Sijui huo uwezo wa kuzungumzia dini mbili tofauti kwenye jambo moja umeupata wapi, ni kama vile umewatisha watu wasiokoke bila kujua, au kwa kujua.
Kimsingi nakuona hauna huo uwezo, ulichojaribu kufanya hapa ni sawa na kusema Mungu huwatupa wale wanaookoka, au kubadili dini.
Kwangu nizungumzie upande wa kuokoka, maandiko yanatuambia malaika hushangilia mbinguni mtu mmoja anapookoka, hii maana yake anajiweka karibu zaidi na Mungu.
Kinachomkuta huyu mpaka aonekane kufeli maisha tofauti na mwanzo, ni majaribu kwake kuongezeka baada ya kuokoka, kwani shetani huangaika zaidi na wanaomtumikia Mungu zaidi ya wale wapenda anasa za dunia..
Anachotakiwa kufanya huyu, ni kusimama kwenye imani, akiyashinda majaribu ya shetani bila kuyumba, basi hakika atarudi katika hali yake ya zamani, au zaidi, kwani maandiko yanatuambia tumtafute kwanza yeye, na mengine tutazidishiwa.