Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
Kiongozi yeyote anayedogosha msahafu wa kazi yake ya uongozi, anaibua maswali mazito sana.
Kinachoendelea sasa hivi ndani ya CCM, kisitushangaze kabisa kwa sababu tulishaonyeshwa dalili zake mapema.
Rais Samia alipoiita katiba kuwa ni kijitabu tu, alikuwa anatuambia ni jinsi gani kwake, sheria na kiongozi ya kuongoza nchi, isivyo na maana kabisa.
Mapuuzo hayo ndo yamepelekea chama chake kukiuka taratibu zake.chenyewe.
Samaki huoza kuanzia kichwani.
Mwenyekiti wa chama anaachia taratibu za chama chake zisifuatwe.
Hapo kuna mawili: [1] ni ama hazijui taratibu za chama chake, au [2] anazijua lakini hajali kuzifuata.
Yote hayo mawili ni mchepuo mbaya sana katika uongozi.
Unaongoza kusiginwa kwa taratibu za chama chako halafu unataka kuwa Rais baada ya kuidogosha katiba uliyoapa kuiheshimu!
Wewe unafaa kweli kuwa kiongozi?
Sidhani kama Rais Samia keshawahi kuisoma na kuielewa katiba ya nchi, achilia mbali ile ya CCM.