Kinachopelekea wanaookoka au kusilimu na kuwa swala tano kufeli kimaisha

Yani nilitaka kusema hivi
 
Asilimia 99 ya ukichoandika ndiyo mafundisho ya Yesu kristo.Kuwa mkristo (mfuasi/mwanafunzi wa Yesu) unapaswa uishi Kama ulivyoandika wewe.Tena Biblia imeandika dini iliyo Bora isiyo na mawaa mbele za Mungu Ni upendo..Pia japokuwa nanena ksa lugha na kuvishika vifungu vyote,natoa zaka Kama Sina upendo nakuwa Kama upatu uvumao. Yesu hakuja na mtazamo wa kidini,Bali kumjua Mungu aketiye ndani yetu ambaye ametupa mamlaka yote

Hata siku moja aliwaambia mafarisayo na waandishi (watu wa dini/washika dini). "ole wenu nyie waandishi na mafarisayo kwa kuwa mmefanana na makaburi, kwa nje yanameremeta na kuvutia kwa malumalu na chokaa ila kwa ndani kumejaa mifupa na uchafu".

Tulio wengi tunaabudu zaidi dini kuliko kumjua Mungu aishie ndani yetu!
 
Sijui huo uwezo wa kuzungumzia dini mbili tofauti kwenye jambo moja umeupata wapi, ni kama vile umewatisha watu wasiokoke bila kujua, au kwa kujua.

Kimsingi nakuona hauna huo uwezo, ulichojaribu kufanya hapa ni sawa na kusema Mungu huwatupa wale wanaookoka, au kubadili dini.

Kwangu nizungumzie upande wa kuokoka, maandiko yanatuambia malaika hushangilia mbinguni mtu mmoja anapookoka, hii maana yake anajiweka karibu zaidi na Mungu.

Kinachomkuta huyu mpaka aonekane kufeli maisha tofauti na mwanzo, ni majaribu kwake kuongezeka baada ya kuokoka, kwani shetani huangaika zaidi na wanaomtumikia Mungu zaidi ya wale wapenda anasa za dunia..

Anachotakiwa kufanya huyu, ni kusimama kwenye imani, akiyashinda majaribu ya shetani bila kuyumba, basi hakika atarudi katika hali yake ya zamani, au zaidi, kwani maandiko yanatuambia tumtafute kwanza yeye, na mengine tutazidishiwa.
 
Jamaa yangu, haya majibu yako hayaendani na maandiko ya wakristu [kwenye biblia], labda upande wa pili.

Maandiko yanatuambia tumtumaini yeye, bila yeye hatuwezi, sasa wewe unatuaminisha hapa tunaweza wenyewe bila yeye!.
 
Mkuu,hivi wewe Ni dini gani, maana threads zako naona unahama hama sn.
**** muda unakuwaje na mtazamo wa kikristo alafu Kuna muda unakuwa na mtazamo wa kiislamu.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Huyu nahisi atakuwa muislamu, lakini anajaribu kugusa pande zote bila ya kuwa na ufahamu kuhusu upande wa pili, au ufahamu alionao ni mdogo.
 
Hapa ndio umenimaliza kabisa, unaposema Mungu kwako sijui ni yupi, ila kwangu ni Yesu Kristu, na unapodai yupo ndani yetu [bila shaka ukimaanisha sisi sote], ndio unafeli kabisa...

Yesu Kristu hayupo ndani ya kila mtu my friend, yupo ndani ya wale wanaoyajua na kuyaishi mafundisho yake pekee, kuna wengine hawajui ndio maana licha ya siku ya mwisho kumuita Bwana, tulitoa majini kwa jina lako, atawaambia ondokeni kwangu siwafahamu.
 
Jamaa yangu, haya majibu yako hayaendani na maandiko ya wakristu [kwenye biblia], labda upande wa pili.

Maandiko yanatuambia tumtumaini yeye, bila yeye hatuwezi, sasa wewe unatuaminisha hapa tunaweza wenyewe bila yeye!.

Jesus !!! U don't seems to understand. Mungu hahitaji wewe umtumainie. Mungu hajakuumba umtumainie.

Mungu amekuumba huku ndani YAKO akiwa ameweka kila kitu ambacho una kihitaji katika maisha yako.

Huhitaji kumtumainia ila kinyume chake yeye ndio anakutumainia wewe.

Anatumaini kwamba kwa nguvu na mamlaka aliyo yaweka ndani YAKO utaweza kuishi maisha YAKO na kutawala viumbe wengine walio chini YAKO...
 
Yesu hajawahi kusema mahali popote kwamba yeye ni Mungu wala mimi sijasema Yesu anaishi ndani yangu.


Nimesema nina pendezwa na baadhi ya mafundisho yake kwa sababu yana appeal with my logic.

Yesu alikuja kutufundisha kwamba kama mwanadamu ukiamini katika nguvu iliyomo ndani YAKO ( hii ni nguvu ya asili ambayo KILA mwanadamu amezaliwa nayo awe mkiristu muislamu mbudha mpagani etc ) BASI utakuwa na uwezo wa kufanya KILA kitu unacho kihitaji chini ya jua.

And this is what I am talking about. Believe in ur power

Don't get me wrong my brother
 
Mawaa👍
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…