Kinachotokea kwa Diamond Platnumz sasa hivi

Kinachotokea kwa Diamond Platnumz sasa hivi

Ngoja nikae hapa nisome uchambuzi wa wataalamu wa nyota, laana , na masuala mbali mbali yanayohusu kuporomoka kwa dimondi🐒
sit-down-go.gif
 
Mziki wa bongo Hauna Hela unakupa fame,na kukuwezesha kupata deals nyingine so mond yupo sahihi now Hana njaa ni mwendo wa business and deals mziki ni kujiburudisha tu aonekane yumo,
Yule sio mwenzetu Tena anamove kutoka kua singer to business man!
Kalagha bhaho!
 
Huwezi kukaa #1 tu kila siku

Hiyo kawaida kwa msanii

Walikuwepo the beatles, wako Jacko,kool n the gang na waliimba mziki sema miziki yao insishi na itaendelea kuishi!
Sasa mondi adumu milele kwa mziki gani au huyo konde...sana sana wanavuta muda tu

Ova
 
Na kila mitume na enzi yake..tatizo bongo tunataka Dai asishuke na akishuka utaskia laana za babake sijui ngada. The guy has been on top kwa miaka karibu 9 hata akiishiwa cha kuimba ni halali tu
Kikubwa atengeneze hela tu

Ova
 
Nilikuwa mgumu kuamini huyu mwamba anaweza potea kwenye gemu. Ila kwa hii nyimbo jamaa kazingua.
Nyimbo utadhan anaimbia chekechea
 
ajabu yake ni kwamba inakimbiza balaa huko kwa social network inakamata no moja anapiga hela.. Dogo janja aliwahi sema jamaa hata mluzi tu unatosha kwake. Nyimbo mbaya kaniangusha ila ni Diamond tutafanyajee die hard fans wake bado tunaimani nae hahaha hamna mwingine wa kumshabikia sasa.
 
Mashabiki wengi wa Diamond Platnumz aka Simba watakua sasa wanajiuliza kimetokea nini kwa msanii wao pendwa kutoa ngoma za hadhi isiyotegemewa kutoka kwake.

Hasahasa mwaka huu tukianzia nyimbo ya Kamata, Gimmie na hii sasahivi ya Unachezaje ndo kabisaa haiendan na hadhi ya msanii tunayemjua na kibao chake kikali cha Jeje.

Inaonekana sasa hivi Chibu hatilii mkazo zaidi kwenye mziki kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Mkali huyu amekua akijiingiza zaidi kwenye biashara na madili ya pesa ndefu.

All in all, itoshe pia kusema kwamba Diamond aliyeitoa bongo fleva kimataifa ni yuleyule anaepitia kipindi kibovu sasahivi kwenye mziki, ni kwamba tu hajaamua kukaa chini na kutoa kazi kali ambazo tumekua tushazizoea kutoka kwake.

Alhamisi njema.
He is above next level hata akitoa boko hawezi kulala njaa
 
Back
Top Bottom