Kinachoendelea hapa Dar es salaam sio mgao wa maji, ni kwamba Dawasa imeshakufa

Kinachoendelea hapa Dar es salaam sio mgao wa maji, ni kwamba Dawasa imeshakufa

Duuuh. Kuna sehemu niliwahi pita miaka hiyo, kuoga ni majagi mawili tu.
Malalamiko yasiwe mengi sana toeni mawazo hao wahusika wachukue hatua gani ili tatizo la maji liishe Kwa miaka mingi baadae.
Kuna wanaopokea mshahara kwaajili ya hili. Ya nini tuwafanyie kazi yao?
 
Laki na 20??? Hayo maji yana bluetooth??? Tabata wanatuletea kwa 20,000 liter 2000.
Najua kijana wangu atakuwa amejiongeza bei maana sipo lakini kwa maeneo yetu ni kawaida. Lita 400 huwa wanaleta kwa elfu 15 kama ikitokea yamekatika.

Tabata bei zenu rahisi kwasababu mlishazoea shida ya maji na mkawa na mifumo yenu ya kupata maji. Yale maeneo ambayo huwa dawasa ipo kila siku huwa hakuna magari ya maji mpaka tupige simu.
 
Duuuh. Kuna sehemu niliwahi pita miaka hiyo, kuoga ni majagi mawili tu.
Malalamiko yasiwe mengi sana toeni mawazo hao wahusika wachukue hatua gani ili tatizo la maji liishe Kwa miaka mingi baadae.
Unahisi hadi sasa hayo mawazo hawajapata? Leo makamu wa Raisi alikua huko
 
Kwa mara ya kwanza naomba niseme wazi tena bila kificho DAWASA na maboss zao wooote walio juu yao hawajui kazi zao, wanachofanya sio kabisa yaan haituingii akilini kabisa
 
Jana wakazi wa Kibaha hawakulala baada ya kupata mgao wao wa maji baada ya siku 5 nzima bila hiyo huduma... Baadhi walijaza mpaka vijiko kwakuwa hawajui yakikatwa yatarudishwa lini
Wangekuwa wajanja wangechimba visima vya dharura na kujaza mooo🤸
 
Unadhani ni waziri ameshindwa kazi? NO !!

Ni mfumo mzima ! Ndio maana Tz sasa imekuwa ni "HAKUNA KANTRE.." Yaani:- hakuna maji, hakuna umeme, hakuna dawa mahospitalini, hakuna vitabu mashuleni, hakuna madarasa ya kutosha, hakuna waalimu wa kutosha, hakuna mikopo ya wanachuo kwa wakati, hakuna tena wanaojali............
Aione Mh. Shaka Hamdu
 
Back
Top Bottom