Kinachoendelea Dhidi Ya Lisu Ni Mwendelezo wa Uharamia wa Wakati Wote, Sawa Walivyotendewa Waliouawawa na Waliotekwa, Lakini Hakuna Kesi.

Kinachoendelea Dhidi Ya Lisu Ni Mwendelezo wa Uharamia wa Wakati Wote, Sawa Walivyotendewa Waliouawawa na Waliotekwa, Lakini Hakuna Kesi.

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
CCM na watawala waovu wameendelea na uovu wao dhidi ya haki. Anachofanyiwa Lisu na polisi, magereza, na mahakimu, na majaji mchongo, ni mwendelezo wa uovu ule ule aliofanyiwa Ali Kibao, Mdude Nyagali, Soka na wengine wengi. Ni mwendelezo wa uovu ule aliofanyiwa Baba wa Kiroho na Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Father Kitima.

Hivi kuna mtu anaweza kusimama hadharani na kusema Ali Kibao, au Mdude au Soka walifanya kosa gani, hadi hawa mashetani kuamua kuwaua, zaidi ya ukweli kuwa waliokuwa wakosoaji wa uovu wa watawala?

Hivi kuna mtu anaweza kusimama na kusema Fr. Dr. Kitima alikuwa ana hatia yoyote ya kumfanya ashambuliwe kwa lengo la kumwua, zaidi ya kitendo chake cha kukemea kwa nguvu zote uporwaji wa bandari zetu?

Hawa watu ni waovu wanaoamua kuwanyamazisha wote wanaokemea uovu wao, wanataka wote waungane nao kwenye uzhetani wao, anayekemea basi hugeuka na kuwa adui yao. Lakini kuna faida gani kuwa rafiki wa watu waovu, kama wewe siyo mwovu? Wananchi wote wema tukubali kuwa maadui zao watawala mashetani, kwani kamwe hatutawaunga mkono kwenye uovu wao.

Yaani Lisu kusema kuwa tutakinukisha au tutafanya uasi, eti ndiyo uhaini!!

Ikumbukwe Lisu aliyasema hayo akiwa kwenye kikao cha ndani akiijibu barua ya wale waliojiita G55. Lisu alisema, "Nimeyasoma madai yao, wanasema eti tusiposhiriki uchaguzi, itakuwa ni uasi, ni kweli utakuwa ni uasi dhidi ya sheria na mifumo gandamizi inayosimamia uchaguzi. Uasi wa namna hiyo tutaufanya. Hatutashiriki uchaguzi kwa sheria hizi gandamizi, tutakinukisha, tutakinukisha kweli kweli"

Halafu kuna watu wendawazimu, wenye dhamira zao chafu, wanaamini wanaweza kuwapata watu punguani watakaoamini maneno hayo ya Lisu ndiyo ya kupindua Serikali!!
Kwa namna nchi inavyokwenda, ni lazima tukubali kuwa Taifa letu lipo kwenye laana ya kuwa chini ya watu waliojaa dhuluma, wasiopenda haki, ambao kuteka, kuua, kuumiza watu, kuwabambikia watu kesi, ndiyo nyenzo zao za kubakia madarakani. Uchaguzi unaitishwa kwa lengo la kubariki uovu wao na siyo kwaajili ya kuwapa wananchi nafasi ya kuamua nani wawaongoze.

Vita vya uhuru vilikuwa ni rahisi kuliko vita hii ya kuitafuta haki, lakini ni lazima tuipigane kikamilifu, na tuishinde. Wakati wa ukoloni, adui yetu alikuwa anajulikana na kuonekana dhahiri, LAKINI vita hii ya dhuluma dhidi ya wananchi, ni ngumu sana, kwa sababu maadui zetu wanafanana na sisi, kuanzia rangi za ngozi, na muda mwingi wanafanya hadaa kutuaminisha ni wenzetu wanaopigania maslahi yetu kumbe ni maadui wabaya kuliko wale wa wakati wa ukoloni.

Tuamke, tuuvae weledi na utu mpya. Adui ni adui tu, haijalishi ana rangi kama ya kwako, anaongea lugha kama ya kwako, anajifanya muumini kama wewe au anakurushia sehemu ya pesa anayowapora ninyi wenyewe.

Tunaomba Mungu wetu utujaze werevu na ujasiri sisi watu wako ili akili zetu zipate kutoka gizani, na kuwatambua maadui zetu wanaotutumia dhidi ya wenzetu.
 
Tumewakamata waliomshambulia Padri Kitima - RPC MULIRO
Wa kupuuzww huyo anapiga siasa mbele ya camera aonekane mtendaji ili afikiriwe kwa nafasi ya juu zaidi au apewe cheo baada ya muda wa utumishi wake kuisha (balozi, apewe cheo ndani ya ccm)​
 
Wa kupuuzww huyo anapiga siasa mbele ya camera aonekane mtendaji ili afikiriwe kwa nafasi ya juu zaidi au apewe cheo baada ya muda wa utumishi wake kuisha (balozi, apewe cheo ndani ya ccm)​

Tukumbuke kuwa kabla ya hilo shambulio, kuna ujumbe toka ikulu ulipelekwa kwa Askofu mmojawapo kuwa maaskofu wa TEC wamwondoe Fr Kitima kwenye nafasi yake ili kuwa na uhusiano mzuri na Serikali. Ndiyo maana Fr. Kitima baada ya kutoka hospitalini alisema kuwa kitendo cha tukio lile kutanguliwa na tukio jingine, tena toka ngazi ya juu, hiyo inaashiria ni nani aliagiza kushambuliwa kwake kwa nia ya kumwua.
 
CCM na watawala waovu wameendelea na uovu wao dhidi ya haki. Anachofanyiwa Lisu na polisi, magereza na mahakimu na majaji mvhongo, ni mwendelezo wa uovu ule ule aliofanyiwa Ali Kibao, Mdude Nyagali, Soka na wengine wengi. Ni mwendelezo wa uovu ule aliofanyiwa Baba wa Kiroho na Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Father Kitima.

Hivi kuna mtu anaweza kusimama hadharani na kusema Ali Kibao, au Mdude au Soka walifanya kosa gani, hadi kuwaua, zaidi ya ukweli kuwa waliokuwa wakosoaji wa uovu wa watawala?

Hivi kuna mtu anaweza kusimama na kusema Fr. Dr. Kitima alikuwa ana hatia yoyote ya kumfanya ashambuliwe kwa lengo la kumwua, zaidi ya kitendo chake cha kukemea kwa nguvu zote uporwaji wa bandari zetu?

Hawa watu ni waovu wanaoamua kuwanyamazisha wote wanaokemea uovu wao, wanataka wote waungane nao kwenye uovu wao, anayekemea basi hugeuka adui yao. Lakini kuna faida ani kuwa rafiki wa watu waovu kama wewe siyo mwovu?

Yaani Lisu kusema kuwa tutakinukisha au tutafanya uasi, eti ndiyo uhaini!!

Ikumbukwe Lisu aliyasema hayo akiwa kwenye kikao cha ndani akiijibu barua ya wale waliojiita G55. Lisu alisema, "Nimeyasoma madai yao, wanasema eti tusiposhiriki uchaguzi, itakuwa ni uasi, ni kweli utakuwa ni uasi dhidi ya sheria na mifumo gandamizi inayosimamia uchaguzi. Uasi wa namna hiyo tutaufanya. Hatutashiriki uchaguzi kwa sheria hizi gandamizi, tutakinukisha, tutakinukisha kweli kweli"

Halafu kuna watu wendawazimu, wenye dhamira zao chafu, wanaamini wanaweza kuwapata watu punguani watakaoamini maneno hayo ya Lisu ndiyo ya kupindua Serikali!!
Kwa namna nchi inavyokwenda, ni lazima tukubali kuwa Taifa letu lipo kwenye laana ya kuwa chini ya watu waliojaa dhuluma, wasiopenda haki, ambao kuteka, kuua, kuumiza watu, kuwabambikia watu kesi, ndiyo nyenzo zao za kubakia madarakani. Uchaguzi unaitishwa kwa lengo la kubariki uovu wao na siyo kwaajili ya kuwapa wananchi nafasi ya kuamua nane wawaongoze.

Vita vya uhuru vilikuwa ni rahisi kuliko vita hii ya kuitafuta haki. Kwa sababu wakati wa ukoloni, adui yetu alikuwa anajulikana na kuonekana dhahiri, LAKINI vita hii ya dhuluma dhidi ya wananchi, ni ngumu sana, kwa sababu maadui zetu wanafanana na sisi, kuanzia rangi za ngozi, na muda mwingi wanafanya hadaa kutuaminisha ni wenzetu wanaopigania maslahi yetu kumbe ni maadui wabaya kuliko wale wa wakati wa ukoloni.

Tuamke, tuuvae weledi na utu mpya. Adui ni adui tu, haijalishi ana rangi kama ya kwako, anaongea lugha kama ya kwako, anajifanya muumini kama wewe au anakurushia sehemu ya pesa anayowapora ninyi wenyewe.

Tunaomba Mungu wetu utujaze werevu sisi watu wako ili akili zetu zipate kutoka gizani, na kuwatambua maadui zetu wanaotutumia dhidi ya wenzetu.
1755604743808.png

Mashitaka ya dhuluma huwa anabariki mwenye dola, kama alifanya kwa maslahi ya taifa atajitokeza kenda kutoa ushahidi kuthibitisha maagizo yake na matokeo aliyapokea kama alivyotarajia.
 
Haki siku zote uibuka mshindi japo Uchelewa kama safari ya kobe pamoja na kua kobe ana mwendo mdogo lakini hajawai kushindwa kufika mwisho wa safari yake ni sawa na Haki
 
Tukumbuke kuwa kabla ya hilo shambulio, kuna ujumbe toka ikulu ulipelekwa kwa Askofu mmojawapo kuwa maaskofu wa TEC wamwondoe Fr Kitima kwenye nafasi yake ili kuwa na uhusiano mzuri na Serikali. Ndiyo maana Fr. Kitima baada ya kutoka hospitalini alisema kuwa kitendo cha tukio lile kutanguliwa na tukio jingine, tena toka ngazi ya juu, hiyo inaashiria ni nani aliagiza kushambuliwa kwake kwa nia ya kumwua.
Kumbe kuna ujumbe ulitumwa kabla aise watu manyang'au sana unaondoa uhai wa mtu kisa anakukosoa/anasema usichotaka kusikia kama ndivyo tuna upungufu wa viongozi maana ukiwa kiongozi kubali kukosolewa pia vinginevyo ondoka kwenye hiyo nafasi haikufai. Yaani wao wanataka wasikie mapambio juu yao tu kasoro zao hawataki kuzisikia inasikitisha sana​
 
Alienda ofisa kabisa toka Ikulu, na akatamka kuwa mama kamtuma.
 
Kwahiyo kuna mgogoro baina ya kanisa na serikali? Kama ndivyo hii haijakaa sawa hata kidgo​

Aliyetumwa hakusema moja kwa moja kama kuna mgogoro, bali alisema kuwa kama kanisa Katoliki linataka mahusiano mazuri na Serikali, limwondoe Dr Kitima kwenye nafasi ya katibu wa TEC. By implication, ina maana hakuna uhusiano mzuri au kama ulikuwepo, basi hautakuwepo kama Fr Kitima angeendelea kuwa katibu wa TEC.

Nadhani anataka kuoga mgumo wa China ya zamani, ambapo Serikali ndiyo ilikuwa inawateua au kuwathibitisha kuwa viongozi wa dini.
 
Nap
Alienda ofisa kabisa toka Ikulu, na akatamka kuwa mama kamtuma.

Aliyetumwa hakusema moja kwa moja kama kuna mgogoro, bali alisema kuwa kama kanisa Katoliki linataka mahusiano mazuri na Serikali, limwondoe Dr Kitima kwenye nafasi ya katibu wa TEC. By implication, ina maana hakuna uhusiano mzuri au kama ulikuwepo, basi hautakuwepo kama Fr Kitima angeendelea kuwa katibu wa TEC.

Nadhani anataka kuoga mgumo wa China ya zamani, ambapo Serikali ndiyo ilikuwa inawateua au kuwathibitisha kuwa viongozi wa dini.
Kukengeuka na madaraka huko KKKT wameweza kuwafanyia hayo ila kwa RC pagumu sana iko wazi hakuna mahusiano mazuri naanza kupata picha kwann vp kaamua kukaa kando awapishe wababe wanaoweza kutishia wenzao​
 
Back
Top Bottom