Kinachoendelea kati ya Russia na Ukraine ndo kitazaa World War III (WW3)

Kama urusi Hana hizo nguvu wamarekani wamvamie tuone basi.
 
Kwanza kinu kikubwa cha nuclear kipo chini ya warusi Kwa hiyo hawawezi kushambulia sehemu ambayo IPO Chini yake labda Ukraine washambulie hicho kinu.
Ukraine wanaweza kweli kuangamiza mali yao na wananchi wake. Watapata wapi umeme wakimtoa Russia
 
Ukraine hajamtoa jasho, sema NATO wanamtoa jasho. Ofopa mtu anapigana na mataifa zaidi ya 30 mda mmoja.
Hebu tusaidie kujibu maswali ambayo tumeuliza moja baada ya lingine ili utuelimishe zaidi.
 
Asante sana, umeeleweka.
1. Umekuwa wa kwanza kujikita kwenye hoja iliyo mezani na umeweka maoni yako vizuri ambayo imetoa majibu kwa baadhi ya maswali ya dodoso.

2. Ukipata muda tupe maoni yako kwa maswali yaliyobaki utuelimishe zaidi
 
Weka statistics tukuamini kuwa urusi kaishiwa silaha kama huna nyamaza Tu Kwa Sababu utakuwa huna tofauti na mbwatukaji.
Hebu weka jazba na ukereketwa pembeni. Nimesema personalities (personal attack) si mahala pake kwenye mada iliyopo mezani.

Hebu tupe analysis yako kwa mtiririko wa maswali tuliyohoji ili watu waone hoja yako. Tumekupa platform ili utupe maoni yako ya kichambuzi japo kwa maswali hata mawili tu
 
Ukraine hajamtoa jasho, sema NATO wanamtoa jasho. Ofopa mtu anapigana na mataifa zaidi ya 30 mda mmoja.
Nope, Urusi angekuwa kwenye vita na NATO hata wiki asingemaliza. Anga lote lingefungwa.

Kwa kifupi NATO wameona udhaifu wa Urusi wemeamua kuimaliza indirectly. Wangeamua kuwapa kila kitu Ukraine basi vita ingeshaisha asubuhi na mapema.

Wanaozijia vizuri silaha za NATO wanatambua kuwa Ukraine kapewa basic necessities tu, kikubwa sana anachopewa na intelligence.
 
1. Binafsi nimeshindwa kujua hoja yako ni nini hasa kwa kuzingatia hoja zilizopo mezani. Unaweza ukatupa maoni yako kwa kujibu maswali yetu.

2. Kwa mbali naona una hoja ya super power wa mchongo. Tupe ufafanuzi kwa nini siyo real super power kama ilivyodhaniwa, weka nyama utuelimishe zaidi.
 
Hebu fafanua vizuri. Why will be end of Putin and Putinism?
Urusi inakwenda kushindwa vita, urais wa Putin unategemea matokeo ya vita hiyo. Very likely atapinduliwa / kuuawa.

Hilo ni miongoni mwa mambo yanayowaumiza vichwa mataifa ya magharibi, Putin wanamjua vizuri, akiondokewa ghafla anaweza kuibuka kiongozi mwingine ambaye ni kichaa zaidi akaikuza vita mpaka kwenye matumizi ya silaha za nyuklia.

Ndio maana hawaipi Ukraine kila kitu, hawataki ishinde kwa kishindo na ghafla kiasi cha kuupasua uongozi wa Putin, wanataka idhoofishe Urusi mpaka ikubali majadiliano ya amani.
 
Na kwenye vita intelligence data ndio kila kitu..

So inatosha kusema NATO au mataifa 30 yanapambana na Mrusi pale Ukraine.
 
Kama nimekuelewa vizuri una maana kuwa;
1. Kwa hoja yako ni kwamba Russia hawezi kupigana na NATO na USA akashinda vita au kuitawala dunia.

2. NATO na USA wana silaha nzito kuzidi Russia.

3. NATO na USA wana military intelligence kubwa kuliko Rusia

Kwenye hoja hizi ungezipa nyama kutuelimisha zaidi ingependeza.
 
Hoja yako nimeielewa na una hoja.
1. Kwamba NATO na USA hawataki kumaliza vita hii mapema ili wamdhoofishe kwanza Russia kiuchumi na military power taratibu.

2. Kwamba, USA na NATO hawataki kumpa Ukraine silaha nzito. Ukiwa unamaanisha kuwa USA na NATO wana silaha nzito kuliko Russia.

3. Hili la Putin kupinduliwa huenda ndo maana 9/5/2023 iliitangazia dunia kuwa anataka kupinduliwa na west akiwa na maana ya USA.
 
Sio jambo geni fuatilia mkasa wa Chernobyl.

 
Hafadhali Ukrain ina serikali imejipanga.
Lakini Afghanistan imewapa kichapo marekani mpaka wamekimbia wenyewe🤣🤣
 
Kwanza kinu kikubwa cha nuclear kipo chini ya warusi Kwa hiyo hawawezi kushambulia sehemu ambayo IPO Chini yake labda Ukraine washambulie hicho kinu.

..kinu kikubwa kiko mikononi mwa Urusi na unasema kiko salama.

..je, vinu vilivyoko ktk mikono ya ukraine viko salama kiasi gani?
 
Media zinavyowachezesha mziki ni raha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…