Wananchi wengi walitegemea kuwa kampeni zikianza tushudie na kusikia kuwa watatutalia vipi kero zetu.
Mfano tulitarajia kusikia kuwa pamoja na haya mambo makubwa yanayotekelezwa na Ccm na serikali yake wao wangeweza kufanya mazuri zaidi ya hiki kinachofanywa.Mfano tulitegea tusikie kuwa sekta ya afya, elimu na miundo mbinu imeimarishwa na Ccm. Je wao wapinzani watafanya nini zaidi kuperfom zaidi ya kinachofanywa na Ccm sasa hivi?
Hii inadhihirisha wazi kuwa hawa wapinzani hawapo tayari kuchukua dola kama watawala na hawana uwezo wa kutawala bali wamezunguka kueneza chuki na vinyongo walivyonavyo mioyoni mwao. Na hili linatupa mashaka huenda wakiwa na nafasi ya kutawala hawatatekeleza kama Ccm inavyofanya na hata kama wakipata nafasi watatuibia mali zetu za umma na kunedeleza ufisadi.
Nimemsikiliza mgombea wa Chadema akiwa Mwanza anaongea kwa jazba na chuki akiwaaminisha wananchi kuwa rais Magufuli ndio alitoa amri ya yeye kupigwa risasi. Na hii ni kwa sababu alikuwa akipinga jitahada za JPM kulinda rasilimali za watanzania. Na ameyasema haya baad ya kumsikia rais na ambaye ni mkuu wa nchi kuwa anampenda na asipoteze muda kufanya kampeni,bali atulie na atapewa kikazi kidogo cha kufanya. Mimi binafsi najua JPM ni mtu wa utani na huenda alikuwa anamtania tu huyu mgombea wa Chadema.
Lakini mgombea wa Chadema wa urais ameongea maneno makali sana akionyesha dhahiri kuwa ana chuki na JPM na amethibitisha kwa wananchi kuwa JPM alitoa amri ya yeye kupigwa risasi. Hii sio picha nzuri na wala sio sula linalofaa. Mgombea wa Chadema kama anauhakika kuwa JPM alitoa amri ili ashambuliwe anatakiwa afuate taratibu za kisheria na kwa sababu yeye ni mwanasheria anafahamu fika Mahakama kuu inayo mamlaka ya kulazimisha vyombo husika vikalishughulikia suala lake.Lakini pale wananchi wanapojazana ili wasikie utawasaidia vipi kutatua kero zao alafu unabaki kueneza chuki hii haisadii chama chake wala yeye mwenyewe.
Badala yake watu watachoka hizi hadithi zake za kupigwa risasi na October ikifika wataambulia mbunge mmoja tu.
NIMEITOA JAMII FORUMS HUKO
SISI SIO WAJINGA.
Ulipochukua tu madaraka ukaanza na kubomoa nyumba zetu katika bonde la Msimbazi. Bila huruma ukatuacha tumelala nje na watoto wetu. Ulidhani tutahama mjini lakini sisi bado tupo.
SISI SIO WAJINGA.
Ulipokuwa unapanua barabara ya Ubungo - Kibaha ukabomoa nyumba zetu. Mbunge wetu Mnyika aliomba utulipe fidia ukampinga mbele yetu. Lengo lako tufe masikini lakini kwetu sisi maisha yanaendelea.
SISI SIO WAJINGA.
Hukutaka tuwaone wawakirishi wetu, wakiwakirisha matatizo yetu Bungeni. Ulisema gharama za kurusha matangazo Live ni kubwa. Lakini leo hii unatuomba tufungue TBC tukuangalie ukikata mitaa kuomba kura.
SISI SIO WAJINGA.
Baada ya kuwa tumefanya kazi kwa miaka 40 na tumebakiza miezi 3 tustaafu ukatufukuza kazi kwa kisingizio cha vyeti feki. Ulidhani tutakufa kwa njaa lakini Mungu anatupigani bado tunaishi.
SISI SIO WAJINGA.
Tulipopata tetemeko la ardhi Watanzania wenzetu walituchangia pesa nyingi lakini wajanja wakatafuna. Ulipokuja Bukoba tulidhani utatutetea wanyonge badala yake ukatusimanga na kutukumbusha majanga ya Ukimwi, MV Bukoba kwamba yote yanatupiga sisi. Sasa nasikia unakuja kuomba kura kwetu! Je, ni kweli wewe utakanyaga Bukoba?
SISI SIO WAJINGA.
Tulipokuwa tuna njaa. Njaa iliyotokana na ukame. Tukakuomba msahada wa chakula. Hii sio kwako tu, hata Serikali zilizopita zilitusaidia tulipokumbwa na ukame. Lakini ulitujibu kwa kejeli na kiburi cha hali ya juu. Eti tusikuombe chakula, Serikali haina shamba. Leo hii unakuja tena kuomba kura?
SISI SIO WAJINGA.
Tukaenda Mtwara kulima korosho. Ukatuma askari wako wakatunyang'anya korosho halafu wakadai tuwaonyeshe mashamba yetu. Mbona wanaolima Mahindi, Pamba, Mpunga, n.k. hamuwaulizi mashamba yao? Ukasema hao askari watabangua korosho kwa meno ili kila Mtanzania atapata kilo 2, lakini hatujapata mgao.
Sasa nasikia unakuja kuomba kura! Labda uishie Nangurukuru kwa sababu.
SISI SIO WAJINGA.
Tumeitumikia nchi yetu kwa bidii kubwa. Tumefanya kazi kwa uzalendo mkubwa, huku tukipokea mishahara kidogo. Leo hii tumestaafu, tupo nyumbani miaka ikikatika. Lakini hutaki kutulipa mafao yetu. Bila aibu unakuja kutuomba kura tena?
#SISI_SIO_WAJINGA.