Wakati uzinduzi wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ukitarajiwa kufanyika Mkoani Kigoma, Julai Mosi, 2024 imeelezwa uboreshaji utaanza siku hiyohiyo na kuendelea katika Mikoa ya Katavi na Tabora, ikifuatiwa na Kagera na Geita
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ramadhani Kailima, amesema zoezi litaendeshwa kwa Siku saba kwenye kila kituo cha kuandikisha Wapiga Kura na wanatarajia Awamu ya Kwanza itakamilika Machi 2025 kisha Awamu ya pili itafanyika Aprili hadi Juni 2025
Ameeleza mchakato huo una lengo la kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi na kuwa uboreshaji wa Awamu ya Kwanza utafanyika kwenye mizunguko 13
Soma
Tanzania inatarajiwa kuwa na Wapiga Kura 34,746,638 watakaoandikishwa katika Daftari la Wapiga Kura
#Democracy #Kuelekea2025 #Governance #JamiiForums