Kinachoendelea suala la tozo ya kodi ya pango kupitia LUKU za TANESCO si sawa

Huo usawa uko wapi ndugu. Kwa vile tu wewe haikuhusu?

Kwanini hiyo kodi isije per day? Au basi per month?

Kwani wizi ni nini?
Kodi ya jengo kimsingi haihusiani na umeme. Hiyo ilipaswa kulipwa hata kama jengo lako halina umeme. Kuilipa kupitia Luku ni kutafuta urahisi tu wa kulipa maana wananchi mmekuwa hamlipi kwa hiyari. Ila nakubaliana na wewe kuwa kukatwa kodi hiyo katika kipindi ambacho jengo halikuwepo hiyo ni hoja ya msingi inayohitaji ufafanuzi, given uwepo wa jengo hilo umeanza mwaka wa pili wa utekelezaji. Kama jengo limekuwepo ndani ya mwaka wa utekelezaji bila shaka anapaswa alipe kodi yote 12000 maana kodi ni ya mwaka si ya mwezi mwezi. Inalipwa kwa mwezi Ili kuleta nafuu tu.
 
Wewe ndo una kichwa kigumu. Nyie ndo wananchi wasumbufu mnaosumbua bila sababu za msingi.

Utakuwa wewe kwa sasa haikuhusu. Mbinafsi tu. Bila shaka hata Ndugai kupotea ni sawa tu kwako avune alichopanda.

Ukraine na apigwe tu! Ben Sanane, Azory, Lijenje wa kwenye viroba nk wale na wa kwao.

Mawazo ya Kimaskini kabisa!
 
Wabongo lazima mnyooke, si mmekubali kuwapa wadhalimu wawe viongozi wenu

Hii nchi itakuwa imelaaniwa. Mambo yanaendelea hivi kwa sababu ya ubinafsi wa watu kama kina Waterloo.

Kwamba haliniathiri mimi leo basi. Waachie watajiju. Si kuwa haki iko je.

Hovyo kabisa!
 

Utaratibu ni mbovu na inakuwa ni kama adhabu ya kwanini umeunganisha umeme.

Kwamba mtu akiamua kuachana na umeme wa Tanesco hii kodi inakuwa haimhusu hata kama ana jengo miaka nenda rudi.

Ila ukienda kuunganisha umeme basi wakora wanahesabu ulikuwa na jengo kuanzia Jul 1 mwaka jana bila kujali umekuwa na jengo tokea lini.

Urugaruga kama huu utatuchukua miaka mingapi kututoka yarabi sisi?
 
Umeelezea vizuri sana

Ahsante

Kuna vitu viwili hapa kwanza tuwe na fact navyo.
1. Kodi ni mwaka ila inalipwa kwa mwezi kww ajili ya unafuu hivyo kama jengo lako limewekewa umeme mwezi Juni hiyo ni ndani ya mwaka wa utekelezaji hivyo unapaswa kulipa 12k yote.
Iliwekwa kwenye umeme kwasababu ya inelastic nature ya matumizi ya umeme.

Kama unafungiwa umeme mwezi July wa mwaka wa 2 wa utekelezaji, nitakuwa kuna kosa iwapo tu watakata kuanzia July ya mwaka uliopita lakini kama wataanzia pale (July) hiyo ni sawa kwasababu kodi ni ya MWAKA si mwezi. Lipeni kodi, hata sisi tunalipa huku.
 

Ni hivi, utaratibu huu ni wa kikandamizi. Umewekwa ki devide and rule. Wametengwa entrants wapya na waliokuwapo. Kwa silika za kitanzania kila mtu anajiangalia yeye.

Haihitaji kwenda shule kujua kuwa:

1. Kutoza kodi inayoitwa ya jengo kwa sababu tu lina umeme ni fyongo.
2. Kutoza kodi hii kama fixed figure kwa mwaka bila kujali jengo hilo katika mwaka limeanza lini kuwepo nayo ni fyongo.

Suala si kulipa kodi. Mbona hata majambazi hupokonya yakatokomea kusikojulikana?
 
Thibitisha, nyumba ikiunganishwa Jun 30, 2022 ikalipa umeme 12,000/- itapata 0 units, ila ikiunganishwa Jul 1, 2022 itapata umeme wa units 11,000/-.
Mkuu official reply ya TANESCO. Ni Bora akae Tu kimya!


Angalia majibu yalivyo mepesi, Ka kavaa dera tuko foleni ya maji, bombani huko Majimatitu!
 
Mimi sio mjuzi sana wa hii kodi ya Jengo.

Swali langu ni kwamba, Kama nyumba sio ya biashara ni mtu binafsi anakaa na familia yake, bado itatakiwa kulipiwa kodi?
 
Kaa jifikirie, wewe unaona sahihi hii, kwanini msianze kumkata mtu alipoanzia kuweka umeme.Muda Fulani mtumie akili zenu angalau kidogo.Mnawafanya watu wachukie nchi yao kwa mambo kama haya.
 
Asante wao kama mawakala wa makusanyo walipaswa kuwa na majibu yalivyo competent enough,
Swali lingejibiwa kwa weledi mbona huu Uzi ungekuwa mfupi Sana!

Inaonekana anayejibu mwenyewe ka robot! Au weekend!?
 
Mnatumia kigezo kipi maana Kun
Mnatumia kigezo kipi mtu kajenga nyumba mwezi wa pili kaunga umeme utamkataje tozo ya mwaka wakati nyumba Haina mwaka

Ushauri anzeni kuhesabu kipindi mtu atakapoingiza umeme hii kuangalia mwaka wa serikali mnaumiza watu,
 
Lipeni tu na hatimaye mmezoea, Mwiguru alisema "watazoea tu" hatimaye mtoa mada umefungiwa umeme ndiyo umekuja na bandiko la malalamiko ya kupigwa.

Tanesco kawajibu hapo vizuri sana ahahahaaa, vinginevyo nendeni TRA🤭!.
😂😂😂 TRA njooni uku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…