Kinachoendelea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 2024

Mimi Nina PDF ya uchaguzi wa mwisho Yani mwaka 2019 imeelezea kuanzia cku majina ya waandishi wa wapiga kura yanavotoka, cku ya uwandikishaji pamoja na uchaguzi..

Uandikishaji mwaka 2019 ulifanyika mwezi wa kumi na uchaguzi ulifanyika mwezi wa 11

Training ilikua siku tatu na uandikishaji ulikua Ni siku saba
Maombi ya kazi umeshapeleka?
 
Ndugu wanajukwaa, natumaini mnaendelea vizuri katika harakati za hapa na pale za kujikwamua kiuchumi.
Bila kuwachosha niende moja kwa moja kwenye hoja husika:

Siku za nyuma hivi karibuni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza nafasi ya kazi ya muda mfupi kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa waandishi wasaidizi na waendeshaji wa BVR ambapo tarehe ya mwisho ya kutumia maombi ilikuwa tarehe 27/04/2024.

Baada ya hapo kumekuwa na maswali mengi watu wakiulizana kwenye mitandao ya kijamii na maswali hayo ambayo watu wamekuwa wakijiuliza yamelenga zaidi juu ya:

1. Lini majibu ama orodha ya waliochaguliwa itatoka?
2. Lini usaili / interview itafanyika?
3. Lini semina itaanza na itafanyika kwa muda gani?
4. Lini kazi yenyewe itaanza na itachukua muda gani?
5. Taarifa juu ya yote hayo yanayojiri yatapatikana kwa njia gani?

Kwa mimi binafsi nadhani kwa mlioomba hizo nafasi muwe watulivu na kwa namna mlivyopokea hayo matangazo ya kazi ndivyo mtakavyojuzwa msije mkapotoshana. Vyanzo vya kuaminika kuna Tovuti ya tume husika, ofisi za kata, vijiji/ mitaa, mkurugenzi e.t.c.

N.B kwa yule atakayekuwa wa kwanza kupata taarifa yoyote sahihi na chanzo sahihi ajulishe wenzake kupitia Uzi huu ama kama una namba zake za simu mjulishe ili asije akapitwa na fursa.

Asanteni na karibuni.
UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA Tume inatarajia kufanya uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa daftati la kudumu la wapiga kura tarehe 01 julai, 2024 mkoani kigoma na mgeni rasmi anatarajia kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, mhe. Kassim majaliwa majaliwa (MB).
 
Hivi inamaanisha hiyo julai 1 ndio tarehe ya zoezi kuanza uandikishaji nchi nzima au litaanzia Kigoma then mikoa mingine?
 
Ingia website ya tume walipost tareh y uzinduzi ila hawakusema majina yatatoka lini
Hiyo kilaa mtu anajua uzinduzi tar 1 July lakini kuhusu lini majina yanatoka hakuna anayejua ni tetesi tu kila mtu ni kama anakisia
 
Watendaji kata na wenyeviti wa Vijiji wameketi Leo kujadili majina ya waombaji, kigezo kikubwa ni kuwa wanachama wa CCM ndio wanaopewa kipaumbele zaidi, kama siyo mwanachama basi omba Sana Mungu kuweza kuvuka hicho kinyang'anyiro.
Huu ni uchochezi 😎
 
Ndugu wanajukwaa, natumaini mnaendelea vizuri katika harakati za hapa na pale za kujikwamua kiuchumi.
Bila kuwachosha niende moja kwa moja kwenye hoja husika:

Siku za nyuma hivi karibuni Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza nafasi ya kazi ya muda mfupi kwa ajili ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa waandishi wasaidizi na waendeshaji wa BVR ambapo tarehe ya mwisho ya kutumia maombi ilikuwa tarehe 27/04/2024.

Baada ya hapo kumekuwa na maswali mengi watu wakiulizana kwenye mitandao ya kijamii na maswali hayo ambayo watu wamekuwa wakijiuliza yamelenga zaidi juu ya:

1. Lini majibu ama orodha ya waliochaguliwa itatoka?
2. Lini usaili / interview itafanyika?
3. Lini semina itaanza na itafanyika kwa muda gani?
4. Lini kazi yenyewe itaanza na itachukua muda gani?
5. Taarifa juu ya yote hayo yanayojiri yatapatikana kwa njia gani?

Kwa mimi binafsi nadhani kwa mlioomba hizo nafasi muwe watulivu na kwa namna mlivyopokea hayo matangazo ya kazi ndivyo mtakavyojuzwa msije mkapotoshana. Vyanzo vya kuaminika kuna Tovuti ya tume husika, ofisi za kata, vijiji/ mitaa, mkurugenzi e.t.c.

N.B kwa yule atakayekuwa wa kwanza kupata taarifa yoyote sahihi na chanzo sahihi ajulishe wenzake kupitia Uzi huu ama kama una namba zake za simu mjulishe ili asije akapitwa na fursa.

Asanteni na karibuni.

View: https://youtu.be/RYWaQUEDlyU
 
Watendaji kata na wenyeviti wa Vijiji wameketi Leo kujadili majina ya waombaji, kigezo kikubwa ni kuwa wanachama wa CCM ndio wanaopewa kipaumbele zaidi, kama siyo mwanachama basi omba Sana Mungu kuweza kuvuka hicho kinyang'anyiro.
Hii comment unaweza jua jamaa anatania lakini huu ndo ukweli 100% japo mchungu. Kubali kataa ndoi imeenda hiyooooo
 
Back
Top Bottom