Kinachotokea Congo ni mapinduzi ya Kijeshi, hakuna cha kuzuia hili kutokea

Kinachotokea Congo ni mapinduzi ya Kijeshi, hakuna cha kuzuia hili kutokea

Kwanini wasipiganie Full Autonomy ya Mashariki ya Kongo badala kujaribu kuibadili Nchi iliyotengenezwa na Mfalume Leopold wa Ubelgiji kama shamba lake binafsi?!

Centralisation ya kila kitu ni Kinshasa imepitwa na wakati.
 
hayo mamb kayaanzisha Tshiked au ameyakuta ? je anawezaj kuyamaliza kwenye miaka 5 tu wkt huo anapambana na vikundi almost 100 , yanayoendelea DRC soon yatatapakaa ukanda huu mzima na watakuja na story nyingine kulingana na nchi husika , huez nambia hao watutsi wameanza baguliwa mwaka 1997 ila miaka mingine yote waliishi vzr ( chini ya adui yao Mobutu ) , tuliingia kweny ukoloni hv hv , HILO NI TATIZO LA BWANA HERI SIO TATIZO LETU WAHEHE , MPK MZUNGU ANAITEKA TANGANYIKA NDIPO TUNAPATA AKILI , WATUTSI ( SIO WABANTU HAWA ) WANAPAMBANA KUTUTEKA WABANTU MDG MDG BAADA YA DRC NEXT IS TANZANIA THEN WATAKUWA STRONG KUMWAMLISHA YEYOTE UKANDA HUU WA MASHARIKI , KUSINI NA KATI YA AFRIKA , TUWE MAKINI
Kwa hiyo na wewe ndio unajenga hoja kwa kumbagua mtu mweusi kwa kigezo cha kuwa si mbantu? Na kwa kwa nini mnalazimisha Tanzania iingie kwenye huu mgogoro? Wewe una akili kuliko viongozi wanaojaribu kusuluhisha? Unadai huyo rais wa congo mgogoro kaukuta kwa nini hataki kusuluhishwa na aliowakuta? Halafu bila aibu eti wanapambana "kututeka" wewe na nani? Mbona hamuongelei viongozi hao hao wakongo wanaoingia mikataba na wazungu kuchimba madini kwa faida zao binafsi? Ukubwa wa congo ni ya kuyumbishwa na waasi kama m23? Kama wanachi wao wangekuwa wanafaidika na rasilimali za congo hakuna mtu angetia pua huko. Wakongo wangeilinda congo kwa jasho na damu!
 
Mtoto wa Mzee Museveni nae anasema anataka kwenda kuiteka Ituri daah...😁😆 Tshisekedi naona kipara kinazidi kupata moto.
 
Wakishampindua Tshisekedi itakuwa zamu ya AFC na M23 kutwangana. Malengo ya AFC na M23 yametofautiana. M23 wanataka wamegewe sehemu ya Congo wakati kina Nangaa wao wanataka madaraka kuongoza DRC nzima. Hii vita ina Part II.
Kumbe Nangaa sio m 23?
 
Afadhali wachukue nchi nzima kuliko kuigawanya drc. Suala la nchi kugawanyika wala siliafiki
 
Kuachana na propaganda zote zinazoendelea kuwa Kagame anasaidia waasi kuiharibu Congo, ukweli ni kwamba Congo is a failed state. Huu ni mwaka 2025, Congo haina mifumo yoyote ya kusaidia kuiongoza nchi.

Jeshi la Congo ni dhaifu, tumeshuhudia picha za wanajeshi wa Congo wakiwa peku, wengine hawana uniform wala vitendea kazi ambavyo kimsingi vinatakiwa kutolewa na serikali.

Congo haina barabara, umeme, maji, hospitali Wala shule hivyo hata wananchi wa Congo hawana elimu kwaiyo wakati mwingine wanawezakuoneka kama ni vichaa wasojua wanachotaka.

Tshisekedi siyo mzalendo Wala hana nia ya dhati ya kusaidia Congo kuwa taifa lenye heshima na kujiweza kiuchumi.

Kwaiyo kinachoendelea Congo ni mapinduzi ya KIJESHI maana wananchi wamewaelewa M23 kwakua serikali ipo mbali hivyo tegemeo lao ni hao wanaowaona. M23 kila wanapopita wanashangiliwa na kupewa support na wananchi.

Majeshi yetu na ushirika wa East Africa Community hamuwezi kuzuia wananchi wa Congo kuijenga upya nchi yao.

Tukae kimya, kila nchi ilinde mipaka yake, acheni M23 na raia wa Congo waijenge nchi yao, wwpeni support wale wanaotakiwa na wananchi.

Inapendeza pale Congo itakapopata Rais atakayekiwa mzalendo, ajenge mifumo ya nchi, aimarishe jeshi, ajenge barabara, shule, hospitali, na miundombinu yote Ili tushirikiane vizuri.

View attachment 3237738

Tawala na Watawala wengi Sana wa nchi za Afrika hawakubaliki Wala hawaungwi mkono na Wananchi walio wengi zaidi katika nchi zao. Tawala hizo kwanza nyingi siyo za Kidemokrasia na Wala hazijawekwa madarakani na Wananchi waliopo kwenye nchi zao, Udikteta ndiyo sababu kuu kabisa ya kuwepo kwa hali hii, that's why unaona kwenye nchi karibia zote kabisa za Afrika kuna Machafuko, Vita au vurugu zisizokoma Kati ya Watawala na Watawaliwa.
 
Tshekedi raisi wa ovyo lakini ameongea ukweli KABILA ndiyo yupo nyuma ya Hawa waasi.
Sioni tatizo kama Kabila yupo nyuma ya Uasi huo unapendelea huko DRC, Hoja ya Msingi hapa ni: Je, kuna sababu za msingi ambazo zipo nyuma ya Uasi huu? Waasi hao wanazo Hoja za msingi na hoja zenye mashiko juu ya Uasi wao?

Hivi ni kwa nini hasa Watawala walioshindwa waachwe tu hivi hivi waendelee kuihujumu nchi na Wananchi wake?

WaCongomani wana haki ya kuwakataa Watawala wao ambao hawawajibiki kwao.

"Njia pekee ambayo Wananchi wataitumia katika kuzungumza au kujadiliana na Watawala wao ambao ni Madikteta ili kufikia muafaka wenye maslahi kwa pande zote Mbili ni kwa kupitia mtutu wa bunduki."

Jefss O'Brien
 
Sioni tatizo kama Kabila yupo nyuma ya Uasi huo unapendelea huko DRC, Hoja ya Msingi hapa ni: Je, kuna sababu za msingi ambazo zipo nyuma ya Uasi huu? Waasi hao wanazo Hoja za msingi na hoja zenye mashiko juu ya Uasi wao?

Hivi ni kwa nini hasa Watawala walioshindwa waachwe tu hivi hivi waendelee kuihujumu nchi na Wananchi wake?

WaCongomani wana haki ya kuwakataa Watawala wao ambao hawawajibiki kwao.
DRC hakuna kiongozi atafanikiwa kuleta maendeleo wakati Kuna vikundi vya uasi kila siku.
Wanaofadhili vikundi (magharibi) siku wakichoka kupora maliasili DRC vikundi vyote vitakufa, amani itarejea maendeleo yataanza kuonekana taratibu.
 
DRC hakuna kiongozi atafanikiwa kuleta maendeleo wakati Kuna vikundi vya uasi kila siku.
Wanaofadhili vikundi (magharibi) siku wakichoka kupora maliasili DRC vikundi vyote vitakufa, amani itarejea maendeleo yataanza kuonekana taratibu.

Sidhani kama umefanya utafiti wa kina kuhusiana na vyanzo halisi vya kuwepo kwa tatizo hilo la vurugu na uasi usiokoma huko nchini DRC (Zaire). Vurugu na uasi nchini humo ni tatizo ambalo lilianza zamani Sana mwanzoni mwa miaka ya 1960's, siyo tatizo jipya.
Sababu kubwa ya kuwepo kwa tatizo hilo ni kuwepo kwa janga kubwa la OMBWE LA UTAWALA KATIKA NCHI HIYO, wala siyo kutokana na kuwepo kwa rasilimali nyingi kwa sababu hata kwenye nchi zinngine nako pia kuna rasilimali. Kama ni madini, hata Afrika Kusini, Tanzania, n.k. madini pia yapo.
 
Wewe upo concerned na Umwamba wa waTutsi? Je hao wanajeshi wa Tanzania wanaokufa huoni, kwa nini usijihusishe na kupinga Samia kupeleka majeshi Congo? Au awarudishe ndugu zetu wanajeshi warudi?
Swala ni kwamba wanajeshi wetu warudi nyumbani maana Congo haipo tayari kupokea msaada tunaowezakuwapa maana hamna mifumo, waijenge nchi yao kwanza maana hakuna walichojenga, watasaidiwa watakapokuwa tayari. Unaombaje moto ilihali sufuria, chakula Wala mafiga huna?
 
Mbona joseph kabila hawakumsumbua hivi
Alikaa na makundi yote wakajadili at least wakakubaliana kwa baadhi ya vitu nchi ikatulia. Na hiyo ndo kazi ya Rais, Tshesekedi ameshindwa hata kuhudhuria kikao tu cha majadiliano eti katuma mwakilishi yeye kaenda Ulaya
 
Wizi wa kura kwenye chaguzi lazima uwatese.
Umeona mbali mkuu. Kura za wananchi zinapopuuzwa, huleta uasi. Yaani watu wanasubiri mtu wa kulianzisha. Wanajeshi hawana mpango wa kupigana ni kama vile wameamua kuangusha serikali.
 
Tisekedi hana Muda mrefu atakimbia Nchi Ameshazoea kuishi Ulaya Africa haelewi
Yeye mwenyewe kazaliwa ulaya, kasomea ulaya, kakulia ulaya, hana connection yoyote na Africa ndo maana nchi yake inakufa yeye ananepa. Mikutano ya ulaya ni muhimu kwake kuliko mikutano ya kusuluhisha mgogoro nchi kwake
 
Back
Top Bottom