na matusi teeele bila sababu.

Mkuu samahani sana kwa kukukwaza kwani hata nami ni muungwana, ila kumbuka hili ni jukwaa huru na hapa ni kwenye mjadala huru. Pindi tunapoona upotoshaji mnaufanya kwa makusudi ni lazima tukemee bila kujali utapenda ama la. Samahani kwa kukukwaza ila jirekebishe na huu upotoshaji unaoufanya wa eti ushoga sijui nini.
 
Daaah!!
Walitaka kuiba uchaguzi ukawa si wa HAKI.
Hivi mzee kama wewe unajijua hapo ulipo unaishi kwa msaada?

Rudi TZ tukae hapa tuanze kujitegemea otherwise wewe utaishia kuongeaongea tu, 'nilisema hapa angalia andiko langu hili' blah blah za uswazi.
 
Imeandikwa "Amelaaniwa binaadamu anaemtegemea binaadamu mwenzie"

leo sina maneno mengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…