Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Kinachoikumba Shule ya Mt. Jude: TRA waliondoa 500,000,000 kwenye akaunti za Shule

Siamini kama Serikali inaweza tu kufanya uonevu wa kuwalipisha hiyo kodi bila kuchunguza,shule nyingi za private za kidini zipo business oriented Ila hujificha kupitia kivuli cha misaada wanayoitoa kwa baadhi ya wanafunzi
MimI naamini wanaweza kufanya hivyo hasa ukizingatia mzee anawachukia sana watu wa kaskazini
Inawezekana sana ingekuwa hiyo shule ipo kanda ya ziwa "kwa wapiga kura wake" isingefungwa.

Hapa ishu ni kukataa kuwavalisha wanafunzi kijani na kwenda kwenye mikutano ya kampeni ya CCM.
 
Miezi MICHACHE iliyopita taasisi FULANI ya HAKI ZA KIBINAADAMU ilizuiliwa AKAUNTI YAKE....

Hebu tafakari kwa MAWAZO CHANYA....

Isije ikawa walikuwa wanafanya MONEY LAUNDERING and other illicit activities....

Sasa isije ikawa kuna "kushahabiana" na hili la hii shule nzuri ambayo partners wetu wa Australia WANAISAIDIA ELIMU YETU....
Hauna akili..
 
Hii post nitaisoma tena kesho... Naona kuna vitu kadhaa muhimu kwa taaluma yangu
 
Maelezo mazuri lakini yana mapungufu. Kwa kuwa wameamua kutoa malalamiko yao kwa umma maana yake wameshindwana na serikali, sasa basi, ili umma tuweze kutoa 'hukumu'ya haki ingekuwa Vema na Haki wakaainisha kodi wanazodaiwa na malimbikizo yake na Kwanini walilimbikiza.

Vinginevyo tukianza kuilaumu serikali bila kujua Hoja za pande zote mbili itakuwa tumekosa maarifa na busara
Hapa kuna ujaujanja wa kukwepa kodi ya serikali kwa kisingizio cha kusomesha watoto bure na ndio maana hataki kueleza mkasa mzima, TRA sio Machizi
 
Inaelekea umekariri au kukaririshwa kauli za wanasiasa. Hii ni shule iiyoanzishwa na mama raia wa Australia kusaidia watoto maskini kupata elimu. Watoto zaidi ya 2000 wa msingi na sekondari wanasoma, kuvalishwa na kulishwa bure, bila kulipa hata senti moja, vijana zaidi ya 300 kutoka kaya hizo hizo wanalipiwa karo na stipend kusoma vyuo vikuu na vyuo vya kati bila wazazi wao kugharimia. Sasa wewe unazungumza kodi gani. Yaani wananchi wa Australia wajitolee kusomesha Watanzania kupunguzia Serikali/TRA mzigo wa kugharimia elimu halafu Serikali iwatake wahisani wanaoisaidia kugharimia elimu kulipa kodi!

Soma hiyo attachment utaelewa kinachojadiliwa. Tafadhali usikariri wa kukubali kukaririshwa.
Hakuna utaratibu kama huo katika sera za elimu ya tanzania, afuate miongozo ya elimu.
 
Ilikuwaje TRA walikanusha kuchota pesa kutoka kwenye akaunti bila idhini ya mwenye akaunti, benki husika lazima ieleze.
Kwa sasa TRA wanayo mamlaka ya kufunga akauti ya mfanyabiashara yeyote anayedaiwa na TRA wala benki haihusiki.
 
Ingekuwa vyema haya mambo yakashuhulikiwa bila kumuathiti mwanafunzi mtoto wa mtanzania maskini
 
Inasikitisha sana, 2000+ ni wanafunzi wengi sana hii inaadhiri moja kwa moja familia nyingi za watanzania na TRA na wamekosea kwenye timing n at least wangefanya hivi wakat wa likizo ili isiathiri moja kwa moja masomo ya wanafunzi waliowengi
 
Awamu hii hakuna janja janja ya kukwepa kodi, muda mnaotumia kwenye mitandao ya kijamii kutafuta huruma bora mtafute mwanasheria mzuri ili mpate haki yenu.

TRA nenda kwenye NGO watu wamejisajili kama shirika linalojiendesha kwa misaada huku ni wanatumia kivuko hicho kukwepa kodi!

Sema shule ingekuwa kanda pendwa isingefungwa.
 
TRA kuchukua pesa kuna jambo ambalo haliko sawa. Shule iweke ukweli nini kinaendelea pale shuleni, haiwezekani TRA wafumuke tu na kujitwalia pesa wana sababu nzuri tu kama sikosei, kama hazipo mleta mada pamoja na shule waende mahakamani wakawashitaki TRA. Tena watalipwa na fidia juu.
 
Back
Top Bottom