Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Sophist

Platinum Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
4,486
Reaction score
3,411
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE

UTANGULIZII

1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi hawa, asilimia 60 ni wasichana.

2. Shule hii inategemea misaada ya wahisani kwa asilimia 100 amabpo aslimia 90 inatoka kwa wahisani wa Australia.

3. Shule ina usajili wa wa shirika lisilo la kiserikali na ina jumla ya shule tatu zilizosajiliwa; Shule ya msingi (Na. AR. 02/7011), Shule ya Sekondari ya Wasichana (Na. S. 5243) and shule ya sekondari ya Bweni wavulana wa O-level na mchanganyiko A-level (Na. S. 4262). Shule ilipewa tamko kuwa ni shule ya ufadhili kupitia cheti S/Na. 53.

4. Shule inatoa ajira kwa zaidi ya watanzania 300 na wageni waajiriwa nane. Zaidi ya asilimia 60 ya uongozi wa Shule ni watanzania.

5. Shule pia inawasaidia wahitimu 326 kusoma elimu ya juu kwenye vyuo vikuu na vyuo vya kati vinginevyo.

6. Tarehe 3 Novemba 2020, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliondoa kiasi cha Shilingi za Kitanzania 500,000,000 kwenye akaunti za Shule.

7. Tarehe 4 Novemba, Mwenyekiti wa Bodi wa wafadhili wa Australia (amabao ndio wanaifadhili bajeti ya mwaka ya shule kwa asilimia 90) aliandika kutujulisha kuwa Bodi haitaweza tena kutuma fedha zozote kwenye shule maana hawawezi kutoa ufadhili kulipa kodi za TRA. Badala yake wanataka kufadhili elimu tu ya wanafunzi wa Kitanzania.

8. Kwa sababu hiyo, St Jude ina uwezo mdogo sana wa kifedha na haiwezi kujiendesha kama kawaida.

9. Bajeti ya shule kwa mwaka 2020 ni Shillingi za Kitanzania 12,682,710,722. Kila mwaka, shule inarudisha bajeti nzima kwenye uchumi wa Tanzania kwa kutumia asilimia 100 ya matumizi ndani ya Nchi. Kwa ufupi jedwali linatoa picha ya matumizi kwa baadhi ya maeneo muhimu sana kama ifuatavyo:

Matumizi ya Kila Siku TZS 35,229,752
Matumizi ya Mwezi TZS 1,056,892,560
Matumizi ya Chakula kwa Mwezi TZS 74,167,771
Matumizu ya Usafiri kwa Mwezi TZS 26,133,418
Mishahara ya Wafanyakazi na kodi za msingi kwa mwezi TZS 550,674,024

10. Shule kwa sasa ina kiasi cha TZS 5,777,658.40 kilichobaki kwenye akaunti ambayo ni sawa na tone dogo la maji katika bahari kwa matumizi ya siku moja ikiwa shule ingekuwa inajiendesha kama kawaida.

11. Tarehe 10 Novemba shule ilitoa mpango wa malipo kama ilivyoombwa na Kamishana Mkuu wa TRA, kwa ajili ya kuainisha namna ambavyo deni litalipwa. Katika mpango huo, shule iliatoa uwezekano wa kuchangisha familia zenye watoto shuleni, mpango ambao ungeondoa dhana ya kwamba tunatoa elimu bure kwa asilimia 100. Hata hivyo hadi hivi leo, shule haijapokea majibu kutoka ofisi ya Kamishina wa Mapato ya Ndani ya TRA.

12. Bodi ya Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Tanzania, Bodi tatu za shule na Afisa Elimu- Arusha walikutana tarehe 13 Novemba na kwa pamoja waliamua kutoa kipaumbele kwa pesa zilizobaki kwa wanafunzi wanaotakiwa kufanya Mitihani yao ya Taifa. Wanafunzi wote ambao hawana mitihani walirudishwa nyumbani tarehe 18 Novemba.

13. Katibu Tawala na Afisa Elimu – Arusha wamekuwa wakipewa taarifa kila mara kadiri mambo yanavyokuwa.

HADI KUFIKIA TAREHE 1 DISEMBA 2020:

1. Wanafunzi wote kuanzia shule ya msingi (Na. AR. 02/7011) wapo nyumbani. Wanafunzi wa Kidato cha nne wa shule ya sekondari ya wasichana (Na. S 5243) na shule ya sekondari (Na. S 4459) wanamalizia mitihani yao ya Taifa na watarudi majumbani siku ya tarehe 8 Disemba. Wanafunzi wa kidato cha 6 kwenye shule ya sekondari (Na. S 4262) wanategemea kufanya mitihani yao ya Mock na watarudi majumbani tarehe 14 Disemba mpaka hapo watakapojulishwa.

2. Wanafuzi watakosa siku 40 za masomo kwa Muhula wa pili na Ripoti za mwisho wa Muhula hazijatolewa bado.

3. Kutokana na ukosefu wa fedha, shule inajiendesha katika upungufu mkubwa kama ilivyoainishwa hapo chini:

Hali ya KawaidaUpungufu wa kujiendesha kwa Mwezi December
Jumla ya wafanyakazi30762 wanao fanya kazi sasa, upungufu wa asilimia 80 ya uendeshwaji katika hali ya kawaida
Mishahara na malipo ya Msingi ya mweziTZS 550,674,024Wafanyakazi 199 wapo kwenye likizo bila malipo kwa sababu shule haina fedha ya kulipa mishara ya mwezi wa Disemba
Kodi za wafanyakazi (PAYE) na michango mingineTZS 163,766,559 (Oktoba) TZS 171,588,427 (November)Tumeshindwa kulipa TZS 335,354,986 ambayo ni jumla ya kodi za Oktoba na Novemba
Wafanyakazi waliopunguzwa/ Mikataba iliyoshindwa kuhuishwa0 staffWafanyakazi 101 wamepunguzwa/ kunyimwa mikataba mipya (sawa na 1/3 ya wafanyakazi wote)


4. Shule pia inaatoa misaada kwa wanafunzi 326 walio kwenye vyuo 53 ambavyo asilimia 95 vipo Tanzania. Tumeweza kulipia asilimia 5% tu (TZS 76,459,000) ya bajeti nzima ya elimu kwa wanafunzi hawa. Jumla ya bajeti kwa mwaka 2020-2021 ni TZS 1,786,671,100 ambayo inajumuisha ada, malazi, chakula, vifaa muhimu, usafiri, na vitabu. Kati ya wanafunzi hawa, wanafunzi 23 wanategemea kuhitimu shahada na astashada za Afya, mwaka 2021.

Gharama za Mwaka kwa Wanafunzi 326Malipo yalihitajika Tarehe 16 Novemba
AdaTZS 490,006,100
Fedha ya kujikimuTZS 892,425,000
MalaziTZS 293,400,000
UsafiriTZS 45,640,000
Vifaa muhimuTZS 65,200,000
Jumla ya gharama:TZS 1,786,671,100
Kiasi kilicholipwa (Asilimia 5%):TZS 76,459,000
Gharama iliyobaki ikiwa haijalipwa:TZS 1,710,212,100


5. Shule imefanikiwa kuchagua wanafunzi 340 kutoka kwenye shule za serikali kujiunga na shule zetu mnamo Januari 2021. Hata hivyo, wanafunzi hawa hawataweza kupewa ufadhili huu wa kimasomo kama hali itabakia hivi ilivyo sasa.

6. Shule ina wahitimu 116 waliomaliza Kidato cha 6 wanaojitolea kufundisha masomo mbalimbai kwa mwaka mmoja kwenye shule 34 za serikali. Wahitimu wote 116 pia wamepewa likizo bila malipo hivyo hawajaweza kupata fedha ya kujikimu ya Shillingi 170,000 kila mmoja, fedha inayowasaidia kugharimu chakula na usafiri kwa mwezi.

7. Shule imeshindwa kulipa zaidi ya watoa huduma 50 kwa mwezi wa Oktoba na Novemba 2020 kiasi cha shilingi 68,997,205.

8. Wanafunzi 90 wanaohitaji msaada zaidi ya elimu hawatapokea msaada wa mwisho wa mwaka wa chakula, sabuni na vifaa vingine vya muhimu vya nyumbani.

9. Wafanyakazi wote 101 waliopunguzwa au kunyimwa mikataba mipya wana haki ya kulipwa mishahara na marupurupu ya mwisho, lakini shule haijajua bado fedha hizi zitatoka wapi.

10. Walinzi 25 wanatakiwa kuendelea kufanya kazi ili kuhakikisha ulinzi wa shule zote tatu, hivyo kupaswa kulipwa mishahara yao, hata hivyo, shule haijajua bado fedha hizi zitatoka wapi.

11. Shule haina fedha kulipa deni linalotajwa kwakuwa haina kipato wala njia ya mapato, zaidi ya zawadi na misaada inayotolewa na wafadhili ili kuendesha shule. Wahisani hawako tayari kutoa fedha ili kulipa deni hili maana kufanya hivyo kunakinzana na sababu ya kujitolea kwao.

12. Ikitokea TRA hawatarudisha fedha waliyochukuwa na kuendelea kuidai shule kodi iliyobaki, shule haitakuwa na chaguo lingine isipokuwa kuifunga kabisa na wanafunzi wote wa vyuoni watalazimika kurudishwa nyumbani.
 

Attachments

Last edited:
Maelezo mazuri lakini yana mapungufu. Kwa kuwa wameamua kutoa malalamiko yao kwa umma maana yake wameshindwana na serikali, sasa basi, ili umma tuweze kutoa 'hukumu'ya haki ingekuwa Vema na Haki wakaainisha kodi wanazodaiwa na malimbikizo yake na Kwanini walilimbikiza.

Vinginevyo tukianza kuilaumu serikali bila kujua Hoja za pande zote mbili itakuwa tumekosa maarifa na busara
 
Nimeipitia document aliyo-upload Sophist pamoja na hukumu uliyoambatanisha wewe...

KIMSINGI, wote... St Jude na TRA wapo sahihi lakini ruling ilitakiwa kutumia busara!!

1. Hukumu imetaja wazi kwamba St. Jude School imesajiliwa kama "Company Limited by Guarantee", hapa itakuwa kukosa busara kuihukumu as a "Company Limited by Share" kwa sababu tu Kamishna wa TRA alikataa ombi lao!!

2. TRA wanasimamia hoja kwamba St Jude wanafanya biashara kwa sababu kimsingi hao watoto wanalipiwa na third part LAKINI hawaangalii lengo kuu la biashara ni nini na ikiwa lengo hilo linafikiwa na St. Jude!

Lengo KUU la biashara yoyote ni kutengeneza FAIDA na ni namna gani faida hiyo inatumika!! Company Limited by Guarantee LAZIMA ipate mapato na si ajabu kuwepo SURPLUS waliyoitaja TRA kwa mwaka 2009 na 2010... issue ni je, hiyo surpulus inaenda wapi!!!

3. Msingi mkuu wa Company by Limited Guarantee ni matumizi ya hizo gains/profits na mambo kama hayo!! Kama gains/the so-called profit inakuwa re-invested for the benefit of the company goal, hiyo huwezi kuita faida unless TRA watuambie Mwanzilishi wa Shule na baadhi ya watu walikuwa WANAGAWANA hizo gains!!!

4. Nimetafuta external source kwa bahati mbaya nikakutana na Wikipedia Source ambayo inasema, kwa mfano, shule ilianza mwaka 2002 na Wanafunzi 3, mwaka 2009 ilikuwa na wanafunzi 989 na mwaka 2011 shule ilikuwa na Wanafunzi 1300, na miongoni mwao 900 walikuwa boarding!

5. Kwa kuangalia hiyo hoja namna 4, ni kukosa busara na maarifa kung'ang'ania hoja ya SURPLUS kwa sababu shule ilikuwa bado inatanua huduma zake!! Ongezeko hilo la wanafunzi zaidi ya 300 inaonesha bado kulikuwa na ujenzi unaendelea, wakaajiriwa wafanyakazi wapya let alone kudahili wanafunzi wengine!!

Again, hoja ya SURPLUS itakuwa na mashiko endapo TRA watatuambia kwamba hiyo Surplus iliingia matumboni mwa watu na haikuwa invested for the community, jambo ambalo ndo msingi wa Company By Limited Guarantee kwamba pesa zinazopatikana as gains/profit or whatever you may call it, hazitoki nje bali zinaendelea kuhudumia jamii!!!

6. Na kampuni za aina hii zinaitwa Company by Limited Guarantee kwa sababu huwa hazina chanzo chake wenyewe bali pesa zinatoka kwa Guarantors ambao, guarantor mmoja mmoja anaweza kuchagua ana-guarantee nini... ikiwa ni kusomesha idadi fulani ya wanafunzi au kuchangia kiwango cha pesa!!

7. Hapo kwa Guarantors na Mapesa yao bado tunarudi pale pale!! Assume shule ina 1000 Guarantors ambao collectively kwa mwaka wanaingiza TZS 50 Billion wakati total expenditure ni 20B... ina maana hapo kuna 30 Billion ambazo TRA inaziita SURPLUS! Je, hiyo surplus inaenda wapi? Wanagawana au mwaka hadi mwaka wanaendelea kuongeza na/au kuboresha facilities na kuongeza wanafunzi na wanufaika wengine?!

8. Ukipitia docs iliyokuwa uploaded na mtoa mada, inaonesha hivi sasa shule ina Wanafunzi 2000 lakini ukiangalia website ya shule husika, inaonesha hivi sasa kuna wanafunzi zaidi ya 1800 wanaoedelea na masomo hapo St Jude na wanafunzi wengine takribani 300 wanafadhiliwa masomo ya elimu ya juu/post-secondary education!!!

9. Kwa maana nyingine, ikiwa hapo mwanzo nimeonesha by 2011 shule ilikuwa na wanafunzi 1300, na hivi sasa kuna Wanfunzi zaidi ya 1800 waliopo shule na wengine 300 wanaofadhiliwa masomo ya elimu ya juu/post-secondary education, ina maana tayari kuna ongezeko la wanafunzi wengine 500 + 300, na website inadai wote hao wanasomeshwa bure kwa 100% ingawaje hukumu inasema 96% ndio wanasomeshwa bure... still 4% is NEGLIGIBLE, au inawezekana hiyo 96% ilikuwa zamani na sasa ni 100% FREE!

Kama ndivyo, kumbe hata kama ingekuwa kila mwaka shule inakuwa na surplus, bado inaonesha surplus hiyo inatumika for the cause, na cause yenyewe si nyingine bali kuwasaidia watoto maskini wapate elimu na sio kugawana hiyo surplus as faida/gains!

Kutokana na hilo, hizo huwezi kuita faida unless, kwa mara nyingine kama TRA wanatuambia part of that surplus inatumika kama "shared profit" au Bodi na Wafanyakazi wanajilipa mishahara ya ajabu ajabu ili mradi tu ionekane pesa zote zinatumika for the cause....

Sijaona popote kwenye hukumu TRA waliposema suala la matumizi yanayotia shaka kutoka kweney hizo pesa!!

10. Nilienda mbali zaidi kuangalia profile ya Gemma Sisia ambae ndie founder wa hiyo St Jude School!!

Huyu ni Mu-Australia, na kutokana na kazi yake hiyo ameshapata kuwa featured kwenye media huko kwao!! Wazungu hawawezi kupeleka mambo kienyeji, na kwa maana hiyo, hata hao guarantors lazima watakuwa wana-channel michango yao through a proper and legal channel!

Nachotaka kusema ni kwamba, ingekuwa ni rahisi kuamini kwamba billions in surplus Gemma atakuwa anazirudisha kwao kwenye akaunti yake binafsi!! Kwa nchi kama Australia atatumia benki ipi kupitishia pesa za kiujanja ujanja ambazo TRA inaweza ku-conclude hiyo ndo profit yenyewe lakini Gemma anatumia shule kukwepa kulipa kodi!!!

11. Hii shule binafsi nilikuwa siifahamu kabisa, kwahiyo nikalazimika kupitia performance yake kwa miaka 5 iliyopita!

Kwa O-Level, Division I na II zinakuwa nyingi maradufu kulinganisha na Div III huku Div IV ni za kutafuta kwa tochi! Kwa miaka 5 iliyopita, mwaka iliyofanya vibaya ni ule ambao ilikuwa ya 7 kimkoa!!!!

A-Level nayo, ingawaje hapa kwa miaka 2 walikuwa na lundo la Div III lakini ni mwaka 2018 ndio wanaonekana hawakufanya vizuri sana na walishika nafasi ya 16 kimkoa lakini miaka mingine yote wanakuwa kwenye Top 10 huku wakiwa na I & II za kutosha!!

Hoja hiyo hapo juu inaeleza umuhimu wa welfare economy!! In a welfare economy, wenye busara wanaweza kukiacha kiwanda kinachozalisha mimoshi hovyo hovyo kwa sababu tu kiwanda hicho kinatoa ajira kwa maelefu ya watu! Hapo utafanya comperative advantage kati ya effect ya mimoshi na kufa kwa ajira endapo utaamua kufunga kiwanda, na ndio maana hata kwenye Project Management, watu huwa wanafanya Cost-Benefit Analysis na SIO Cost-Profit Analysis!!

Lakini kwa upande mwingine, performance hiyo ya shule inathibitisha matumizi sahihi ya raslimali kwa sababu ukiona shule inafanya vizuri, inaonesha ni namna gani hapo pesa inatumika kufikia hatua hiyo!

Nilichoona cha maana kabisa kutoka kwenye tuhuma za Jude School, ni pale hukumu inaposema St Jude's School kuna maombi waliyapeleka kwa Kamishna wa Mapato kwamba wao ni charitable org lakini yakakataliwa!

Sasa as said earlier, endapo TRA hawana ushahidi wowote wa kuonesha hizo gains zinatumika kinyume na malengo ya company by limited guarantee ambayo kimsingi ni charitable organization, basi ku-jeopardize elimu ya watoto 2000+ kwa sababu tu Kamishina hakuwakubalia maombi yao ni kukosa uelewa wa welfare economy!

Hapa tukimshauri Gemma Sisia a-file for insolvency kisha ajirudie zake Australia awaachie shule "yao" kuna wajinga watatokea watasema "tunapenda kuona serikali ikishindwa" wakati mambo mengine mnasababisha wenyewe!!

Anyway, let it be!! Gemma, popote ulipo! Huko Arusha kuna Wamasai, Wameru, Waarusha, Wachaga, Warangi, n.k! Wewe na hao watu wapi na wapi?! Kujipendekeza tu!!

Waachie akina Prishaz wenyewe wasomeshe ndugu zao!! Acha ujinga... rudi nyumbani kalee watoto wako 4 manake sie Miafrika ni Mijitu ya hivi hivi tu!!

Si bora hata ukawasaidie Wa-Aborigini huko kwenu!
 
Maelezo mazuri lakini yana mapungufu.
kwa kuwa wameamua kutoa malalamiko yao kwa umma maana yake wameshindwana na serikali,saaa basi,ili umma tuweze kutoa 'hukumu'ya haki ingekuwa Vema na Haki wakaainisha kodi wanazodaiwa na malimbikizo yake na Kwanini walilimbikiza.

Vinginevyo tukianza kuilaumu serikali bila kujua Hoja za pande zote mbili itakuwa tumekosa maarifa na busara
Busara ipi? Wakati uonevu upo wazi
 
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE

UTANGULIZII

1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi hawa, asilimia 60 ni wasichana...
Awamu hii hakuna janja janja ya kukwepa kodi, muda mnaotumia kwenye mitandao ya kijamii kutafuta huruma bora mtafute mwanasheria mzuri ili mpate haki yenu.

TRA nenda kwenye NGO watu wamejisajili kama shirika linalojiendesha kwa misaada huku ni wanatumia kivuko hicho kukwepa kodi!
 
Maelezo mazuri lakini yana mapungufu.
kwa kuwa wameamua kutoa malalamiko yao kwa umma maana yake wameshindwana na serikali,saaa basi,ili umma tuweze kutoa 'hukumu'ya haki ingekuwa Vema na Haki wakaainisha kodi wanazodaiwa na malimbikizo yake na Kwanini walilimbikiza.

Vinginevyo tukianza kuilaumu serikali bila kujua Hoja za pande zote mbili itakuwa tumekosa maarifa na busara

Sasa kodi hapo inaingiaje wakati wafadhili wameamua kusomesha watanzania sasa hiyo kodi inatokana na biashara gani inayofanyika hapo hakuna mtu yeyote anayeuziwa huduma. Au huelewi kodi ni kitu gani. Kwanini watanzania tunakuwa mazezeta kiasi hiki. Watu wamejitolea kusomesha watoto wetu bado tunashindwa kushukuru tuna matatizo gani.
 
HALI YA SASA YA SHULE YA ST. JUDE

UTANGULIZII

1. Shule ya St Jude inatoa asilimia 100 ya elimu bure na bora kwa Zaidi ya watoto 2000 kuanzia shule ya msingi, sekondari na elimu ya juu kwa familia zenye hali duni ya kiuchumi wanaoishi kwenye mikoa ya kaskazini ya Tanzania. Kati ya wanafunzi hawa, asilimia 60 ni wasichana...

Hii shule ni ya zamani sana..tangu mwaka 2007 nakumbuka..kwanini iwe leo ndio waangalie suala la kodi mlima hivyo..
 
Awamu hii hakuna janja janja ya kukwepa kodi, muda mnaotumia kwenye mitandao ya kijamii kutafuta huruma bora mtafute mwanasheria mzuri ili mpate haki yenu.
TRA nenda kwenye NGO watu wamejisajiri kama shirika linalojiendesha kwa misaada huku ni wanatumia kivuko hicho kukwepa kodi!
Unafanya biashara gani wewe kitu?
 
Back
Top Bottom