Kinachotokea Congo ni mapinduzi ya Kijeshi, hakuna cha kuzuia hili kutokea

Kinachotokea Congo ni mapinduzi ya Kijeshi, hakuna cha kuzuia hili kutokea

Tukae kimya, kila nchi ilinde mipaka yake, acheni M23 na raia wa Congo waijenge nchi yao, wwpeni support wale wanaotakiwa na wananchi.
Unakosea mkuu.
M23 kuna mchanganyiko mbaya zaidi ya makundi 100 makundi mengi ni wahalifu hasa wakilenga kujinufaisha na madini, wachache ni kundi linalodai kutambuliwa, angalau hawa wana haki.

M23 hata ikiipindua uongozi wa Kinshasa wataanza kugeukana wao kwa wao kwa kuvombea madaraka.
Ieleweke wazi hata m23 i hukue nchi leo utulivu hautakuwepo kamwe
 
Ndo maana Tanzania na East Africa Community haitakiwi kupeleka majeshi Kongo, let them fix their problems.
Nilishauri hivi humuhumu, jamaa akaniambia nakosea kwa sababu congo ni mshirika wa tz kibiashara (bandari), na akasema yafaa tz iinunue kesi kwa kupeleka full scale.. Matatizo ya waafrika yanatengenezwa na viongozi WAPUMBAVU wa afrika.
 
hayo mamb kayaanzisha Tshiked au ameyakuta ? je anawezaj kuyamaliza kwenye miaka 5 tu wkt huo anapambana na vikundi almost 100 , yanayoendelea DRC soon yatatapakaa ukanda huu mzima na watakuja na story nyingine kulingana na nchi husika , huez nambia hao watutsi wameanza baguliwa mwaka 1997 ila miaka mingine yote waliishi vzr ( chini ya adui yao Mobutu ) , tuliingia kweny ukoloni hv hv , HILO NI TATIZO LA BWANA HERI SIO TATIZO LETU WAHEHE , MPK MZUNGU ANAITEKA TANGANYIKA NDIPO TUNAPATA AKILI , WATUTSI ( SIO WABANTU HAWA ) WANAPAMBANA KUTUTEKA WABANTU MDG MDG BAADA YA DRC NEXT IS TANZANIA THEN WATAKUWA STRONG KUMWAMLISHA YEYOTE UKANDA HUU WA MASHARIKI , KUSINI NA KATI YA AFRIKA , TUWE MAKINI
Hilo la kuiteka haliwezekaniki Mzee Miaka elf 10
 
Tpdf should get good lesson as M23 decision to liberate the country from severe misusing of country resources under chama Cha majambazi(CCM)
 
Nilishauri hivi humuhumu, jamaa akaniambia nakosea kwa sababu congo ni mshirika wa tz kibiashara (bandari), na akasema yafaa tz iinunue kesi kwa kupeleka full scale.. Matatizo ya waafrika yanatengenezwa na viongozi WAPUMBAVU wa afrika.
Kumsaidia mhalifu na wewe pia unakuwa mhalifu pia.
Hatma ya Congo DR ipo mikononi mwa WaCongoman wenyewe.

Mambo ya ngoswe sharti aachiwe mwenyewe ngoswe.
Rais Felix Tsishekedi anapaswa aachwe apambane na hali yake.
Let him reap what he sow!
 
Nilishauri hivi humuhumu, jamaa akaniambia nakosea kwa sababu congo ni mshirika wa tz kibiashara (bandari), na akasema yafaa tz iinunue kesi kwa kupeleka full scale.. Matatizo ya waafrika yanatengenezwa na viongozi WAPUMBAVU wa afrika.
Kumsaidia mhalifu na wewe pia unakuwa sehemu ya mhalifu pia.
Hatma ya Congo DR ipo mikononi mwa WaCongoman wenyewe.

Mambo ya ngoswe sharti aachiwe mwenyewe ngoswe.
Rais Felix Tsishekedi anapaswa aachwe apambane na hali yake. Let him reap what he sow!
 
Huu uvamiz ni bora uendelee kujulkana tuu kama wa M23 dhid ya drc.
Wala watutsi na wanyarwanda wasijiingize mazima as if nawao ni sehemu ya hiyo conflict.
Maana hapo nikuchafua watutsi waishio nchi za ukanda wa Africa.
Wajifunze madhara ya ugaid kuwa connected na dini ya Uislam ujue kuna namna mambo yanakuwa sivyo ndivyo.
Maana ukiangalia jinsi watu wanavyoiona M23 utadhani wanauwezo wa kuiteza dunia nzima ila kiufupi muda ni mwamzi mzuri kikubwa tutunze kumbukumbu zetu vzuri.
 
Kuachana na propaganda zote zinazoendelea kuwa Kagame anasaidia waasi kuiharibu Congo, ukweli ni kwamba Congo is a failed state. Huu ni mwaka 2025, Congo haina mifumo yoyote ya kusaidia kuiongoza nchi.

Jeshi la Congo ni dhaifu, tumeshuhudia picha za wanajeshi wa Congo wakiwa peku, wengine hawana uniform wala vitendea kazi ambavyo kimsingi vinatakiwa kutolewa na serikali.

Congo haina barabara, umeme, maji, hospitali Wala shule hivyo hata wananchi wa Congo hawana elimu kwaiyo wakati mwingine wanawezakuoneka kama ni vichaa wasojua wanachotaka.

Tshisekedi siyo mzalendo Wala hana nia ya dhati ya kusaidia Congo kuwa taifa lenye heshima na kujiweza kiuchumi.

Kwaiyo kinachoendelea Congo ni mapinduzi ya KIJESHI maana wananchi wamewaelewa M23 kwakua serikali ipo mbali hivyo tegemeo lao ni hao wanaowaona. M23 kila wanapopita wanashangiliwa na kupewa support na wananchi.

Majeshi yetu na ushirika wa East Africa Community hamuwezi kuzuia wananchi wa Congo kuijenga upya nchi yao.

Tukae kimya, kila nchi ilinde mipaka yake, acheni M23 na raia wa Congo waijenge nchi yao, wwpeni support wale wanaotakiwa na wananchi.

Inapendeza pale Congo itakapopata Rais atakayekiwa mzalendo, ajenge mifumo ya nchi, aimarishe jeshi, ajenge barabara, shule, hospitali, na miundombinu yote Ili tushirikiane vizuri.

View attachment 3237738
tsishekedi ni mbeleji ni mpuuzi haswaa
 
Hayo madini mapya yalivyo onekana kwenye ule mlima ulio anguka nilijua kinachofuatia Congo ni vita.

Hapo tatizo ni hayo madini yao. Congo ni tajiri sana ila pia ni masikini sana. Africa tuna safari ndefu
Mlima unaanguka😳
 
Lakin wanaoisapot M23 wao waruhusiwe kwakuwa wao ni watakatifu.
Acha waikamate Congo na wao wachore ramani ya nchi yao upya, Congo hakuna mfumo na waliopo wameshindwa kujenga mifumo
 
Ina maana kuruhusu magharibi kuhusika hilo ni kosa lao ina maana mifumo yao ni dhaifu ndo maana mtu yoyote anaweza kuja from nowhere na kuanza kufadhili watu wapigane
Hayo mazingira walitengenezewa tangu wanakaribia kupata Uhuru na baada tu ya uhuru.
Unafahamu Patrice Lumumba aliuwawa na nani na Mobutu aliingiaje madarakani?
Hata Tanganyika tungetengenezewa mazingira hayo toka siku ya uhuru tungekuwa na vurugu hadi leo.
 
Dhambi ya Patrick Lumumba haitaiacha DRC salama,Mobutu alijinufaisha badala ya kujenga nchi na kuwa na jeshi imara,toka enzi Mobutu jeshi la Kongo lilikuwa halina unifom,hawalipwi mshahara walikuwa wanajilipa kwa kupora wananchi.
 
Mobutu Sese Seko alikuwa na nafasi kubwa sana ya kuliunda Jeshi la nchi hiyo ya DRC (Zaire) na kuwa Imara, lakini kwa bahati mbaya sana alilihujumu Jeshi la nchi hiyo makusudi na kulifanya lisiwe na nguvu kwa kuogopa Kupinduliwa na Jeshi. Kwamba endapo kama Jeshi lingekuwa na nguvu basi yeye Rais Mobutu angeweza kupinduliwa kwa urahisi, ndio maana unaona kwamba Mobutu mwenyewe aliamua kulihujumu Jeshi la Ulinzi wa nchi hiyo makusudi kwa kulinyima Fedha za kutosha za kuendesha shughuli za kijeshi, na Kisha alikigeuza Kikosi Maalumu Cha Kumlinda yeye Rais kuwa Kama Jeshi lingine linalojitegemea kikiwa na Mkuu wake wa Kikosi hicho ambaye ni Kama CDF kwa nchi yote wakati huo huo tayari alikuwepo CDF wa Jeshi la Ulinzi wa nchi yote.
Kumbuka kwamba Mkuu wa Kikosi Maalumu Cha Kumlinda Rais Mobutu Sese Seko alikuwa na Mamlaka kamili kama ya CDF, alikuwa hapokei Amri kutoka kwa Mkuu wa Majeshi wa nchi hiyo. Kikosi Maalumu Cha Kumlinda Rais ndicho kilikuwa kinapewa upendeleo zaidi na Rais Mobutu Sese Seko na ndio kilikuwa Kikosi kilichokuwa kinaendesha Operesheni Kali Sana ya Kuwateka Watu wengine waliokuwa Wakimkosoa Rais Mobutu.
 
Back
Top Bottom