Kinachoendelea hapa Dar es salaam sio mgao wa maji, ni kwamba Dawasa imeshakufa

Kinachoendelea hapa Dar es salaam sio mgao wa maji, ni kwamba Dawasa imeshakufa

Walianza kwa kusema kutakuwa na mgao wa maji na wakatoa ratiba lakini maeneo mengi ambayo nina ndugu jamaa na marafiki hapa Dar sasa ni zaidi ya wiki mbili hakuna maji.

Ni vyema sasa serikali isitishe kulipa mishahara kwa wafanyakazi wa Dawasa kwasababu huwa wanalipwa kwa kutoa huduma ambayo sasa hivi haipo.
Kuna upendeleo mkubwa kwenye suala la maji na umeme. Ninapoishi kila siku maji na umeme vipo muda wote.
 
Jana wakazi wa Kibaha hawakulala baada ya kupata mgao wao wa maji baada ya siku 5 nzima bila hiyo huduma... Baadhi walijaza mpaka vijiko kwakuwa hawajui yakikatwa yatarudishwa lini
Kibaha ipi..

Mimi nipo Madafu , huku maji na umeme vipo muda wote.
 
Sasa kibaha si ndo wako karibu na hapo ruvu .utakosaje maji?
Ila Leo nimeona watu hapo kibaha wanakimbizana na madumu ya maji ni kama vile maji hayakuwepo
 
Mkuu usalama wa maji ya visima vifupi ni kwa maji ya vijijini tu, lakini kwa mjini maji ya visima vifupi ni maji taka.
Mkuu umenichekesha sana.😂😂
Tulifundishwa shule kwamba ardhi inachuja hivyo yatakuwa ni masafi.
 
Mkuu umenichekesha sana.😂😂
Tulifundishwa shule kwamba ardhi inachuja hivyo yatakuwa ni masafi.
Kinachochujwa na udongo hapo mkuu ni ile "mboji" tu inayoweza kuonekana kwa macho makavu, lakini bacteria na micro organisms wengine wote walio"contaminate" tokea kwenye mavyoo huko hubakia.

Ukitaka kukata tamaa kwa kinyaa, kama una jamaa yako anafanyia maabara, mshirikishe kuyapima, mchotee kidogo hayo ya kisima kifupi muombe akayapime , utashangaa majibu yatayotoka, waweza kutapika.

Kama maji ya bomba yanatibiwa kwa kufuata kanuni zote, ni salama kuliko maji ya visima vifupi, hasa vya mjini.

Kama hauna njia nyingine ya kupata maji ya kunywa bali ni hayo tu ya kisima, basi usiwe mvivu wa kuyachemsha.
Tena yachemshwe kwa kupikwa haswa.
 
Hii Nchi kama tinalaana hivi,tuna mito maziwa lukuki lakini eti tinashida ya maji.Ziwa Victoria la pili kuliko yote duniani ni KM 1100 hadi Dar lakini hatuna maji.
Hii Nchi inahitaji dikiteta zaidi ya Magufuli kuiongoza ina ujinga mwingi sana.
 
Wakazi wa Dar ni kama wameshakubaliana na hii hali, ndo maana Dawasco wame relax. Nawaona wakizurura mtaani na vibajaji vyao bila wasiwasi
 
Hahaa poleni sana ndugu zangu , maziwa yapo, mito ipo, visima vipi, looh hatari sana jamani na vile vile bahari ipo
 
Hivi key performance indicators za wizara ya afya zipoje? Wangetoa taarifa Kwa kutumia KPI ingekuwa poa
 
Tujiandae tu kuchimba visima binafsi, utapata na ziada ya kuwapa majirani na ya kuchangia ngarama za umeme na pump
Visima vya aina hii vilipigwa marufuku kwa kuwekewa tozo za kutosha , na mlipishaji ni huyo hyo dawasa
 
Back
Top Bottom