Kinachoendelea hapa Dar es salaam sio mgao wa maji, ni kwamba Dawasa imeshakufa

Kuonyesha walivyo hovyo na incompetent, DAWASA wametoa ratiba ya mgao wa maji ambayo wameshindwa kuitekeleza. Kumbe walikuwa hawajui hata kiasi cha maji kilichopo ku supply huo mgao wao. Halafu DAWASA na Mkuu wa Mkoa wamekaa kimya kuhusu hiyo ratiba yao ya ki.senge isiyotekelezeka. Na huyo Waziri Mkuu anaendelea na ziara zake za kijinga na micro management yake ya kufokea watu kuhusu milango isiyofunga kwenye taasisi za serikali.
 
Sasa kuna haja gani ya kuendelea kuwa Waziri usiye na meno?
Aliyemteua ndo amfukuze , hata Mimi siwez kuachia ugali wakat walioko juu yangu ndo wabovu zaidi , waanze wao na Mimi nitafata , vinginevyo labda wanifukuze Kwa mamlaka waliyo nayo
 
Duuuh. Kuna sehemu niliwahi pita miaka hiyo, kuoga ni majagi mawili tu.
Malalamiko yasiwe mengi sana toeni mawazo hao wahusika wachukue hatua gani ili tatizo la maji liishe Kwa miaka mingi baadae.
 
Unadhani ni waziri ameshindwa kazi? NO !!

Ni mfumo mzima ! Ndio maana Tz sasa imekuwa ni "HAKUNA KANTRE.." Yaani:- hakuna maji, hakuna umeme, hakuna dawa mahospitalini, hakuna vitabu mashuleni, hakuna madarasa ya kutosha, hakuna waalimu wa kutosha, hakuna mikopo ya wanachuo kwa wakati, hakuna tena wanaojali............
 

Kwenye hili nani anaupiga mwingi?
 
Jana wakazi wa Kibaha hawakulala baada ya kupata mgao wao wa maji baada ya siku 5 nzima bila hiyo huduma... Baadhi walijaza mpaka vijiko kwakuwa hawajui yakikatwa yatarudishwa lini
Mkuu angalau hao ni siku tano tu, kuna watu wiki tatu sasa hamna maji. Hapa kwangu leo imebidi niagize maji lita 2000 kwa 120,000.
 
Nchi imekosa kabisa uwajibikaji na hii imepelekea watu kutoa taarifa za uongo bila aibu.
 
Wakati huo nmeona kuna visima vya maji wakivifufua ambavyo havikutumika kwa kutoa maji miaka mingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…