Kinachokwenda kufanyika kwenye miamala ya simu, ni Serikali kuuchukua tena uchumi sadifu wa kati kwa walala hoi kwamba hawastahili kuwa nao

Hao watu wa chini unaowasema ndio chanzo cha Serikali kutowajibika kwa wananchi. Hawa ndiyo wanakuwa watu wa kwanza kuunga mkono Serikali kwa kila kiti, hata inapowaonea watu...
Mkuu, Sio vema tuwaache wamezwe mdomoni mwa simba, hata kama kuna mahali wanamakosa, tuendelee kuwatetea mkuu
 
Kitu kigumu kabisa kwa wasomi wa Tanzania, ni kufikiri vizuri na kuona mwisho wa mawazo yao

Hizi ni kodi za hovyo kuwahi kutokea, Kuwa na simu siyo ufahari, kutuma pesa iende mahali siyo ufahari
 
Wafanye wawe masikini ili uwatawale, marehemu katusomesha huyu kaja kutuzika kabisa
 
Unategemea hilo bunge ambalo 'halikuchaguliwa' na wananchi lifanye kazi hiyo!!
Hilo la kurudi kwenye utoto, ni hoja isiyo na mashiko na kama ingewezekana kuacha kutumia simu kwa miamala basi serikali itakuwa ya kwanza kukosa mapato (kukusanya kwa cash)
 

Tatizo ni kuwa mnajali mno maslahi ya vyama. Hivi wale 19 hadi sasa ngapi zimeshafujwa?

Mkisikiaga wengine wakiambiwa hakutakikani chokochoko basi muwe mnaelewa kuwa ndiyo kama huku kudai kilicho haki.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Umeweka hoja yako kwa umakini na weledi mkubwa sana, ili dhahabu ing'ae basi lazima ipite kwenye moto mkali ..kwa hiyo ili akili za hawa masikini wenzangu wanaojiona wanyonge wakipigwa na hili rungu basi kwa wakati mwingine akili zitakaa sawa. kongratis uliejibu hoja[emoji108]
 
Mkuu, Sio vema tuwaache wamezwe mdomoni mwa simba, hata kama kuna mahali wanamakosa, tuendelee kuwatetea mkuu
Utetezi wenye nguvu ni ule wenye kuungwa mkono na umma. Utetezi mwingine wowote hauwezi kuwa na impact ya kuweza kuleta mabadiliko.

Kama watu wanaguswa na haya madhira, nina hakika ndani ya wiki moja Serikali inaondoa hizi tozo dhulumati.

Kwa mfano, wananchi tunaweza kuamua kuwa hatutatumia huduma yoyote ya fedha kupitia simu kwa wiki 1 ili kuishinikiza serikali iondoa tozo dhulumati. Halafu tukasema, kwa siku tatu, hakuna atakayepiga simu, mawasiliano yatakuwa kwa sms, whatsap. Hivi unajua watakaokuwa wa kwanza kusaliti hizo jitihada? Ni hao hao watu wa hali ya chini.

Unamsaidia mtu ambaye na yeye anaonesha kwa vitendo kuwa anahitaji kusaidiwa. Hivyo ni vrma machungu yamguse kila mtu, machungu yachochee umoja dhidi ya dhuluma ya serikali kwa wananchi wake.
 
Ni taifa la kujitolea kwa kila khali, lakini kwa bahati mbaya kabisa utasikia, Fedha zimepotea, fedha bilioni ngapi zimeibiwa sjui na nani, sijui taasisi fulani inajilipa posho ngapi kwa siku

Hii ndio inayoliza walipa kodi
Wewe ni moja ya watu humu mliojifanya hamuoni umuhimu wa katiba mpya sasa hivi unajifanya kulalamika.unalalamika nini sasa?.Wacha ukamiliwe wakazitumie wenye nchi wewe endelea kukodoa macho hadi akili zitakapokujia.
 
Wewe ni moja ya watu humu mliojifanya hamuoni umuhimu wa katiba mpya sasa hivi unajifanya kulalamika.unalalamika nini sasa?.Wacha ukamiliwe wakazitumie wenye nchi wewe endelea kukodoa macho hadi akili zitakapokujia.
Mkuu, unaushahidi?

na hata kama unaushahidi, huwezi kunilazimisha nistoe maoni yangu kisa niko kinyume na mawazo yako
 
Wewe ni moja ya watu humu mliojifanya hamuoni umuhimu wa katiba mpya sasa hivi unajifanya kulalamika.unalalamika nini sasa?.Wacha ukamiliwe wakazitumie wenye nchi wewe endelea kukodoa macho hadi akili zitakapokujia.
Na bahati mbaya sana sina akili ya kushikiwa
 
Unapigwaaa mwingi kwel kwel..alisikika malisa godlisten, tindo, babati..n.k.
JPM mtamkumbukaaa tuu..iwe isiweee..
 
Eehh..kama walishindwaa kutumia kodi za nyuma kufanya hata mambo madogo tu mfano madawati kwa wanafunzi had jpm akaja na kuliondoa hilo tatizo kwa kiwango kikubwaa unazani hata wakikata elfu sana kwa kila raia wataweza kufanya jambo zaid ya kujilipa wao na familia zao..sahau hilo halipo..barabara zitabak kama zilivyo...na kila kitu kitakuwa business as usual..
 
Kweli nimeamini nchini Ina viongozi wahuni tu,nina hasira Sana basi tu.
Magu aligusa mafisadi mkalalamika kwamba anabambika kesii..anaonea watu..sasa hv mama anawagusaa nyie wanyonge hohe hahee..sasa sijui mtafanyajeee..kaz iendeleeeeeeeeee
 
Unapigwaaa mwingi kwel kwel..alisikika malisa godlisten, tindo, babati..n.k.
JPM mtamkumbukaaa tuu..iwe isiweee..
Laki moja ukitumiwa, ukienda kutoa unakatwa jumla ya sh 6000 badala ya sh 3250, huu ni wizi kwa serikali kwa wananchi wake
 
Hivi tunatambua ata mb zilizotumia humu. Ni matumizi yasiyo yalazima?
 
JPM aliwezaje kuendesha nchi hii bila vitozo vya ajabuajabu?
 
Kumtoza abiria hiyo Kodi Kuna tofauti gani na kutoza kwenye Simu.After all ukitoza kwenye nauli pesa haitafika yote serikalini
 
Mkuu, unaushahidi?

na hata kama unaushahidi, huwezi kunilazimisha nistoe maoni yangu kisa niko kinyume na mawazo yako
Acha kuweweseka wewe.sasa hivi baada ya hili kukugusa ndio unajifanya unatoa mawazo yako.Wale wengine waliokua wanatoa mawazo yao kuhusu katiba mbona hukuona nawao walikua wanatoa mawazo yao?.au ulidhani mambo ovyo nchi hii hayatakugusa.Na usijisahaulishe maana coment zako zakubeza ziko nyingi tu.Dunia duara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…