Kinachoendelea hapa Dar es salaam sio mgao wa maji, ni kwamba Dawasa imeshakufa

Kinachoendelea hapa Dar es salaam sio mgao wa maji, ni kwamba Dawasa imeshakufa

Championship

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2019
Posts
5,500
Reaction score
10,616
Walianza kwa kusema kutakuwa na mgao wa maji na wakatoa ratiba lakini maeneo mengi ambayo nina ndugu jamaa na marafiki hapa Dar sasa ni zaidi ya wiki mbili hakuna maji.

Ni vyema sasa serikali isitishe kulipa mishahara kwa wafanyakazi wa Dawasa kwasababu huwa wanalipwa kwa kutoa huduma ambayo sasa hivi haipo.
 
Walianza kwa kusema kutakuwa na mgao wa maji na wakatoa ratiba lakini maeneo mengi ambayo nina ndugu jamaa na marafiki hapa Dar sasa ni zaidi ya wiki mbili hakuna maji...
Jana wakazi wa Kibaha hawakulala baada ya kupata mgao wao wa maji baada ya siku 5 nzima bila hiyo huduma... Baadhi walijaza mpaka vijiko kwakuwa hawajui yakikatwa yatarudishwa lini
 
Mfumo mbovu , hawezi sikika , ili afanye maamuzi lazima awaguse matycom mana hao ndo chanzo cha shida ya maji , hapo usipopata backup ya mkuu wa nchi ni kama unajipalia mkaa tuu, utashushwa kaburini sku si zako , best option ni kucheza na beat
Sasa kuna haja gani ya kuendelea kuwa Waziri usiye na meno?
 
Afu kuna tetesi zilianza kipindi flani eti ukiwa na kisima binafsi...kuwasambazia na kuwauzia wapendwa wananchi lazima uwe na leseni toka mamlaka husika...

Labda ndio wameamua biashara ihamie kwenye utoaji wa leseni may be mamlaka husika haipati faida zaidi ya hasara tu.
Waturuhusu basi na kuwa na vyanzo binafsi vya umeme ili watuuzie leseni za usambazaji wa huduma.
 
Back
Top Bottom