Kinachoendelea Msumbiji, magaidi na Jeshi - Part 3

Hiyo mbinu ya Winning hearts and Mind strategy ina fanikiwa vipi wakati jamii ina fahamu matatizo yote hayo yana sabibshwa na kikundi hicho ndio maana serikali imeingia vitani kuwaondoa
Pale mwenye nyumba haaminiki; hana uwezo, mengine post na. 9 imejibu.
Ya Crystal Ventures ndio mishe za 'vijana' wanapotumwa kufanya nje ya himaya.
Vp kuna mwenye clue yoyote ya mishe za SUMA JKT?
 
Bro tulia Sisi tuendelee na story usianze habari kufukua mwandishi ni nani sijui nini yasije yakawa yale ya yoga na Dark Days SteveMollel lete sehemu ya 4
 
Baada ya kusoma makala yako mkuu maoni yangu ni haya;

kwanza nimeanza kuelewa chanzo cha hawa magaidi sababu si dini kama tunavyoaminishwa hii ni michezo michafu inayochezwa na baadhi ya serikali ili kujihakikishia wanabaki madarakani ila pia wanahodhi njia za kiuchumi.

hawa wanaoitwa magaidi kwa kisingizio cha dini ya uisilamu wanatumiwa tu kufanikisha malengo ya watu bahati mbaya dini ya uislam inajinasibu sana na vita vya kulinda imani na udhaifu huo unatumiwa vyema na hawa viongozi makatili..

nini tanzania ifanye?
kwa upande wetu tuendelee kuimalisha mifumo yetu ya ulinzi hasa ya ndani ila pia ni wakati wa sisi pia kudeal na hawa bwea wanaotuchukulia poa mimi naamini tunaweza kuwadhibiti vizuri tu kwa hali iliyopo msumbiji hakuna mwekezaji atakuja kuwekeza hapo mtwara kwenye gas yetu hii.. ila tunajua ni nani yupo behind this kwa hili ilipaswa na sisi tuwatekenye hawa wahuni hizi tabia zetu za kijamaa sometime zina tuumiza kama nchi.

leo hii wamejaa waamiaji haramu kila pembe ya nchi na kuna fununu wahamiaji kutoka nchi fulani wao wanajisogeza zaidi karibu na uongozi wanatafuta nini huko tushtuke.. naona walijaribu njia ya magaidi wakafail na wameona njia nyepesi kufikia lengo lao ni kupitia kujipenyeza kwenye uongozi tushtukeeee!

ikiwa SADC itafunga operation zake kule msumbiji na kuwaacha majeshi ya rwanda pekee tutegemee matatizo zaidi mimi naona tunazungukwa pande zote na adui huku sisi tukiwa mtu kati..

namaliza kwa kusema upande wangu naona kwa hiki kinachoendelea target kuu ni Tanzania kinachofanyika kwanza kwa sasa ni kudhoofisha mipaka yetu ambayo ilikuwa imara kwenye ulinzi wa nchi yetu.

kuna nchi inajikuta ni israel ya Africa sasa kabla tatizo halijawa kubwa na sisitunapaswa kuchukua hatu lasivyo tutakuja kushtuka tupo uchi. tutaishia kutupa taulo kwa aibu!
 
Critical insight, mkuu.
 
Thanks for this insight, brother.
 
Hatari ya ugaidi kutoka Msumbiji ni tishio kubwa kwa usalama wa Tanzania. Serikali yetu inapaswa kuchukua hatua za haraka na za makusudi ili kupunguza hatari hii, ikiwa ni pamoja na kuimarisha usalama wa mpaka, kupambana na ufadhili wa ugaidi.
Jeshi la Tanzania litaendelea kubaki huko hata pale wengine wa SADC watakapokuwa wamejiondoa.
 
Ukichunguza kwa umakini Sana utagundua kwamba yale maeneo karibia yote yenye vurugu kule Msumbiji yana historia kongwe sana kuhusiana na suala la vurugu za kisiasa, hata kabla ya Taifa hilo la Msumbiji halijapata uhuru wake kutoka kwa mkoloni wao Ureno. Kambi nyingi sana za Makundi ya kisiasa ya Wapigania Uhuru wa nchi hiyo ya Msumbiji ziliwekwa katika ukanda huo wa Kaskazini mwa nchi hiyo, maeneo ambayo hadi leo hii bado yanaendelea kukumbwa na vurugu. Makundi ya Wapigania Uhuru ya vyama vya Siasa vya FRELIMO na RENAMO vilikuwa na Kambi zao nyingi za wazi na za siri kubwa ktk maeneo hayo yenye vurugu kwa sasa. Baada ya kufanikisha suala la kuuangusha utawala wa mkoloni wao Ureno, maeneo hayo tayari yalikuwa yamevurugwa vibaya sana na vita vya ukombozi, miundombinu yote ya kujenga uchumi kama vile viwanda viliharabiwa kabisa na mapigano ya vita.
Mbaya zaidi, hata chama cha Siasa cha FRELIMO kilipofanikiwa kushika madaraka ktk nchi hiyo ya Msumbiji, haikukishirikisha Chama cha RENAMO ktk kuitawala nchi hiyo ya Msumbiji, badala yake vyama hivyo viligawanyika na kuwa vyama vinavyohasimiana, vikapigana vita tena wao kwa wao ili kugombea kupata udhibiti wa madaraka ktk nchi hiyo, hatimaye Chama cha RENAMO kilizidiwa nguvu na kushindwa vita. Chama cha FRELIMO kutokana na msaada mkubwa waliopata kutoka kwa Mwl. J. K. Nyerere na CCM yake, walifanikiwa kuhodhi na kudhibiti mamlaka na madaraka yote ya nchi hiyo ya Msumbiji, na RENAMO kikawa Chama kikuu cha Upinzani dhidi ya FRELIMO.
Mbaya zaidi tena, utawala wa FRELIMO ulikichukulia Chama cha RENAMO kama Kundi la Waasi wala siyo Chama cha Siasa, Matokeo yake Wanachama na Wapiganaji wa RENAMO wakakimbilia msituni na kuweka Kambi zao nyingi za Siri kwenye huo Upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Msumbiji.

Serikali ya Msumbiji Kama ililitelekeza kabisa kwa muda mrefu eneo hilo lililopo Kaskazini mwa nchi hiyo kwa sababu ililiona kama eneo lenye maficho ya Waasi wa RENAMO, hata huduma za kijamii zilikuwa duni sana kwenye maeneo hayo. Wananchi wengi wa upande huo wa Kaskazini mwa nchi waliona kama Serikali ya Msumbiji imewatenga na haikuwa inawajali. Serikali ilijichimbia mizizi kwenye eneo la Kusini mwa nchi hiyo ya Msumbiji na kuigawa nchi ktk mapande mawili ya Kaskazini na Kusini. Serikali hiyo ya Msumbiji ilirudi tena kwa kasi upande wa Kaskazini mwa nchi hiyo baada ya Ugunduzi wa Nishati ya Gesi kwenye maeneo hayo ya Kaskazini, hapo ndipo ukawa mwanzo mpya wa kuibuka kwa Vurugu hizi zinazoendelea hivi sasa ktk eneo hilo la Kaskazini mwa nchi hiyo ya Msumbiji.

Suala la Dini au Udini ktk vurugu hizo za huko Msumbiji linatumika tu na wahusika kama "SCAPEGOAT" ili kuweza kupata msaada wa kijeshi na wa silaha za kupigania vita.
 
Kagame tunamchukulia poa sana.
CDF kwenye hotuba yake ilitakiwa Uhamiaji waanze msako na Ikulu ianze temesha watu
Acha kuhemuka wewe, war is a big business, interest ni pesa tuu na kuyapa majeshi yake utayari, mission kama hizo askari wanalipwa big money kwa mwezi wanalipwa mpa 2000$ na serikali pia inalipwa , ila akili yako tayari unaona unavamiwa wewe unaanza msako wa waha na watu wa wako wa mipakani, akili za hovyo sana
 
Jeshi la Tanzania litaendelea kubaki huko hata pale wengine wa SADC watakapokuwa wamejiondoa.
Mimi binafsi kwa Maoni yangu ni kwamba Jeshi la Tanzania (JWTZ/TPDF) linapaswa lijiondoe kutoka huko Msumbiji, badala yake Jeshi hilo lijikite kwenye Ulinzi wa Mipaka ya nchi yetu ya Tz. Iimarishe ulinzi ktk mipaka ya Tz na Msumbiji, lisijiingize kwenye Migogoro ya ndani ya nchi ya Msumbiji na hata ktk nchi zingine zote ambazo tunapakana nazo, tuache kufanya hivyo kwa sababu kuendelea kujiingiza kwenye hiyo Migogoro ndio chanzo Cha kuhatarisha usalama wa Wananchi wa nchi hii pamoja na mali zao.
Mbaya zaidi kwenye huo Mgogoro wa huko Msumbiji ni kwamba hata baadhi ya Viongozi wakubwa wa Serikali ya Msumbiji nao wapo nyuma ya Mgogoro huo, hao Wapiganaji wa hilo Kundi la RENAMO wamekuwa wakipata taarifa zote muhimu kutoka kwa INFORMERS wao ambao wapo ndani ya Serikali ya Msumbiji.
Je, mmeshawahi kujiuliza ni kwa nini Jeshi la Serikali ya Msumbiji halikuwa na Kambi nyingi za Jeshi ktk maene hayo ya Kaskazini kwa nchi hiyo ya Msumbiji, hususani kwenye hilo Jimbo la Cabo Delgado? Kwa nini kwenye Jimbo hilo kulikuwa na kambi chache sana za Jeshi na badala yake Kambi nyingi sana za Jeshi ziliwekwa upande wa Kusini mwa nchi hiyo?? Je, mnazijua sababu????
Hata pale Kampuni za kutoka Ulaya za Uchimbaji wa Gesi zilipoenda kuchimba Gesi kule Jimboni Cabo Delgado Serikali ya Msumbiji ilizijulisha na kuziruhusu Kampuni hizo kwenda huko wakiwa na Ulinzi wao binafsi, na pia Kampuni hizo ziliruhusiwa kwenda na Jeshi lao binafsi kwa ajili ya Ulinzi wao na hatimaye Kampuni hizo Walikodi Jeshi binafsi la Kujitegemea kutoka kwa Makaburu wa Afrika ya Kusini, Je, mmeshawahi kujiuliza ni kwa nini Serikali ya Msumbiji iliamua kufanya Maamuzi 'ya ajabu' Kama hayo????
Kwa Nini Jeshi la Msumbiji halikuhusishwa kwenye ulinzi kwenye maeneo hayo yenye machimbo ya Gesi huko Cabo Delgado badala yake liliruhusiwa Jeshi binafsi la kukodishwa kutoka nchini Afrika ya Kusini??

I remind you, "No research no right to speak ", Mgogoro wa huko Msumbiji una historia ndefu, haukuibuka tu hivi hivi from nowhere.
 
Turekebishane kwa lugha ya staha tu, mkuu.
 
Nimefuatilia comments zako kwenye Uzi wa SteveMollel kuna picha naiona kwako inanitisha sana.

Vipi mnanufaika nini na ugaidi wenu?
 
Hivi mnaelewa hata mnaandika nini? Kwa sass TZ haina matatizo kwenye mipaka yao wanajeshi wapo tuu makambini sio busy, mission kama hizi wanalipwa pesa nyingi sana wanajeshi wanaokwenda na kuwapa experience ya vita na mambo mengine, acheni wajeshi wapige pesa au mnataka wawe busy kuwavua uniform za jeshi mitami na kuwatandika wanavijiji kwa utemi tuu na ulevi
 
Huyo mhuni anaandika kwa code
 
Hoja yako haina mashiko hata kidogo.
Je, unakijua kitu au sababu iliyoiponza Kenya kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi kutoka kwa Al-Shabaab???
 
Nimefuatilia comments zako kwenye Uzi wa SteveMollel kuna picha naiona kwako inanitisha sana.

Vipi mnanufaika nini na ugaidi wenu?
Unatoa comments kutokana na msukumo fulani fulani uliopo nje ya uwezo wako. Isipokuwa tambua tu kwamba Mimi Ninatoa Maoni yangu hapa nikiwa na moyo thabiti kabisa wenye nia njema kwa nchi hii ili tusije kuingia kwenye shimo ambalo hatutaweza kujinasua endapo kama tutatumbukia humo.

Aidha, Mimi siyo Mwislamu Wala sina maslahi yoyote yale huko kwenye dini hiyo ambayo inanasibishwa na hao Wapiganaji wa huko Msumbiji.
Nimetoa Maoni yangu haya nikiwa ni mtu mwenye mitizamo na fikra huru kabisa, ambapo sijaegemea upande wowote usiostahili, Bali ni kueleza ukweli na uhalisia wa mambo jinsi yalivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…